Serengeti:
WAKAZI wanne kutoka wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha
wamehukumiwa na mahakama ya wilaya ya
Serengeti kifungo cha miezi sita jela
ama kulipa faini ya sh,120,000 kila mmoja kwa kosa la kuingia hifadhi ya taifa ya Serengeti bila
kibali.
Waliohukumiwa na mahakama hiyo ni Ndotei Sundi(30)Siatoi Warukwar(19) Kitupe Lesiani
(30)wakazi wa kijiji cha Warbai na Daud Kesoi(19)mkazi wa kijiji cha Maranja Ngorongoro ambao walikosa fedha na kuamriwa
kwenda gerezani.
walitenda kosa hilo
oktoba 23 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana.
Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Franco Kiswaga , Mwendesha mashitaka wa polisi sajenti Paskael Nkenyenge alidai oktoba 23 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana askari wa hifadhi hiyo wakiwa doria eneo la
Naabi waliwakamata washitakiwa hao na hawakuwa na kibali cha kuingia hifadhini.
Washitakiwa wote walikiri shitaka la kuingia hifadhini bila
kibali na kuilazimu mahakama hiyo kutoa adhabu kulingana na kosa walilotenda.
Akitoa hukumu Hakimu Kiswaga ameiambia mahakama kuwa
kufuatia washitakiwa kukiri shitaka bila kuisumbua mahakama ,anawahukumu kila mmoja kulipa faini ya shilingi 120,000 ama kutumikia kifungo cha miezi sita jela ili
iwe onyo kwa wenye tabia kama hiyo .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment