MWENYEKITI WA KAMA YA KUDUMU YA BUNGE YA MALIASILI ARDHI NA MAZINGIRA JAMES LEMBELI.
|
|
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Mazingira, imeitaka
serikali kuhakikisha inashughulikia migogoro yote ya ardhi inayohusu
Tanapa na wananchi.
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari kamati hiyo
ilipofanya ziara jijini Mbeya, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James
Lembeli, alisema kuna migogoro ya mipaka inayozikabili baadhi ya
hifadhi za taifa nchini.
Akitolea mfano, Lembeli alisema hifadhi ya taifa ya Ruaha yenye eneo
oevu la Ihefu iliyoko mkoani hapa ilikumbwa na mgogoro huo baada ya
Kkikao cha Maendeleo cha Mkoa (RCC), kushindwa kusimamia suala hilo
kikamilifu.
Alisema baada ya kujitokeza mgogoro huo serikali iliunda kamati
mbalimbali kwa ajili ya kuchunguza na tayari umeshafanyiwa kazi.
Alisema kilichosababisha kuchelewa kutolewa kwa maamuzi ya kamati ni
kesi zilizofunguliwa mahakamani zinazohusu mgogoro huo wa mipaka
katika hifadhi hiyo.
Aidha alienda mbali na kusema kuwa serikali inapaswa kuwa mstari wa
mbele katika kuhakikisha wananchi wake hawapati mateso au usumbufu
usio wa lazima katika maeneo yao kwa kwani ndiyo wenye rasilimali
hizo.
Pia alibainisha kuwa maeneo mengi yanayotumiwa na wananchi, yamekuwa
na migogoro mingi inayohusu mipaka ya ardhi hasa wakati wa shughuli za
upanuzi wa hifadhi za taifa au uwezekezaji mkubwa unapotakiwa
kufanyika jirani na makazi ya wananchi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna
Kibenga, alisema mipango ya wizara yake iko katika hatua nzuri ikilenga
kuondoa au kumaliza migogoro yote ambayo imekuwa ikijitokeza katika
maeneo mengi ya hifadhi za taifa nchini.
Maimuna alisema kuwa wizara yake kupitia bodi ya hifadhi za taifa
imekuwa ikifanya kazi kwa kufuata taratibu kanuni na sheria
zinazoiongoza wizara hiyo hivyo hatarajii kuona mambo yanaenda kinyume
kwa kuwa kila mtumishi wa wizara hiyo anatakiwa kufanya kazi kwa
kuheshimu na kuzingatia sheria.
Pia Dk. Martin Loibooki ambaye ni Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa
(Tanapa), alisema kuwa kazi na majukumu ya Wizara ya Maliasili na
Utalii ni uhifadhi si vinginevyo.
Hata hivyo alitahadharisha kuwa huenda shirika hilo likafungwa
katika siku zijazo kutokana na mifumo mipya iliyopo ambayo lengo lake
halilengi kuendeleza shirika bali kusababisha mwingiliano wa
kiutendaji na kudhoofisha uwajibikaji kwa kuwa mfumo uliopo, hauko kwa
ajili ya maslahi ya shirika hilo.
juu
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment