Na Mwandishi maalum
26th September 2015
Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ameeleza
changamoto kubwa zinazozuia kukua haraka kwa sekta ya utalii katika
Afrika na kushindwa kuchuma matunda ni kutotangazwa sahihi kwa sekta hiyo
katika bara hilo.
Alisema pamoja na kuwa na vivutio
vingi vya utalii, Bara la Afrika, bado linabakia nyuma kwa kiasi kikubwa
katika kuvutia watalii wa kimataifa na mapato yanayotokana na utalii.
Alisema Tanzania itaendelea kutenga eneo kubwa la ardhi yake kwa ajili ya
hifadhi na pia kukabiliana na ujangili dhidi ya tembo, ambao hata hivyo
amesema umepungua katika mwaka uliopita.
Aliyasema hayo juzi wakati alipotoa
hotuba ya ufunguzi wa shughuli za miaka 10 ya chama cha Usafiri cha
Afrika (ATA) na miaka 10 ya Jukwaa la Rais Kuhusu Utalii ñ Presidential
Forum on Tourism kwenye Kituo cha Kimmel cha Chuo Kikuu cha New York (New
York University Kimmel Center) Africa House, mjini New York.
Rais Kikwete alitumia mkutano huo
pia kuaga jukwaa hilo akiwa kama Rais wa Tanzania. Kwa mujibu wa Katiba,
Oktoba 25 itakuwa mwisho wa kipindi chake cha pili.
Rais Kikwete anahudhuria shughuli za
mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) baada ya kumaliza
kuendesha vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani ambao wanatafuta jinsi
gani dunia inavyoweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na magonjwa ya
mlipuko, jijini hapa.
Rais Kikwete ametambulishwa na
kukaribishwa kutoa hotuba yake na Dk. Yaw Nyarko, Raia wa Ghana na
Mkurugenzi wa Africa House ambaye pia ni Profesa wa uchumi kwenye Chuo
Kikuu cha New York na Edward Bergman, Mkurugenzi Mtendaji Mwanzilishi wa
ATA.
Rais Kikwete na familia ya Bergman
ya New York, walianzisha na kujadili wazo la kuanzishwa kwa chama
hicho miaka 10 iliyopita.
Mawaziri waliozungumza kwenye
shughuli hiyo iliyoendeshwa na Peter Greenberg, Mhariri wa Usafiri wa
Televisheni ya CBS ni Lazaro Nyalandu wa Tanzania, Dk. Maria
Mutagamba, Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Nyaraka wa Uganda ambaye pia
ni Rais wa ATA na NíDiaye Ramatoulaye Diallo, Waziri wa Utamaduni, Utalii
na Usanii wa Vinyango wa Mali.
Mawaziri wengine ni Phylis Kandie wa
Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya na Pohamba
Shifeta wa Mazingira na Utalii wa Jamhuri ya Namibia.
Rais Kikwete alisema: Changamoto kuu
zinazokabili maendeleo ya utalii katika Afrika ni miundombinu ya kitalii,
utangazaji wa masoko ya utalii na matatizo ya usafiri wa anga kuingia na
kutoka Afrika.
Lakini pia kuna jambo kubwa la
mtazamo hasi kuhusu Afrika. Kwa kawaida, vyombo vya habari vya nje
vinalielezea Bara la Afrika kama Bara hatari ambalo sifa zake kuu ni
migogoro, magonjwa na matatizo yanayotokana na umasikini.
Alitaka ukweli kuhusu Afrika uelezwe
kwa usahihi na waafrika wenyewe.
Alisema picha inayojengwa ni kuwa
tatizo la nchi moja ni tatizo la bara zima kitu ambacho si cha
kweli.
Alisema upotoshaji huo umesababisha
watu kufuta safari za kitalii kwenda Afrika wakati ugonjwa wa ebola ulipolipuka
nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
CHANZO: NIPASHE
Habari Zaidi
No comments:
Post a Comment