Uchunguzi
huo ulibaini kuwa vinasaba vya pembe hizo vilifanana, hivyo kujenga dhana
kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiwinda katika hifadhi hiyo mara kwa mara
katika utaratibu maalumu unaotambuliwa na Serikali.PICHA|MAKTABA
Na Peter Elias, Mwananchi
Posted Jumatano,Aprili30 2014 saa 24:0 AM
Posted Jumatano,Aprili30 2014 saa 24:0 AM
Kwa
ufupi
Ripoti
hiyo inafafanua kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), katika tani 11 za pembe za
ndovu zilizokamatwa Taiwan, Japan na Hong Kong mwaka 2006, ilibainika kuwa
pembe 1,500 zilitoka Tanzania (Selous).
Dar
es Salaam. Ongezeko la kasi ya ujangili nchini
limedaiwa kusababishwa na vitendo vya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na
mfumo dhaifu wa usimamizi wa sheria katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kwa
mujibu wa ripoti iliyopewa jina la Urasimishaji wa Ujangili wa Kitaalamu
Afrika, tangu mwaka 2000 wizara hiyo imejikuta katika kashfa za rushwa na kusababisha
mawaziri na watendaji wakuu kuvuliwa nyadhifa zao.
Katika
ripoti hiyo, Taasisi ya Kimarekani ya Utunzaji Wanyamapori ya Born Free USA kwa
ushirikiano na Shirika la Ripoti za Kichambuzi na Takwimu la C4ADS, imeeleza
pia jinsi vikundi vya waasi barani Afrika wanavyoendesha shughuli za ujangili.
Ripoti
hiyo iliyozinduliwa mwezi huu nchini Kenya, inaitaja Tanzania kama kitovu cha
kusafirisha pembe za ndovu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bandari ya Dar
es Salaam imekuwa ikishindana na ile ya Mombasa katika kutumia bandari
kibiashara.
Kutoka
mwaka 2008 mpaka 2013, inaelezwa zaidi ya tani 20 za pembe za ndovu ama
zilikamatwa zikisafirishwa kuingia au kutolewa katika Jiji la Dar es Salaam,
hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya C4ADS.
Ripoti
hiyo inafafanua kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), katika tani 11 za pembe za
ndovu zilizokamatwa Taiwan, Japan na Hong Kong mwaka 2006, ilibainika kuwa
pembe 1,500 zilitoka Tanzania (Selous).
Uchunguzi
huo ulibaini kuwa vinasaba vya pembe hizo vilifanana, hivyo kujenga dhana
kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiwinda katika hifadhi hiyo mara kwa mara
katika utaratibu maalumu unaotambuliwa na Serikali.
“Kuna
udhaifu mkubwa katika usimamizi wa uwindaji halali na wawindaji wenye vibali
hawasimamiwi ipasavyo kufanya uwindaji kwa taratibu zilizowekwa kisheria. Hivyo
hutumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya ujangili,” inasema sehemu ya ripoti
hiyo.
Serikali
yakanusha
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Paul Sarakikya alikanusha madai hayo akisema
siyo kweli kwamba wawindaji halali huachwa bila usimamizi, bali wana mifumo ya
kusimamia shughuli hiyo.
“Sikubaliani
na ripoti hiyo, tumeshaongea sana juu ya suala hili, Rais alishalizungumzia na
waziri pia. Ufafanuzi ndio huo, hamna ukweli wowote katika ripoti hiyo,” alisisitiza
Sarakikya.
Salakikya
alisema idadi ya tembo nchini inazidi kuongezeka katika hifadhi tofauti na
upungufu unaoelezwa katika ripoti hiyo.
Mkurugenzi huyo alihoji kuwa kama hakuna
usimamizi madhubuti katika uwindaji halali, wamewezaje kusimamia uwindaji miaka
yote mpaka idadi ya tembo inaongezeka, baada ya upungufu uliokuwepo miaka ya
nyuma.
Wakati Sarakikya akisema tembo wanaongezeka,
ripoti hiyo inaeleza kuwa idadi ya tembo katika hifadhi za Selous na Mikumi kwa
mwaka 1976, ilikuwa ni 109,419 lakini kufikia mwaka 2009, idadi hiyo ilishuka
hadi kufikia tembo 38,975.
Nchi zilizoathirika zaidi na ujangili barani
Afrika, zinatajwa kuwa ni Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), Cameroon, Msumbiji, Kenya, Zimbabwe na Tanzania ambayo pia
inatajwa kuwa kitovu cha usafirishaji wa pembe za ndovu.
Idadi ya tembo waliosalia
Na kwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Frankfurt
Zoological Society mwishoni mwa mwaka 2013, ripoti hiyo inaeleza kuwa ni tembo
13,084 wanaokadiriwa kusalia katika hifadhi, sawa na upungufu wa asilimia 66
katika kipindi cha miaka minne tangu 2009.
Hii imefafanuliwa kuwa zaidi ya tembo 25,000
waliuawa katika Hifadhi ya Selous ndani ya miaka minne pekee. Pia, ripoti hiyo
inabainisha upungufu wa tembo katika hifadhi ya Ruaha-Rungwa kutoka tembo
35,461 mpaka tembo 20,090 sawa na upungufu wa asilimia 36.5 kuanzia mwaka 1990
mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment