Sunday, September 16, 2012

Pigia kura vivutio vyetu; sevennaturalwonders.org


Tumia fursa hii kupigia kura vivutio vya Tanzania ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili ya bara la Afrika. Vivutio vya Tanzania vinavyoshindanishwa na vingine tisa (9) barani Afrika ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na hifadhi ya Serengeti.
Tembelea sevennaturalwonders.org na upigekura yako.

www.tanzaniatouristboard.com

www.tanzaniatouristboard.com

Pimbi

Pimbi akiwa amepumzika katika Kituo cha Utalii Soronera kwenye Hifadhi ya Serengeti

Watalii

Watalii wakisoma taarifa mbalimbali katika kituo cha kupumzikia kilichopo kwenye Hifadhi ya Serengeti

TTB yawataka Watanzania kupigia kura vivutio

BODI ya Utalii nchini,(TTB) imewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi, kupigia kura
vivutio vitatu vya utalii nchini, ambavyo vimeingizwa katika mashindano ya
maajabu saba ya asili barani Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika mapokezi ya wanyama aina ya Nyumbu, ambao
wanarejea katika hifadhi ya Serengeti wakitokea hifadhi ya Masai Mara nchini
Kenya, Afisa uhusiano Mkuu wa TTB, Geofrey Tengeneza alisema, vivutio vitatu
ambavyo vimeingizwa katika mashindano ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,Mlima
Kilimanjaro na Hifadhi ya Ngorongoro.
Tengeneza alisema, tofauti ya shindano lililopita la maajabu saba ya asili ya dunia
ambayo, Tanzania haikufanya vizuri, shindano la sasa watu, watapiga kura kwa
kutumia mitandao.
“Tayari upigaji kura umeanza na utakamilika mwezi Desemba, safari hii tumeanza mapema
kuhamasisha ili watanzania  wengi wajitokeze kupiga kura ambapo pia katika upigaji kura wanaweza kuvipigia vivutio vingine vine ambavyo wanavijua, sambamba na hivi vitatu”alisema
Tengeneza.
Alisema katika shindano hilo, kuna maajabu 12 ya asili ambayo yanashindanishwa na
Tanzania pekee,imeingiza maajabu matatu katika shindano hilo.
Akizungumzia mapokezi ya nyumbu zaidi 1.5 milioni ambao wanarejea Serengeti, alisema tukio
hilo ni la aina yake duniani na linatoa nafasi kubwa kwa hifadhi hiyo, kuwa
kivutio cha asili duniani na kuwa na sifa ya kipekee kushinda katika maajabu
saba ya asili barani Afrika.
“Leo tunashuhudia idadi kubwa ya Nyumbu wakiwa wanarejea Serengeti katika mzunguko
wao wa asili, hili ni tukio la kipekee duniani ambalo linafuatiliwa na idadi
kubwa ya wadau wa utalii”alisema Tengeneza.
Awali Meneja uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete alisema kurejea wa nyumbu Serengeti
kunathibitisha kuwa wanyama hao nyumbani kwao ni Tanzania kwani wamekaa
Hifadhi ya Masai Mara kwa wiki tatu tu.
“Nyumbu na wanyama wengine wanaoandamana nao, sasa wanarejea Serengeti baada ya kutoka
mapumziko Hifadhi ya Masai Mara na hii inathibitisha kuwa wanyama hawa nyumbani
kwao ni Tanzania,”alisema Shelutete.
Mamia ya watalii toka ndani ya nchi kwa wiki moja sasa wamekuwa wakishuhudia maelfu
ya nyumbu wakirejea nchini kupitia Mto Mara ambao una maji yanayokwenda kwa kasi na mamba ambao hutumia kipindi hiki pia kujipatia chakula cha uhakika.