Jumamosi,
Octoba 26, 2013 07:20 Na Pendo Fundisha, Mbeya
KAMATI ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, imesema Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha ni kiini cha mgogoro wa ardhi unaoendelea katika Bonde la Ihefu kutokana
na kumega maeneo yasiyoainishwa na kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya
(RCC). Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James
Lembeli, katika ziara ya kukagua shughuli na miradi ya Serikali.
Alisema kikao cha RCC ndicho kilipaswa kuyaingiza maeneo hayo au kutoyaingiza ndipo hifadhi hiyo ingetekeleza majukumu yake ya kuweka mipaka.
Alisema eneo lililoongezwa na hifadhi hiyo ni kutoka kilomita 10,000 za mraba hadi kufikia kilomita 20,000 za mraba ambazo hazikuainishwa katika kikao cha RCC.
Aidha, imeitaka Serikali kutoa majibu haraka ya tume zilizoundwa kwa ajili ya kuchunguza mgogoro wa mpaka baina ya wananchi wa vijiji hivyo na hifadhi hiyo.
“Serikali iliunda tume mbalimbali za kuchunguza tatizo hili ikiwamo timu ya wataalamu iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Hivyo ni vema ikaharakisha kutoa majibu kwa kuwa muda mrefu umepita pasipo kusema lolote lile,” alisema Lembeli.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, alisema mgogoro huo upo njiani kumalizika kwa kuwa suluhisho lake limefika katika ngazi za mwisho.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Martin Loibooki, alisema jambo hilo limechukua muda mrefu baada ya kuwapo kwa mkanganyiko juu ya uwekaji wa mipaka hiyo, ambapo kuna wananchi walipeleka kesi hiyo mahakamani kuwa walipunjwa fidia zao.

No comments:
Post a Comment