Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Posted Alhamisi,Mei1 2014
Posted Alhamisi,Mei1 2014
Kwa ufupi
Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo
zimeeleza kuwa watendaji wote waliokuwa wamesimamishwa kazi wamerejeshwa na
katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi.
Dar es Salaam. Agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu la
kuwasimamisha kazi vigogo wa Idara ya Wanyamapori kwa kwenda kinyume na maadili
ya kazi limetenguliwa baada wakurugenzi hao kurejeshwa katika nyadhifa zao.
Februari mwaka huu, Waziri Nyalandu
alimsimamisha mkurugenzi wa wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na
mkurugenzi msaidizi wa matumizi endelevu ya wanyamapori, Jafari Kidegesho,
ikiwa ni utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Bunge Desemba 22 mwaka jana,
iliyotaka Serikali kuwawajibisha watendaji waliozembea kwenye Operesheni
Tokomeza Ujangili.
Taarifa kutoka ndani ya wizara hiyo
zimeeleza kuwa watendaji wote waliokuwa wamesimamishwa kazi wamerejeshwa na
katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi.
Alipotafutwa kwa njia ya simu katibu
mkuu huyo hakuonyesha ushirikiano baada ya kugundua anaongea na mwandishi badala
yake alibaki kusema: “Halooo..halooo…halooo” na hata alipotumiwa ujumbe mfupi
wa maandishi hakujibu.
Hata alivyoendelea kupigiwa simu
aliamua kumpa mwanaume apokee simu hiyo ambaye naye aliendelee kusema hasikii
ingawa alikuwa akisikika vyema.
Kwa upande wake Profesa Songorwa
alipotafutwa ali thibitisha kwamba ni kweli yupo kazini.
Kwa upande wake Kidegesho alisema
yuko Morogoro akiendelea na vipindi Chuo Kikuu cha cha SUA lakini amesikia
taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment