Wednesday, February 27, 2013

MATUKIO MBALIMBALI SIKU TANZANIA ILIPOIBUKA KIDEDEA MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA ,FEBRUARI 11,2013

 WAZIRI WA UTALII NA MALIASILI BALOZI KHAMISI KAGASHEKI AKITOA UFAFANUZI KWA WAANDISHI WA HABARI NJE YA UKUMBI WA MOUNT MERU HOTEL JIJINI ARUSHA  JINSI WIZARA HIYO IMEJIPANGA KUKABILIANANA WIMBI LA UJANGILI
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIKABIDHI ZAWADI KWA RAIS WA SHIRIKA LILILOKUWA LIMEANDAA MASHINDANO YA MAAJABU SABA YA VIVUTIO VYA ASILI AFRIKA DK,PHILIP IMLER

ZAWADI NYINGINE ALIYOPEWA NI PICHA YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI YENYE MAAJABU AMBAYO HAYAPATIKANI POPOTE DUNIANI KUTOKANA NA WANYAMA AINA NYUMBU KUHAMA KWA IDADI KUBWA KWENDA MASAAI MARA KISHA KUREJEA KWA KUVUKA MTO MARA NA KUJA KUZALIANA TANZANIA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA,WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII WA UGANDA KUSHOTO KWAKE ,DKIMLE NA MKEWE ,WAZIRI KAGASHEKI NA BAADHI YA VIONGOZI WAANDANMIZI WA TANAPA

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIKABIDHI TUZO KWA KAIMU MHIFADHI WA NGORONGORO BAADA YA KUIBUKA KUWA MIONGONI MWA VIVUTIO VYA MAAJABU SABA YA AFRIKA.

KUTOKA KUSHOTO NI MHIFADHI MKUU WA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI,KATIKATI  NI MKURUGENZI WA UTALII TANAPA MARTIN LOIBOOKI  NA MTANGO MTAHIKO WOTE WAMEWAHI KUONGOZA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

MABALOZI MBALIMBALI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

MKURUGENZI MKUU WA TANAPA ALLAN KIJAZI AKINYANYUA JUU TUZO YA USHINDI WA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI AMBAPO TANZANIA ILIIBUKA KIDEDEA KWA VIVUTIO VYA MLIMA KILIMANJARO,BONDE LA  NGORONGORO NA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI KUSHINDA MAAJABU SABA YA ASILI AFRIKA.
WAZIRI KAGASHEKI AKITETA JAMBO NA DK.IMLER

I
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIKABIDHI TUZO KWA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII WA UGANDA BAADA YA KIVUTIO CHA MTO NILE KUWA MIONGONI MWA MAAJABU SSABA YA AFRIKA.

Monday, February 25, 2013

MSIMU WA NYUMBU KUZALIANA KWAWAVUTA WATALII NA WATAFITI HIFADHI YA SERENGETI.I



.MAAJABU YA NYUMBU SERENGETI YAZIDI KUWAVUTA WATALII

WATALII na watafiti 16,500 wa masuala ya wanyamapori kutoka mataifa mbalimbali duniani wamefurika katika Hifadhi ya Taifa Serengeti, kushuhudia tukio la aina yake la nyumbu zaidi ya 8,000 kuzaliwa kwa siku, katika kipindi cha wiki sita.

Nyumbu hawa, wameanza kuzaliwa mapema mwezi huu na baada ya wiki sita wanatarajiwa kuzaliwa 500,000 lakini kati ya hao, karibu nusu yao, huliwa na wanyama wengine, wakiwapo simba, fisi na mamba kabla ya kukua huku wengine wakifa kutokana na kupotezana na wazazi wao.

Hifadhi hiyo yenye zaidi ya nyumbu 1.5 milioni, ina jumla ya simba 3,000 na fisi 7,500 ambao ndio walaji wakubwa wa nyama katika hifadhi hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya watalii hao, toka nchini Ubelgiji, Uingereza, Marekani na Ufaransa, walieleza kuvutiwa na tukio hilo, waliloliita kama “The Great Migration” .

Robert Joseph Raia wa Ubelgiji alisema, wamevutiwa sana na tukio la idadi kubwa ya nyumbu kuzaa kwa wakati mmoja.

“Ni tukio la ajabu duniani kila siku hapa nyumbu zaidi ya 8,000 wanazaliwa na watoto baada tu ya kuzaliwa dakika tano hadi nne,wanatembea”anasema.

Nicky Johnson raia wa Ufaransa, anaeleza kuwa, huu ni mwaka wake wa kwanza kufika Tanzania na Serengeti na alikuwa akiona kwenye mikanda ya video tukio la nyumbu zaidi ya 1.5 milioni kuhama na baadaye wakiwa Serengeti wanavyozaa na kuendelea na safari yao.
“Hili ni tukio zuri, sikuwahi kuliona sehemu yoyote duniani,hili ni jambo la ajabu , Tanzania mnapaswa kujivunia kwa tukio hili”alisema Jonson.

Mkuu wa Idara ya Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Godson Kimaro alisema tofauti na miaka ya nyuma mwaka huu kuanzia Februari Mosi hadi Februari 24, jumla ya watalii 10,621 toka nje ya nchi wamefika Serengeti kushuhudia nyumbu wakizaliwa.

Kimaro alisema katika kipindi hiki pia kuna Watanzania 5,815 wametembelea hifadhi, ikiwa pia ni ongezeko la zaidi ya asilimia 50 katika kipindi kingine.

Naye Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete alisema Tanapa kuanzia mwaka jana, imeanza kulitangaza kimataifa tukio la nyumbu kuingia nchini, kuzaliana na kuondoka ili kuwavutia watalii.
Shelutete alitoa mwito kufika kuona maajabu hayo.

Hifadhi hiyo yenye zaidi ya nyumbu 1.5 milioni, ina jumla ya simba 3,000 na fisi 7,500 ambao ndio walaji wakubwa wa nyama katika hifadhi hiyo
Mwisho. 

Friday, February 22, 2013

BURUDANI KUTOKA KWA WASANII KWA WAGENI WALIOHUDHURIA HAFLA YA KUTANGAZWA KWA MAAJABU YA ASILI AFRIKA

WASANII WAKIBURUDISHA WAGENI KABLA YA MGENI RASMI WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA HAJATANGAZA VIVUTIO VYAASILI AFRIKA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA MOUNT MERU JIJINI ARUSHA FEB,11,2013


MATUKIO SIKU YA KUTANGAZA MAAJABU YA VIVUTIO SABA VYA ASILI AFRIKA

BAADHI YA WAGENI WAKIWEMO MABALOZI KUTOKA NCHI MBALIMBALI WAKIFUATILIA BURUDANI ZA ASILI ZIKIONGOZWA NA MRISHO MPOTTO