chanzo-Tanzania daima
WABUNGE
wawili jana walitaka Bunge liahirishe shughuli zake ili lijadili migogoro
kati ya wafugaji inayoendelea nchini pamoja na malalamiko kuhusu Operesheni
Tokomeza Ufugaji Haramu na Operesheni Tokomeza Ujangili.
Wabunge
hao; Said Nkumba (Sikonge) na Kangi Lugola (Mwibara) walitaka wabunge
wajadili jambo la dharura kuhusu migogoro ya wafugaji inayoendelea nchini.
Mbali
na migogoro hiyo walitaka pia operesheni hizo zijadiliwe na wabunge kwa kuwa
kwa sasa zinatumika kuwanyanyasa wafugaji na hali inayotishia machafuko
kutokea nchini.
Alianza
kusimama Nkumba baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu na
kunukuu kanuni ya 47 (1, 2, 3) akitaka shughuli za Bunge zilizopangwa jana
ziahirishwe, ili kujadili jambo hilo la dharura kuhusu migogoro ya wafugaji.
Alisema
kwa sasa ipo migogoro ya aina tatu ambayo ni kati ya wafugaji na wakulima,
wafugaji na wawekezaji na wafugaji na wahifadhi.
“Tatizo
hili limekuwa kubwa kiasi cha kutishia uvunjifu wa amani hasa katika mikoa ya
Mbeya, Morogoro na Pwani.
“Na
zaidi operesheni mbalimbali zinazoendelea kwa sasa zimesababisha uhasama na
athari kubwa kwa wakulima na wafugaji kutokana na kupoteza mali zao, mifugo
kuuawa na kupotea na vifo vya watu,” alisema.
Kwa
upande wake, Lugola ambaye naye alilitaka Bunge kujadili migogoro hiyo,
alisema hali ya wafugaji kwa sasa ni mbaya kutokana na operesheni hizo.
“Hivi
ninavyozungumza ng’ombe 4,000 wamekamatwa kwa nguvu huko Kaliua na tayari
ng’ombe 12 wameshachambuliwa kwa ajili ya kupigwa risasi kuwashinikiza
wafugaji walipe sh 180,000 kwa kila ng’ombe.
“Tusipojadili
jambo hili mnada utaendeshwa na ng’ombe 4,000 watauzwa, ng’ombe wengine
wanatumbukizwa kwenye madimbwi. Tatizo hili lisiposhughulikiwa litaleta
machafuko makubwa hasa pembezoni mwa Serengeti,” alisema.
Hoja za
wabunge wote hao ziliungwa mkono na wabunge.
Hata
hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema kikanuni hoja hizo hazitakiwi
kuungwa mkono.
“Hoja
zote ni nzito haziwezi kudharauliwa, naiagiza serikali ikafanyie kazi jambo
hili na ilete taarifa bungeni katika mkutano huu,” alisema.
|
Thursday, October 31, 2013
Migogoro ya wafugaji yatikisa Bunge
Mawaziri wajadili mgogoro wa wakulima, wafugaji
Na Sharon
Sauwa, Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013
Kwa ufupi
Alisema wafugaji hao wamekuwa wakitozwa faini kubwa na kujeruhiwa katika
operesheni hiyo ambayo imekuwa haina masilahi kwa wafugaji.
Dodoma. Mawaziri watano wamekutana mjini hapa kujadili malalamiko ya wafugaji
kuhusiana na operesheni tokomeza inayolenga kupambana na majangili.
Mawaziri hao ni Mambo ya Ndani, Maliasili na Utalii, Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa. Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdurhaman Kinana, alipokuwa
akizungumza na wawakilishi wa wafugaji.
“Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alikutana na wawakilishi wa wafugaji
kutoka katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga, “alisema. Wafugaji hao walifika kwa
Kinana ili awaite mawaziri wanaohusika waweze kuwaeleza malalamiko yao na
kuyatafutia ufumbuzi.
Awali, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), alisema
wafugaji wamekuwa wakinyanyaswa katika operesheni hiyo.
“Naomba uwaambie Wabunge wa CCM waisisitize Serikali kusitisha
operesheni hii ambayo imekuwa ikitokomeza mifugo na maisha ya wafugaji,”alisema
Kinana.
Alisema wafugaji hao wamekuwa wakitozwa faini kubwa na kujeruhiwa katika
operesheni hiyo ambayo imekuwa haina masilahi kwa wafugaji.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel
Nchimbi alisema wakati Serikali ikiendelea kuchukua hatua za kuondoa malalamiko
hayo, wafugaji wahakikishe kuwa hawachungi katika mashamba ya wakulima.
TAHARIRI-TANZANIA DAIMA -Watawala wanawalinda majangili
JANA
vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini viliandika kuhusu madai ya wabunge
kutaka kuwafichua mapapa wa ujangili.
Madai
hayo yaliibuliwa siku ya kwanza ya mkutano wa 13 wa Bunge unaoendelea sasa
mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kuituhumu
serikali kwa kutoa hoja nyepesi bungeni.
Mbunge
huyo alikuwa akitaka kujua hatua iliyofikiwa na serikali kwenye uendeshaji wa
Operesheni Tokomeza Ujangili inayofanyika kwenye mbuga zote nchini.
Mbunge
alilaani namna operesheni hiyo inavyoendeshwa kwa kukiuka haki za binadamu
kwa sababu watu wasio majangili wanakamatwa, kuteswa na kuharibiwa mali zao
ilhali majangili wanaojulikana wakiachwa waendelee na uhalifu wao.
Wakati
mbunge huyo akilalama, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi
Vuai Nahodha, aliwatuhumu wabunge na wanasiasa wengine kwa kuingilia utendaji
wa operesheni hiyo kwa kuwatetea wanaokamatwa kwa tuhuma za ujangili.
Kauli
ya Waziri Nahodha, ililenga kumpiga kijembe Waziri mwenzie wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, ambaye hivi karibuni,
msaidizi wake (ofisi ya ubunge) alikamatwa mkoani Iringa kwa tuhuma za
ujangili.
Hoja ya
Lugola ni kuitaka serikali kuhakikisha wanakata mizizi ya ujangili kwa kuwa
biashara hiyo inafanywa na matajiri wakubwa wenye ushawishi kwa watawala
ndani na nje ya nchi.
Tunaunga
mkono hoja hiyo kwa maana ya kuitaka serikali kuacha kukamata ‘vidagaa’ wa
ujangili huku ‘mapapa’ yakifumbiwa macho.
Tanzania
Daima tunafahamu kwamba ujangili, hasa wa tembo na bidhaa zake unatishia
ustawi wa wanyama hao.
Takwimu
zinaonyesha kwamba kila siku tembo 30 wanauawa kwenye hifadhi mbalimbali
nchini. Hiyo ni dalili kwamba katika kipindi cha miaka isiyozidi 10 Tanzania
itakuwa na hifadhi zisizo na tembo.
Katika
hili tunaitaka serikali kuchukua hatua makini bila kutizamana machoni, licha
ya ukweli kwamba utekelezaji wa operesheni hiyo utawaacha wahusika, sababu ni
biashara inayofanywa na matajiri wakubwa wenye uswahiba na watawala.
Tunaishangaa
serikali kwa kuendelea kuwaacha kazini makamanda wa polisi wanaopakana na
hifadhi mbalimbali. Hao lazima wawe watuhumiwa wa kwanza wa ujangili kabla ya
kwenda kuwakamata wanavijiji wanaoingia mbugani kutafuta kitoweo.
Mara
kadhaa makamanda hao wamehusishwa ama wakiwalinda majangili na kuwavusha
mipakani au kwa kutumia magari ya serikali kufanya uwindaji haramu.
Si
hivyo tu, makamanda hao wanatuhumiwa pia kuvuruga ushahidi na wakati mwingine
kuwatorosha watuhumiwa wa ujangili jambo linalokwamisha utendaji wa mahakimu
wanaosikiliza kesi za ujangili.
Kuwakamata
makamanda hao inashindikana kwa sababu waliowaweka ndiyo wanaowatuma
kuwalinda majangili wanaoua wanyamapori wetu.
Dhamira
ya kweli ikiwepo, ikasukumwa na utashi wa kisiasa kisha wananchi wakaelezwa
athari za kuua wananyama pori hao, tunaamini mitaji ya mapapa wa ujangili
itapungua kwa kiasi kikubwa.
|
chambuzi- Operesheni dhidi ya ujangili iungwe mkono
Na Mwananchi
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Oktoba31 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Ni kweli, operesheni hiyo inatakiwa
isiwe ya mateso, unyanyasaji, ukatili wala fursa ya ulipaji wa visasi, bali
inatakiwa kuendeshwa kwa umakini, weledi na haki ili kuhakikisha kila mmoja
anatendewa kadri ya matendo yake.
Kwa wiki kadhaa hapa nchini
inaendeshwa operesheni ya kupambana na ujangili wa tembo na wanyama wengine
chini ya kikosi maalumu kinachoundwa na maofisa kutoka katika vyombo vya dola,
maarufu kwa jina la Operesheni Tokomeza.
Taarifa mbalimbali zimekuwa
zikiripotiwa kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya kikosi hiki, ikiwamo watu
mbalimbali kukamatwa wakidaiwa kuhusika na ujangili, hasa wa meno ya tembo,
uhalifu ambao kwa siku za karibuni umeichafua sana nchi yetu kimataifa.
Watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa
umma na wa kisiasa wamekamatwa katika maeneo ya Serengeti, Ngorongoro, Arusha,
Ruaha, Iringa, Mahenge, Maswa, Meatu na kwingineko ambako pia, ushahidi wa aina
tofauti umepatikana kuhusiana na vitendo vya ujangili.
Kukamatwa kwa watuhumiwa katika
maeneo yote hayo ni ushahidi kwamba majangili wana mtandao mpana unaotumia
nguvu za kifedha, kisiasa au za ulinzi wa dola kujiimarisha katika maeneo mengi
ya nchi, na kuendelea kuhujumu maliasili za taifa.
Hata hivyo, pamoja na lengo zuri la
operesheni hiyo, yapo madai ya kikosi hicho kutumia mabavu na ukiukwaji wa haki
za binadamu, ikiwamo kupiga watu ovyo, kujeruhi na hata kuua watu kadhaa
wanaotuhumiwa kujihusisha na ujangili.
Pamoja na kwamba malalamiko dhidi ya
operesheni hiyo yanatakiwa kushughulikiwa na ukiukwaji huo wa haki za binadamu
kukomeshwa, madai hayo yanatakiwa kutazamwa kwa umakini kulingana na unyeti wa
tukio na mazingira yake.
Ni kweli, operesheni hiyo inatakiwa
isiwe ya mateso, unyanyasaji, ukatili wala fursa ya ulipaji wa visasi, bali
inatakiwa kuendeshwa kwa umakini, weledi na haki ili kuhakikisha kila mmoja
anatendewa kadri ya matendo yake.
Tunatambua kuwa operesheni yoyote
inayowahusisha watu wazito inakuwa na changamoto na vikwazo vingi, hali
inayowasukuma hata wabunge kuanza kushinikiza Serikali kutoa orodha ya vigogo
wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ujangili.
Kwa mujibu wa madai ya wabunge hao na
taarifa za vyombo vya habari, biashara hiyo haramu inawahusisha baadhi ya
wabunge, mawaziri, watumishi wa Serikali na maofisa katika vyombo vya dola.
Jeshi la Polisi limetajwa kuongoza
miongoni mwa makundi manne ya majeshi, ambayo watumishi wake wamekamatwa
wakijihusisha na ujangili katika matukio saba ya ujangili. Wengine ni kutoka
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na
Magereza.
Mathalan, kwa jinsi tatizo hilo
lilivyo kubwa, katika matukio ya karibuni yaliyohusisha maofisa wa vyombo vya
dola, jumla ya meno ya tembo 686 yaliyotokana na kuuawa kwa tembo 343
yalikamatwa, na vipande vingine 447 vilipatikana.
Kwenye operesheni ya namna hii ambayo
Serikali imekiri kuwapo fununu za wanasiasa kuwa miongoni mwa majangili, ni
lazima kuwepo vikwazo na shinikizo la kuizuia au kukwamisha, kwa vitisho au
malalamiko ya umma kutoka kila kona ili kuhakikisha operesheni husika
haifanikiwi.
Kutokana na hali hiyo,
tunaunga mkono kauli ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai
Nahodha aliyoitia juzi bungeni akiwataka wanasiasa kuacha kushikiza kwa kutumia
nguvu zao za kisiasa, kusitishwa kwa operesheni hiyo kwa sababu yoyote, kwa
kuwa tunaamini shughuli kama hii haiwezi kufanikiwa iwapo itaendeshwa kama
lelemama.
Wednesday, October 30, 2013
ASKARI AKUTWA NA RISASI ,MAPANGA NA NYAMA PORI NYUMBANI
SIKU chache baada ya askari
polisi wa idara ya upelelezi wilaya ya Serengeti wakiwa na raia wawili
wakishirikiana kuuza jino la tembo,mmoja amekutwa na risasi,nyama mbichi ya
pori na mapanga na sime nyumbani kwake.
Askari hao walikamatwa oktoba 25,mwaka
huu majira ya usiku na kikosi cha oparesheni okoa maliasili kinachoongozwa na
JWTZ baada ya kuweka mtego na kuwanasa kirahisi.
Upekuzi huo uliofanywa nyumbani
kwa askari koplo Isaack na Sixbert na kushuhudiwa na maafisa wa polisi walikuta
risasi 7 za bunduki aina ya SMG na SRA ,nyama mbichi ya porini kwenye ndoo ya
mnyama anayedhaniwa kuwa nyumbu,mapanga 15 na visu 9 nyumbani kwa koplo Isaack.
Licha ya kubainika kuwepo kwa Rco Mkoa wa Mara Mohammed kwenye upekuzi huo
hata hivyo alipoulizwa kwa njia ya simu kushiriki upekuzi na nini kilibainika
na inatoa ishara gani kwa idara yake alikana kuwa hakuwepo,”mimi sikuwepo huko
Mugumu niko Musoma”alisema.
Alisema kuwa wao hawahusiki na
operesheni hiyo,”kila wanachopata taarifa wanapeleka Dar es Salaam…sisi huku
kama kuna information kwa ajili ya
kufanyia kazi tunawapa …nao wakituhitaji wanasema …tunashirikiana kwa karibu
Kukamatwa kwa vitu hivyo kwa askari huyo kumezidi kuibua maswali na
hofu kutoka kwa raia huku ikitiliwa shaka kuwa mtandao huo ni mkubwa na huenda
wakawa na silaha maalum inayotumiwa kwa ajili ya uwindaji wa wanyama pori na matukio mengine.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara
Fernandi Mtui akiongea na Mwananchi kwa njia ya simu kuhusiana na upekuzi huo
alikiri ulifanyika lakini hakushiriki katika zoezi hilo kwa kuwa operesheni
hiyo inaundwa na askari mchanganyiko na wanakuwa na hati maalum za upekuzi.
“Ni kweli upekuzi umefanyika
lakini sikuhusika…sijajua kwa undani nini kimekamatwa…maana kikosi hicho wapo
askari wa kwetu,usalama wa taifa,wanyamapori na JWTZ na wana searc warrant(Hati
ya upekuzi)…mimi nasubiri kama wamekutwa na kosa wataletwa kwangu”alisema
kamanda.
Kamanda Mtui alisema kwa kuwa si
msemaji wa operesheni hiyo bado anasubiri taarifa ya uchunguzi na kama
watabainika kuwa na tuhuma watashitakiwa kijeshi kabla ya kushitakiwa
kiraia,”hapo ndipo nitakuwa na nafasi ya kulizungumzia hilo…nasema kila kitu
kitawekwa wazi…sitawanyima taarifa.
Oktoba 25 majira kati ya saa 4-5 usiku mwaka huu askari wawili waliotajwa kwa jina moja moja la Koplo Isaack na Sixbert wa
idara ya upelelezi walikamatwa wakiwa na raia mmoja Samweli Chacha
walikamatwa wakijaribu kuuza jino la
tembo katika eneo la Sedeco mjini Mugumu baada ya kuweka mtego maalum.
Askari hao wakiwa na gari aina ya
Toyota Corolla yenye namba za usajiri T269 BRN mali ya askari Sixbert walifika
eneo hilo na jino hilo kwa ajili ya kuuza wakiwa na raia wawili mmoja anadaiwa kutoroka baada ya wenzao
kukamatwa.
Baada ya kukamatwa kwa askari hao
walichukuliwa na kupelekwa eneo la
Andajenga lililomo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambako kikosi hicho
kina kambi maalum.
Serikali: Migogoro ya Tanapa, wananchi imalizwe
MWENYEKITI WA KAMA YA KUDUMU YA BUNGE YA MALIASILI ARDHI NA MAZINGIRA JAMES LEMBELI.
|
Ujangili walitesa Bunge
chanzo Tanzania daima
TUHUMA
za ujangili na Operesheni Tokomeza UIjangili inayoendeshwa na serikali, jana
ziliiteka Bunge baada ya Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kuituhumu
serikali kwa kutoa hoja nyepesi bungeni.
Lugola
alisema operesheni hiyo inafanyika kwa kukiuka haki za binadamu, kwamba watu
wasiokuwa majangili wamekamatwa, kuteswa na kuharibiwa mali zao ilhali
majangili wanaojulikana wakiachwa waendelee na uhalifu wao.
Wakati
mbunge huyo akitoa tuhuma hizo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Shamsi Vuai Nahodha, aliwatuhumu wabunge na wanasiasa wengine kwa kuingilia
utendaji wa operesheni hiyo kwa kuwatetea wanaokamatwa kwa kujihusisha na
ujangili.
Kauli
ya Nahodha ilionekana kumpiga kijembe Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, ambaye wiki iliyopita msaidizi wake
(ofisi ya ubunge) alikamatwa mkoani Iringa kwa tuhuma za ujangili.
Jana
Lukuvi alidai anao ushahidi ‘mzito’ wa mateso aliyoyapata msaidizi wa ofisi
yake, ambaye aliachiwa juzi baada ya kuonekana kutohusika na ujangili kama
ilivyokuwa ikidhaniwa.
Hoja
ilivyoanza
Hoja
hiyo ilitokana na swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Kahama, James
Lembeli (CCM), aliyetaka kujua kwanini serikali inaendelea kuwalinda
wanasiasa, askari na watendaji wake wanaojihusisha na ujangili.
Lembeli
pia alitaka kujua kwanini serikali haiwachukulii hatua za kisheria makamanda
wa polisi wa mipakani, hasa wale wanaopakana na mbuga ya Serengeti,
wanaojihusisha na ujangili, kutorosha nyara za serikali pamoja na
kushirikiana na majangili.
Akijibu
maswali hayo, Naibu Waziri wa Maliasili na Mazingira, Lazaro Nyalandu,
alisema kamwe wizara yake haiwalindi wanasiasa, wabunge, maofisa wa polisi na
watendaji wa serikali wanaohusika na ujangili.
Nyalandu
alisema kuanzia sasa kila kiongozi atakayekamatwa kwa tuhuma za ujangili
atatangazwa hadharani.
Alisema
si sahihi kuwatuhumu wabunge, polisi na watendaji wengine wa serikali bila ya
kuwa na utafiti juu ya tuhuma zao.
Hoja ya
Lugola
Mara
baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika, Lugola aliomba mwongozo wa
spika akitumia kanuni ya Bunge ya 67, ambapo alilitaka Bunge liiagize
serikali kutoa taarifa ya operesheni hiyo inayofanyika nchi nzima.
Lugola
aliomba mwongozo huo akisema kuwa majibu ya Waziri Nahodha na Nyalandu juu ya
suala hilo ni ya mzaha mzaha yenye lengo la kuendeleza kulindana.
Mbunge
huyo alilitaka Bunge liilazimishe serikali kutoa taarifa rasmi juu ya
Operesheni Tokomeza Ujangili.
Mara
baada ya Lugola, kuzungumza alisimama Lukuvi ambaye alitaka serikali iachwe
imalize operesheni hiyo bila kutoa taarifa kwani wakifanya hivyo wanaweza
kusababisha wahusika wakimbie au kupoteza ushahidi.
Alisema
taarifa za operesheni hiyo zitapelekwa katika kamati zinazohusika mara baada
ya kufikia tamati na baadae zitafikishwa bungeni kulingana na taratibu
zinazotakiwa.
Lukuvi
pia alionyesha simu yake ya mkononi akidai ina ushahidi wa mateso
yanayofanywa dhidi ya wanaokamatwa kwa tuhuma za ujangili.
“Nina
ushahidi wa msaidizi wangu alivyoteswa baada ya kukamatwa kuwa ni jangili,
huyu wamemuachia jana, nawaombeni tuache operesheni hii imalizike ndipo
tupatiwe taarifa zake,” alisema.
Naibu
Spika Job Ndugai, aliunga mkono kauli ya Lukuvi akidai taarifa za operesheni
hiyo zikitolewa sasa zitaharibu zoezi hilo.
Hoja ya
Lema
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema anatarajia kuwasilisha maelezo
binafsi bungeni kuitaka serikali izuie uwindaji wa tembo katika vitalu
vilivyo karibu na hifadhi au mbuga.
Lema
alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ujangili kuzidi kushika kasi.
Inakadiriwa tembo 30 wanauawa kila siku.
|
Anti-poaching unit accused of killings
By Mussa
Juma and Zephania Ubwani in Arusha, Bernard Lugongo in Dar, Peter Nyanje and
Frank Kimboy,The citizen
Posted Wednesday, October 30 2013
In Summary
Other reports say eight pastoralists from Orbomba
Village in Longido District have not been seen since they were arrested last
week.
Dar/Dodoma/Arusha. The anti-poaching campaign in
the country has come under sharp criticism following reports of widespread
human rights abuses, including the killing of a woman believed to have died at
the hands of officers of the anti-poaching unit--which is comprised of the
police, the army and intelligence officers.
Emaliana Gasper Maro, 46, is reported to have been
snatched from her house by people who identified themselves as anti-poachers.
They said they wanted to question the resident of Galapo in Babati, Mara
Region. This came only a few days after they reportedly grabbed her husband,
Elias Kibuga, 56.
Mr Kibuga has not been seen since but Emiliana’s
body was found at Mrara hospital mortuary in Babati. Scores others are missing.
The officers are also said to have burnt houses and are reported to be holding
large herds belonging to pastoralists in Arusha region. The government has
reportedly been urged to stop the exercise and ensure that lives and property
are respected.
Yesterday, the government came under attack from
MPs in Parliament over claims of widespread abuse of human rights.
The Manyara region police commander, Mr Akili
Mpwapwa, confirmed the reports but said an ongoing investigation would unearth
the truth. “I have received reports of the death of Emaliana and the
investigations have started,” Mr Mpwapwa said.
The results of a post-mortem that was jointly
carried out by the police and the family doctor have not been made public.
A total of 27 pastoralists and 2,169 livestock are
being held by the anti-poaching unit, according to the coordinator of the
Tanzania Pastoralist Community Forum, Mr Joseph ole Parsambei. “We will go to
court to stop this exercise if human rights violations continue,” said Mr
Parsambei.
Other reports say eight pastoralists from Orbomba
Village in Longido District have not been seen since they were arrested last
week. The unit is also said to be holding 2,000 livestock. Efforts to get the
authorities to address the allegations hit a wall.
The minister for Natural Resources and Tourism, Mr
Khamis Kagasheki, who had set off the special anti-poaching campaign when he
gave the shoot-to-kill order during the Global Elephant March in October 4, was
tight lipped. “I have nothing to say on that issue,” Mr Kagasheki told The
Citizen. “Every ministry has its spokesperson. Talk to him not me.”
The director for Wildlife at the ministry of
Natural Resources and Tourism, Mr Alexander Songorwa, referred the matter to
Tanzania People’s Defence Force (TPDF). The TPDF spokesman, Mr Erick Komba,
told The Citizen he was not aware of the allegations. He added: “The operation
is carried out jointly by the police, game wardens and intelligence.”
The Attorney General, Justice Frederick Werema, said
no minister had the powers to give a shoot-to-kill order. He told The Citizen:
“I did not hear the minister give the order. I suppose he was aggrieved by the
high rate of poaching in the country. All security forces must arrest suspects.
They can only shoot in self-defence.”
It is estimated that Tanzania loses 30 elephants
per day--or 10,000 a year. If the poaching trend persists, there might well be
no elephants in Tanzania in 10 years. Of the ivory seized in ports and airports
in the past decade, it is estimated that one-third originated from Tanzania.
The elephant population in the country has dropped to below 100,000 from about
130,000 a few years ago.
In Parliament, Alphaxard Kangi Lugola, the
outspoken Mwibara MP (CCM), said it was amazing that while the actual poachers
are known, the government has been targeting people who have nothing to do with
the vice.
“We have heard names of people suspected of
poaching who include government officials and politicians,” he charged. Mr
Lugola wanted the government to table in Parliament a report on Operation
Tokomeza, which is aimed at addressing poaching.
Mr James Lembeli (Kahama–CCM) said evidence
suggests that public officials, MPs and big businessmen are behind the poaching
but they have not been touched.
The State Minister in the PM Office (Policy,
Coordination and Parliament), Mr William Lukuvi, said his assistant was
arrested two days ago, beaten seriously and tortured--and was released only
yesterday by the anti-poaching unit. He added: “We should wait for the
operation to end and the ministry will table a report before a relevant
committee.”
The acting leader of government business in
Parliament, Mr Shamsi Vuai Nahodha, said the government was aware of the
accusations and asked those involved in the operation to respect human rights.
“There are also politicians who have been influencing this operation,” he
added. “When we started, we asked you to bear with us, please give us time and
space to conduct this operation.”
‘Tunataka majina ya vigogo majangili’
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMISI KAGASHEKI
Na Sharon Sauwa na Habel Chidawali,Mwananchi
Posted Jumatano,Oktoba30 2013 saa 24:0 AM
Posted Jumatano,Oktoba30 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
“Inashangaza sana kuwa wale wanaotajwa hawachukuliwi hatua, lakini
wananchi wanazidi kuteseka… Mathalani, zipo taarifa kuwa wakuu wa polisi katika
mikoa inayopakana na Mbuga ya Serengeti ndio waratibu wa shughuli za ujangili,
lakini hatujasikia hao wakichukuliwa hatua,”
Dodoma. Wabunge jana walichachamaa na kushinikiza kutolewa kwa orodha ya vigogo
wanaojihusisha na ujangili wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa 13 wa
Bunge unaofanyika mjini Dodoma.
Wabunge hao walitaka kutajwa kwa majina ya mawaziri, viongozi wa
Serikali na wabunge wanaojihusisha na biashara hiyo.
Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Mwibara
(CCM), Kangi Lugola, aliomba mwongozo, akiitaka Serikali kuwataja hadharani na
kuwachukulia hatua viongozi wake na wanasiasa, wakiwamo mawaziri na wabunge,
ambao wanatajwa kuhusika na vitendo vya ujangili nchini.
Lugola aliomba mwongozo wa Naibu Spika baada ya kutoridhishwa na jibu
lililotolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati
akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli.
Katika jibu hilo, Nyalandu alilieleza Bunge kuwa Operesheni Tokomeza
inayolenga kukomesha vitendo vya ujangili nchini bado inaendelea, lakini
alishindwa kulieleza Bunge ni nani hasa wamebainika kuhusika na vitendo hivyo.
Lugola, hata hivyo, aliitaka Serikali kuwasilisha ripoti bungeni
kuhusiana na utekelezaji wa operesheni hiyo.
“Tangu Aprili tumekuwa tukipewa majibu mepesi kuhusiana na operesheni
hii, wakati suala hili si la masihara,” alionya Lugola.
Lugola alisema kuwa taarifa zimewataja watu wanaohusika na vitendo hivyo
wakiwamo viongozi serikalini, mawaziri pamoja na wabunge, lakini tangu
operesheni hiyo ilipoanza hakuna yeyote miongoni mwa hao wanaotajwa ambaye amekamatwa
isipokuwa wananchi wa kawaida.
Alisema operesheni hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa unyama kwani
wanaokamatwa hupigwa na kuteswa bila ya ushahidi unaoonyesha kuhusika kwao na
vitendo vya ujangili.
“Inashangaza sana kuwa wale wanaotajwa hawachukuliwi hatua, lakini
wananchi wanazidi kuteseka… Mathalani, zipo taarifa kuwa wakuu wa polisi katika
mikoa inayopakana na Mbuga ya Serengeti ndio waratibu wa shughuli za ujangili,
lakini hatujasikia hao wakichukuliwa hatua,” alisema.
Kabla ya Naibu Spika kutoa majibu ya mwongozo ulioombwa na Lugola,
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William
Lukuvi, alisimama na kukiri kuwapo kwa vitendo vya utesaji wa watu wanaokamatwa
katika operesheni hiyo.
Alitolea mfano tukio la kukamatwa kwa msaidizi wake jimboni ambaye
alipigwa na kuteswa na askari hao kabla ya kuachiwa baada ya kushikiliwa kwa
siku moja, huku akionyesha kuwa ushahidi wa tukio hilo anao kwenye simu yake.
“Lakini sisemi haya kwa kutaka
kuitetea Serikali kuwa isilete ripoti hapa bungeni. Nadhani kuwa kuleta ripoti
hivi sasa haitakuwa vizuri. Ni vizuri tusubiri mpaka kazi hii ikamilike na nina
uhakika kuwa Wizara itaandaa ripoti na kuiwasilisha kwenye kamati husika,”
alisema na kuongeza:“Nadhani kuwa `entry point’ (mahali pa kuanzia) yetu iwe ni kwenye ripoti hii itakayowasilishwa kwenye Kamati,”
Suala la ujangili limeingizwa bungeni wakati kukiwa na usiri mkubwa wa nani anahusika na vitendo hivyo, huku majina ya vigogo wanaotajwa kuhusika nayo wakiwa hawafahamiki.
Polisi watajwa vinara
Awali akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine Ndugulile, Nyalandu alisema Jeshi la Polisi ni vinara miongoni mwa makundi manne ya majeshi ambayo watumishi wake wamekamatwa wakijihusisha na ujangili.
Katika matukio saba ya ujangili yaliyowahusisha watumishi tisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, Nyalandu alisema kati ya hao sita ni polisi wakati kwa kupande wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Magereza alikamatwa mtu mmoja mmoja.
“Katika matukio hayo, jumla ya meno ya tembo 686 na vipande 447 vikiwa na uzito wa kilogramu 4,253.9 vilikamatwa, jambo ambalo linaonyesha ukubwa wa tatizo hilo kwa vyombo vya ulinzi,” alisema Nyalandu.
Katika swali la msingi, Dk Ndugulile alitaka kufahamu idadi ya matukio ya upatikanaji wa pembe za ndovu yaliyohusisha vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika swali la nyongeza, Lembeli ambaye ndiye aliyeuliza swali hilo kwa niaba ya Dk Ndugulile, aliitaka Serikali kuacha kigugumizi na kueleza ukweli kuwa wapo baadhi ya viongozi, wakiwamo wabunge ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo.
“Katika biashara ile kuna hali ya kulindana sana, hebu Serikali itueleze taarifa za kuwa wahusika wengine ni wanasiasa na baadhi ya wabunge, ukweli uko wapi, na kuna taarifa kuwa viongozi wa Polisi wanaoishi kuzunguka hifadhi zetu ndio ambao wanatumiwa kusafirisha nyara hizo, Serikali inasemaje?” alihoji Lembeli.
Nyalandu alisema Tanzania iko katika hali mbaya katika kiwango cha mauaji ya tembo ambapo wastani unaonyesha kuwa kila siku tembo 30 huuawa na majangili.
“Hata hivyo, suala la ulinzi bado tuko nyuma sana kwani wastani wa ulinzi wa kimataifa ni askari mmoja kwa kilomita za mraba 25, lakini sisi askari wetu mmoja analinda kilomita za mraba 150 ndani ya hifadhi,” alisema Nyalandu.
Serikali yakiri tatizo
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha
akizungumza bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu, alikiri kuwapo fununu za
wanasiasa ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo na kusema Serikali
italifanyia kazi jambo hilo.
Nahodha aliwataka Watanzania kuwa watulivu wakati vyombo vya Ulinzi na
Usalama vinaposhughulika na kusafisha tatizo hili na kuonya wanasiasa kuacha
kutoa shinikizo kwa kutumia nguvu zao za kisiasa.
Tuesday, October 29, 2013
MJADALA BUNGENI KUHUSU UJANGILI
Toka jan-okt mwaka huu matukio 7 yaliyohusisha kukamatwa kwa maaskari wa polisi,magereza,jwtz na wanyama pori wakihusika na biashara haramu ya meno ya tembo yametajwa bungeni.
Matukio hayo yalihusisha ukamataji wa meno 646,na vipande zaidi ya 440 ,hali hiyo inatia shaka juu ya vyombo vyenye dhamana ya ulinzi wa maliasili .
Akijibu maswali ya liyoulizwa na James Lembeli aliyetaka kujua maafisa wa polisi walioko mikoa iliyo kando ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushirikiana na majangili kutorosha nyara na pia kulindana kwa kuwa watuhumiwa baadhi ni wanasiasa.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema hakutakuwa na kulindana na operesheni Tokomeza inayohusisha vyombo vyote vya ulinzi haitamuacha hata mtu mmoja
anayetuhumiwa kuhusika na vitendo vya ujangili hata angalikuwa mwanasiasa.
Hata hivyo Lugola mbunge wa mwibara ameibuika na mwongozo kuwa operesheni tokomeza inayohusu ujangili wa tembo,"kuna watu wako ndani ya hifadhi wamekamatwa na wanapigwa...lakini wawindaji wa tembo hawakamatwi,hawapigwi huu ni mzaha,hapa kuna kulindana maana inaonekana wanaohusika ni watu wakubwa ,wabunge ,mawaziri wasemwe na wakamatwe si kuendelea kuonea wananchi wasiokuwa na hatia,naomba mwongozo wako.
Lukubi anasema taarifa itatolewa kwa kamati ya Maliaisli maana operesheni inayoendelea inalenga kuwabaini na kuwakamata wahusika ,amekiri kuwa msaidizi wake wa jimbo amekamatwa na amepigwa sana na alikutwa ofisini kwa Lukuvi na anao ushahidi wa kilichotokea.
Matukio hayo yalihusisha ukamataji wa meno 646,na vipande zaidi ya 440 ,hali hiyo inatia shaka juu ya vyombo vyenye dhamana ya ulinzi wa maliasili .
Akijibu maswali ya liyoulizwa na James Lembeli aliyetaka kujua maafisa wa polisi walioko mikoa iliyo kando ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushirikiana na majangili kutorosha nyara na pia kulindana kwa kuwa watuhumiwa baadhi ni wanasiasa.
Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema hakutakuwa na kulindana na operesheni Tokomeza inayohusisha vyombo vyote vya ulinzi haitamuacha hata mtu mmoja
anayetuhumiwa kuhusika na vitendo vya ujangili hata angalikuwa mwanasiasa.
Hata hivyo Lugola mbunge wa mwibara ameibuika na mwongozo kuwa operesheni tokomeza inayohusu ujangili wa tembo,"kuna watu wako ndani ya hifadhi wamekamatwa na wanapigwa...lakini wawindaji wa tembo hawakamatwi,hawapigwi huu ni mzaha,hapa kuna kulindana maana inaonekana wanaohusika ni watu wakubwa ,wabunge ,mawaziri wasemwe na wakamatwe si kuendelea kuonea wananchi wasiokuwa na hatia,naomba mwongozo wako.
Lukubi anasema taarifa itatolewa kwa kamati ya Maliaisli maana operesheni inayoendelea inalenga kuwabaini na kuwakamata wahusika ,amekiri kuwa msaidizi wake wa jimbo amekamatwa na amepigwa sana na alikutwa ofisini kwa Lukuvi na anao ushahidi wa kilichotokea.
Monday, October 28, 2013
WAHUKUMIWA KIFUNGO KWA KUINGIA H.IFADHINI BILA KIBALI
Oktoba 28,2013.
Serengeti:
WAKAZI wanne kutoka wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha
wamehukumiwa na mahakama ya wilaya ya
Serengeti kifungo cha miezi sita jela
ama kulipa faini ya sh,120,000 kila mmoja kwa kosa la kuingia hifadhi ya taifa ya Serengeti bila
kibali.
Waliohukumiwa na mahakama hiyo ni Ndotei Sundi(30)Siatoi Warukwar(19) Kitupe Lesiani
(30)wakazi wa kijiji cha Warbai na Daud Kesoi(19)mkazi wa kijiji cha Maranja Ngorongoro ambao walikosa fedha na kuamriwa
kwenda gerezani.
walitenda kosa hilo
oktoba 23 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana.
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Franco Kiswaga , Mwendesha mashitaka wa polisi sajenti Paskael Nkenyenge alidai oktoba 23 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana askari wa hifadhi hiyo wakiwa doria eneo la
Naabi waliwakamata washitakiwa hao na hawakuwa na kibali cha kuingia hifadhini.
Washitakiwa wote walikiri shitaka la kuingia hifadhini bila
kibali na kuilazimu mahakama hiyo kutoa adhabu kulingana na kosa walilotenda.
Akitoa hukumu Hakimu Kiswaga ameiambia mahakama kuwa
kufuatia washitakiwa kukiri shitaka bila kuisumbua mahakama ,anawahukumu kila mmoja kulipa faini ya shilingi 120,000 ama kutumikia kifungo cha miezi sita jela ili
iwe onyo kwa wenye tabia kama hiyo .
Mwisho.
Tido: Sekta ya habari inaweza kukuza utalii
Chanzo- Mwananchi
Posted Ijumaa,Oktoba25 2013
Posted Ijumaa,Oktoba25 2013
Kwa ufupi
Alisema muda umefika kwa filamu na
matangazo yote yanayoelezea vivutio vya utalii Afrika kuandaliwa, kurekodiwa na
kurushwa na Waafrika wenyewe.
Arusha. Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), Tido Mhando amesema tasnia ya habari
ikitumika vyema inaweza kutoa mchango mkubwa kuinua sekta ya utalii kutokana na
kuaminiwa na kufikia watu wengi kwa wakati mmoja.
Mhando alisema hayo jana akizungumzia
nafasi ya vyombo vya habari katika kuinua sekta ya utalii Afrika wakati wa
mkutano wa Umoja wa Vyombo vya Utangazaji Kusini mwa Afrika (SABA).
Kwa mujibu wa Mhando , umuhimu wa
vyombo vya habari unachagizwa na maendeleo na matumizi ya sayansi na teknolojia
inayorahisisha utengenezaji na urushaji wa matangazo yenye ubora.
Naye Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi aliwataka watengenezaji wa vipindi
na filamu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuandaa, kutengeneza na kurusha
vipindi vinavyoonyesha na kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika
ukanda huo, ili kukuza sekta ya utalii.
Alisema muda umefika kwa filamu na
matangazo yote yanayoelezea vivutio vya utalii Afrika kuandaliwa, kurekodiwa na
kurushwa na Waafrika wenyewe.
Awali akifungua Mkutano Mkuu wa 21 wa
SABA, Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal alivitaka vyombo vya SADC
kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi zao, badala ya kuacha kazi
hiyo kufanywa na vyombo vya habari vya nje.
Dk Bilal alivitaka vyombo ya utangazaji
kutumia kuaminika kwao kwa jamii kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na ulinzi wa
maliasili.
Sunday, October 27, 2013
Lembeli: Ruaha kiini cha mgogoro wa Ihefu
Jumamosi,
Octoba 26, 2013 07:20 Na Pendo Fundisha, Mbeya
KAMATI ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, imesema Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha ni kiini cha mgogoro wa ardhi unaoendelea katika Bonde la Ihefu kutokana
na kumega maeneo yasiyoainishwa na kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya
(RCC). Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James
Lembeli, katika ziara ya kukagua shughuli na miradi ya Serikali.
Alisema kikao cha RCC ndicho kilipaswa kuyaingiza maeneo hayo au kutoyaingiza ndipo hifadhi hiyo ingetekeleza majukumu yake ya kuweka mipaka.
Alisema eneo lililoongezwa na hifadhi hiyo ni kutoka kilomita 10,000 za mraba hadi kufikia kilomita 20,000 za mraba ambazo hazikuainishwa katika kikao cha RCC.
Aidha, imeitaka Serikali kutoa majibu haraka ya tume zilizoundwa kwa ajili ya kuchunguza mgogoro wa mpaka baina ya wananchi wa vijiji hivyo na hifadhi hiyo.
“Serikali iliunda tume mbalimbali za kuchunguza tatizo hili ikiwamo timu ya wataalamu iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Hivyo ni vema ikaharakisha kutoa majibu kwa kuwa muda mrefu umepita pasipo kusema lolote lile,” alisema Lembeli.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, alisema mgogoro huo upo njiani kumalizika kwa kuwa suluhisho lake limefika katika ngazi za mwisho.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Martin Loibooki, alisema jambo hilo limechukua muda mrefu baada ya kuwapo kwa mkanganyiko juu ya uwekaji wa mipaka hiyo, ambapo kuna wananchi walipeleka kesi hiyo mahakamani kuwa walipunjwa fidia zao.
Alisema kikao cha RCC ndicho kilipaswa kuyaingiza maeneo hayo au kutoyaingiza ndipo hifadhi hiyo ingetekeleza majukumu yake ya kuweka mipaka.
Alisema eneo lililoongezwa na hifadhi hiyo ni kutoka kilomita 10,000 za mraba hadi kufikia kilomita 20,000 za mraba ambazo hazikuainishwa katika kikao cha RCC.
Aidha, imeitaka Serikali kutoa majibu haraka ya tume zilizoundwa kwa ajili ya kuchunguza mgogoro wa mpaka baina ya wananchi wa vijiji hivyo na hifadhi hiyo.
“Serikali iliunda tume mbalimbali za kuchunguza tatizo hili ikiwamo timu ya wataalamu iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Hivyo ni vema ikaharakisha kutoa majibu kwa kuwa muda mrefu umepita pasipo kusema lolote lile,” alisema Lembeli.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, alisema mgogoro huo upo njiani kumalizika kwa kuwa suluhisho lake limefika katika ngazi za mwisho.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Martin Loibooki, alisema jambo hilo limechukua muda mrefu baada ya kuwapo kwa mkanganyiko juu ya uwekaji wa mipaka hiyo, ambapo kuna wananchi walipeleka kesi hiyo mahakamani kuwa walipunjwa fidia zao.
Saturday, October 26, 2013
TAHARIRI-TANZANIA DAIMA
Ujangili ni zao la kulindana
|
KWA muda mrefu sasa nchi mbalimbali zimekuwa kwenye mapambano ya ujangili, hasa ule wa meno ya tembo.
Inakadiriwa kila dakika 15 tembo mmoja huuawa duniani. Biashara ya meno ya tembo hivi sasa imeshamiri zaidi. Kwa mujibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki jino moja huuzwa kati ya dola za Marekani 1,500 na 2,000. Pamoja na jitihada za kupambana na ujangili huu, bado matukio ya vifo vya tembo yanaongezeka kila kukicha kutokana na ukosefu wa vifaa pamoja na uadilifu mdogo wa watendaji waliopewa jukumu la kusimamia. Tunaamini kama utaratibu wa kulindana, kuoneana aibu na kupuuzia mambo usingekuwepo, Tanzania ingepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya ujangili. Limekuwa jambo la kawaida kila kukicha kusikia watendaji wa serikali, vyombo vya dola, idara au taasisi mbalimbali kukamatwa wakiwa na meno ya tembo na nyara mbalimbali ambazo ni kosa la kisheria. Pamoja na watu hao kukamatwa na nyara hizo, bado inaonekana hakuna uwajibishanaji ndiyo maana watumishi wengine wamekuwa wakiendelea na uahalifu huo, na hata kushirikiana na watu kutoka nje. Tunaamini kuwa mpango wa serikali wa kutumia ndege zisizo na marubani kupambana na ujangili hauwezi kufanikiwa kama tabia ya kulindana, kuoneana aibu haitakomeshwa. Tunaamini ‘Operesheni Tokomeza Majangili’ itakuwa na manufaa zaidi ikiwa Wizara ya Maliasili na Utalii itasafisha kwanza nyumbani kwake, ikiwemo kuwachukulia hatua kali watumishi wanaohusishwa na uhalifu. Tunachukua fursa hii kumpongeza Waziri Kagasheki kwa kutangaza hadharani kuwa Kikosi Cha Kupambana na Ujangili (KDU), wanasiasa, watumishi wa umma na wafanyabishara mbalimbali wanahusika na biashara hii. Tunajua kuwatangaza watu kuhusika na biashara hii ni hatua moja muhimu, hivyo ni vema hatua nyingine ya kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ikachukuliwa. Bila kuwajibishana, kudhibitiana, biashara ya meno ya tembo, faru na mazao ya misitu itaendelea kushamiri huku taifa likiangamia kwa kukosa mapato yatokanayo na wanyama hao. Tunaamini kuwa serikali itaitumia kikamilifu Operesheni Tokomeza Ujangili kukabiliana na watu wote wanaohusishwa na vitendo hivyo vya kihalifu bila kujali nyadhifa zao. |
Waziri Kagasheki matatani
• Raia wa kigeni
aliowaita majangili, walibambikwa kesi
na Grace Macha, Arusha-Chanzo Tanzania Daima
|
JESHI
la Polisi mkoani Arusha, limeingia kwenye kashfa nzito baada ya kubainika
kumdanganya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kwa
kuwahusisha raia wawili wa kigeni na biashara ya ujangili wakati si kweli.
Hatua
hiyo inakuja baada ya Waziri Kagasheki kudai kuwa watumishi wa serikali
wanakwamisha juhudi za kukabiliana na majangili wa tembo, akitolea mfano wa
Mkuu wa Upelelezi wa Polisi mkoani hapa (RCO), Duwan Nyanda, kwamba
aliwatorosha raia wawili wa Saudia ambao walikamatwa wakiwa na meno ya tembo
pamoja na silaha nzito.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali na nyaraka kadhaa, Tanzania Daima limebaini kuwa
raia hao waliingia nchini Septemba 12, mwaka huu, kupitia Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kisha kufikia kwenye hoteli ya kitalii
ya Mount Meru.
Nyaraka
hizo zinaonyesha kuwa wageni hao waliondoka nchini Oktoba 4, mwaka huu,
kupitia uwanja huo huo.
Kwa
mujibu wa waraka wa upekuzi wa polisi (search order) uliosainiwa na Inspekta
James, maofisa wa jeshi hilo walifika kwenye hoteli hiyo Oktoba 3, mwaka huu,
na kupekua vyumba vya wageni hao, lakini hawakukuta kitu chochote
kinachohusiana na nyara za taifa za maliasili kama ilivyodaiwa na Waziri
Kagasheki.
Nyaraka
hiyo inaonyesha kuwa walioshuhudia upekuzi huo mbali na waliokuwa watuhumiwa,
Ali na Nader, ni pamoja na Gidion David na Joseph Enock ambao
waliisaini.
Tanzania
Daima lilifika hotelini hapo na kuzungumza na meneja mapokezi, Enock Maselle
ambaye pia alithibitisha kuwa Oktoba 3, mwaka huu, walifika polisi kwa ajili
ya kukagua vyumba vya wateja wao, Ali na Nader.
Alisema
kuwa waliwaruhusu, lakini akadai ni vigumu kujua nini kiliendelea.
Raia
hao wanadaiwa kujihusisha na kutafuta watu nchini mwao ambao huwaleta Tanzania
kutalii, na kwamba waliingia nchini na kundi la wageni tisa ambao walifanya
safari kwa nyakati mbili tofauti, wakitembelea hifadhi za taifa za Manyara na
Tarangire na
Ngorongoro iliyopo chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA).
Mmiliki
wa kampuni ya uwakala wa utalii ya Kalabash, Ally Kalabash aliliambia gazeti
hili kwa simu kuwa Ali na Nader walimletea wageni tisa ambao alifanya nao
safari ya siku tatu katika mbuga za Manyara, Ngorongoro na Tarangire.
“Hawa
ni mawakala wapya, na hii ni mara yangu ya kwanza kufanya nao kazi, ila
wageni walioniletea niliwahudumia mpaka siku wanaondoka, kwani wengine
walilala Mount Meru Hotel na wengine Themi Suite,” alisema.
Naye
Salim Islam Salim ambaye ndiye alikuwa karibu na raia hao wa Saudia, alisema
kuwa walipokuwa hapa nchini walikutana na Richard Kalembe ambaye
aliwaambia anamiliki kampuni ya uwindaji wa kitalii ya RS Kalembe Hunting
Routes.
Alisema
kuwa Septemba 14, mwaka huu, Ali na Nader walimlipa Kalembe malipo ya awali
kwa ajili ya kwenda kuwinda kitalii, kiasi cha dola za Marekani 3,000.
Salim
alifafanua kuwa Kalembe aliwapatia wageni hao risiti yenye namba 012
ikionyesha kuwa bado wanadaiwa dola 7,000 endapo watatumia siku tano na ikiwa
watatumia siku tisa wakiwinda, basi wangelazimika kuongeza dola 9,000.
Kwa
mujibu wa Salim, baada ya Kalembe kupokea malipo hayo, hakufanya mawasiliano
tena na wageni hao, hatua iliyowalazimu kutoa taarifa polisi Oktoba 2, mwaka
huu.
Alisema
kuwa siku iliyofuata, raia hao walipigiwa simu na polisi wa upelelezi
aliyemtaja kwa jina moja la James, akiwaambia kuwa mtuhumiwa wao
ameshapatikana, hivyo wafike polisi ili wakakabidhiwe fedha zao.
“Katika
hali ya kushangaza, walipofika polisi waligeuziwa kibao na kuwekwa chini ya
ulinzi, wakitakiwa kwenda kupekuliwa kwenye vyumba vyao katika hoteli
waliyofikia ya Mount Meru, ambako hata hivyo hawakukutwa na kitu.
“Baadaye
walirudishwa polisi na kuelezwa sababu za kupekuliwa, kwamba walitiliwa
shaka kuwa wanajihusisha na ugaidi,” alisema Salim.
Alifafanua
kuwa polisi waliwaambia kuwa kutokana na tukio la kigaidi lililotokea
hivi karibuni nchini Kenya, wamekuwa makini kwa kila
mtu wanayemuhisi au kumtilia shaka, na hivyo humfanyia upekuzi.
Kwa
mujibu wa Salim, baada ya maelezo hayo walielezwa kuwa wanaweza kuwadhamini.
Yeye na mtu mwingine aliyemfahamu kwa jina moja la Ibra, walimdhamini
Ali huku Nader akidhaminiwa na msichana mwingine ambaye hakumfahamu vizuri.
“Oktoba
4, tulifika pale polisi asubuhi, baada ya panda shuka, watuhumiwa hao
waliwaeleza polisi kuwa wanapaswa kuondoka siku hiyo, hivyo wakaomba wapewe
ruhusa wakabadili tiketi zao au wapelekwe mahakamani ili wajue wanashikiliwa
kwa makosa gani.
“Tukiwa
pale, akaja polisi mmoja mwanamke akasema ‘kama hawa mmewapekua mkaona hawana
kitu, waachieni waende zao’. Ilikuwa kama saa tano asubuhi,” alisema.
Salim
alisema kuwa wageni hao walipewa simu na hati zao za kusafiria na hivyo
wakaondoka kituoni hapo, na baadaye jioni walipanda ndege ya Shirika la Ndege
la Ethiopia na kurudi kwao.
Alisema
kuwa alishangazwa na taarifa zilizoandikwa na vyombo mbalimbali vya habari
zikiwahusisha Ali na Nader na uwindaji haramu huku wakidaiwa kukutwa na pembe
za ndovu, jambo alilodai ni uongo na upotoshaji mkubwa.
Salim
alisema madai ya kwamba dola 3,000 zilitolewa polisi kama rushwa si ya kweli,
kwani kiasi hicho ni fedha anazodaiwa Kalembe alizochukua kwa raia hao,
huku akidai taarifa iko polisi.
Alipotafutwa
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas kuzungumzia sakata hilo,
alisema hayuko tayari kwa sababu linashughulikiwa na mkuu wa jeshi hilo, IGP
Said Mwema ambaye ameunda tume ya uchunguzi.
Naye
Waziri Kagasheki alipotafutwa, simu yake iliita bila kupokelewa.
Salim
ageuziwa kibao
Katika
hatua nyingine, Salim na Gerald Kashiro wamelalamikia kitendo cha kukamatwa
na askari wa kuzuia ujangili kwa nyakati tofauti na kupewa mateso makali,
huku mfanyabiashara Shafiq Feroz akidai kuwa alishikiliwa bila kuteswa.
Walisema
chanzo cha mateso hayo ni nyama ya nyati kilo tano ambayo Feroz alimpatia
Kashiro baada ya kuwa amemsindikiza kuwinda kwenye pori la Terati wilayani
Simanjiro.
Kashiro
alisema kuwa yeye alipopewa nyama hiyo alimwachia mke wake, Judith
Gerald nyumbani akiendelea kuiandaa, huku yeye akiendelea na shughuli
zake.
Alisema
kuwa baadaye alipigiwa simu akiambiwa kuwa mkewe na mama mkwe, wamekamatwa na
askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili (KDU) wakiwa na wanajeshi.
Akisimulia
mkasa mzima, Salim alisema kuwa Kashiro alimpigia simu akimuomba ampeleke
alipo Feroz ili aweze kupeleka vibali vyake vya uwindaji kwa kambi ya KDU
iliyopo Njiro waweze kuwaachia mkewe na mama mkwe.
Alisema
kuwa baada ya kumfikisha kwa Feroz, aliwaacha wakaelekea Njiro, na yeye
akarudi kuendelea na shughuli zake, lakini wakampigia simu tena wakimuomba
akawadhamini kwani wameshikiliwa.
Kwa
mujibu wa Salim, juhudi za kuwadhamini Kashiro na Feroz
hazikufanikiwa, hivyo aliamua kuondoka. Lakini kabla hajafika kwenye
lango kuu la kutokea, akaitwa na kuulizwa na askari nyumbani kwake ni wapi
ili wakampekue.
Aliongeza
kuwa alipopekuliwa nyumbani kwake Kimandolu, alikutwa na bunduki tatu aina ya
riffle na bastola aina ya short-gun ambazo zote anazimiki kihalali na kwamba
walijiridhisha baada ya kuwaonyesha nyaraka zote muhimu kisha wakarudi naye
hadi KDU Njiro.
“Mimi
na Feroz tuliambiwa tujidhamini wenyewe kwani tunaacha silaha zetu pale.
Feroz naye alikuwa amepekuliwa kwenye hoteli ya Themi Suites alipokuwa
amefikia kutoka Dar es Salaam anakokaa.
“Tulitakiwa
kurudi siku inayofuata, yaani Oktoba 8, mwaka huu, lakini tulipofika siku
hiyo, tukachukuliwa na kufungwa pingu, tukapakiwa kwenye
gari tukapelekwa Terati. Huko kuna eneo limefungwa hema, tulipofika
sikuamini kama Tanzania kuna watu wanateswa hivyo,” alidai.
Kwa
mujibu wa Salim, aliwekewa vijiti katikati ya vidole vyake na kuanza
kuminywa, lakini akawahakikishia kwamba hajihusishi na ujangili.
“Wakachukua
dumu la maji baridi la lita 10 na muda huo ni usiku, baridi ni kali,
wakanimwagia mwili mzima nikiwa na nguo, kisha wakaniambia nitambae kwenye
mchanga mpaka saa tisa usiku ndipo nilipewa fursa ya kulala,” alisema Salim.
Alisema
kuwa walikuwa watu wengi wanaopatiwa mateso ya aina mbalimbali, ikiwemo
kuchapwa viboko pamoja na kufanyishwa kwa nguvu mazoezi ya kupiga ‘push-up’.
Waliondolewa baada ya siku tatu wakapelekwa Serengeti kwenye eneo
lililotengwa kwa ajili ya kikosi hicho.
Salim
alisema kuwa walipofika huko waliendelea kuteswa, na aliomba kuonana na
daktari baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya kwani anakabiliwa na matatizo ya
kisukari pamoja na figo iliyokuwa ikimuuma sana kutokana na mateke
aliyopigwa.
“Daktari
alishauri nipatiwe dawa na nipumzishwe, jambo lililonipa hauweni ya
kutoendelea kupata mateso, maana nilihamishiwa Kituo cha Polisi Bunda
nilikokaa kwa siku nne kabla ya kufikishwa mahakamani.
“Hata
hivyo, baada ya kufikishwa mahakamani sikusomewa shitaka lolote, bali hakimu
aliniambia kuwa mahakama inaniachia huru kwani sina kosa. Nilihoji ni kwanini
nikateswa bure siku 14,” alisema.
Kashiro
ambaye naye alilalamikia kuteswa, alisema kuwa amefunguliwa shitaka la
uhujumu uchumi pamoja na Feroz. Watatakiwa kufika mahakamani Bunda Novemba 7,
mwaka huu wakati shauri lao litakapofika kwa ajili ya kutajwa.
Operesheni
Tokomeza Ujangili ilianza rasmi Oktoba 5, mwaka huu katika hifadhi za taifa,
mapori ya akiba na mbuga za wanyama ikishirikisha Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Idara ya Wanyamapori.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)