Sunday, March 30, 2014

Meno ya tembo ya mil. 120/- yanaswa Ifakara



Na Beatrice Shayo
30th March 2014
Maofisa wanyamapori mjini Ifakara mkoani Morogoro wamekamata vipande 14 vya meno ya tembo pamoja na meno mengine mazima  manne  yote yakiwa na  thamani ya Shilingi  milioni 120.

Katika kamata hiyo, mtuhumiwa  Sudi Nyumbi  mfanyabashara wa jijini Dar es Salaam, alinaswa akiwa katika kijiji cha Katindiuka wilayani Kilombero akiwa   na vipande 14 vya meno  hayo yenye thamani ya Sh. 72,000,000 na  manne yenye thamani ya sh 48,000,000.

Akizungumza na NIPASHE wakati wa mahojiano,  Afisa wa Wanyamapori Kilombeo, Madaraka Amani alisema mtuhumiwa alinaswa  Jumanne  wiki hii  wakati huo akitoka ndani ya lango la kizuizi cha ukaguzi  la Kidatu akielekea Dar es Salaam.

Amani alisema askari wa wanyapori waliokuwa kwenye doria kijiji cha Katindiuka waliwaona watu wawili wakiwa kwenye baiskeli na walipokuwa wakiwafuatilia walikimbia na kuitelekeza baiskeli pamoja na meno hayo manne.

Hata hivyo, alisema meno hayo manne inaonyesha kuwa yalikuwa yamechimbiwa  ardhini  na kwamba walikwenda kuyafukua. Aliongeza kuwa kabla ya oparesheni tokomeza ujangili ulikuwa umeshika kasi lakini baada ya kusimamishwa unaanza tena.

Ofisa tarafa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema wanafanya juhudi za kupambana na ujangili ila tatizo lililopo ni kukosekana kwa ushirikiano  kesi zinapokuwa mahakamani.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


Saturday, March 29, 2014

MAJANGILI WAFANYA KUFURU HIFADHI YA WAMIMBIKI




Marchi 29, 2014

Kitaifa

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1596858/data/44/-/27fot7/-/digg.gifhttp://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1596860/data/45/-/sfurme/-/facebook.gifhttp://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1596862/data/46/-/15d1xeqz/-/delicious.gifhttp://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1596864/data/47/-/reuipkz/-/stumble.gifhttp://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/1596866/data/48/-/ego41ez/-/yahoo.gif

Bottom of Form
“Mwaka 1997 kulikuwa na wanyamapori 7,000 katika hifadhi hiyo na kwamba kutokana na usimamizi mzuri mwaka 2010 wanyama waliongezeka hadi kufikia 32,000 tembo wakiwamo,”.PICHA|MAKTABA


Posted Marchi29 2014 saa 9:39 AM
Kwa ufupi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida askari huyo anakiri kuwa wanasiasa ni tatizo kubwa kwenye eneo hilo, wamefikia hatua ya kufungua matawi ya vyama vyao ndani ya hifadhi kwa kuwa kuna watu wamevamia na kufanya makazi.
Dar es Salaam. Wanyamapori wakiwamo tembo katika Hifadhi ya Wami Mbiki wapo hatarini kutoweka, kutokana na kasi ya vitendo vya ujangili.
Mbali ya ujangili wa wanyamapori, pia ukataji miti kwa ajili ya uchomaji mkaa, na ufugaji wa mifugo ndani ya eneo hilo, ni vitendo vinavyozidi kuongezeka na kutishia kutoweka kwa hifadhi hiyo.
Eneo hilo linaundwa na vijiji 24, wilaya tatu za mikoa ya Morogoro na Pwani, ambapo vijiji vitatu viko Wilaya ya Morogoro, Mvomero vijiji(8), 13 ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, liko kati ya Morogoro, Chalinze, Mbewe, Kanga, Turiani na Wami Dakawa.
Wilaya ya Morogoro, Mvomero vijiji(8), 13 ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, liko kati ya Morogoro, Chalinze, Mbewe, Kanga, Turiani na Wami Dakawa.
Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa ujangili wa wanyama katika hifadhi hiyo huendeshwa kwa kutumia magari, pikipiki, mbwa, mitego ambayo husambazwa eneo kubwa, huku bunduki aina ya gobori na za kivita zikitumiwa kwa ajili kuua wanyama wakubwa kama vile tembo.
Gazeti hili limebaini kuwa wanyama kama simba, chui na mbwa mwitu huuawa kwa sumu ili kukinga mifugo iliyohamishiwa ndani ya eneo hilo isiliwe, huku tembo wakiuawa kwa bunduki na sumu ili kupata meno yake.
Kutokana na kuwapo kasi kubwa ya ujangili na uharibifu wa mazingira katika hifadhi hiyo, idadi ya wanyama inapungua kwa kasi.
Taarifa ya watafiti ya mwaka jana kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Teps, inaeleza kuwa hali hiyo ilianza kuwa mbaya zaidi kwa kipindi cha 2010-2013 baada ya kukosa ufadhili kutoka nje na kwamba hata mikataba ya wafanyakazi wa hifadhi hiyo iliisha mwaka 2010 na kukosekana kwa doria.
Pamoja na malori kusomba tani za mkaa kutoka ndani ya pori hilo, hakuna hatua zinazochukuliwa na uongozi wa halmashauri na wizara husika.
Inakadiriwa wanyama zaidi ya 15,000 wamehama ama kuwindwa kwa kipindi cha miaka miwili na eneo limegeuzwa kuwa ranchi ya mifugo na kulimwa ekari za maelfu ya mazao ya mahindi na mpunga ndani ya hifadhi.
Dk. Alfred Kikoti
Dk. Alfred Kikoti ambaye alishiriki katika utafiti huo aliliambia gazeti hili kuwa tangu mwaka 1997 kulikuwa na wanyama 7,000, na waliongezeka hadi kufikia 32,000 mwaka 2010.
“Mwaka 1997 kulikuwa na wanyamapori 7,000 katika hifadhi hiyo na kwamba kutokana na usimamizi mzuri mwaka 2010 wanyama waliongezeka hadi kufikia 32,000 tembo wakiwamo,”alisema.
Dk. Kikoti alisema hadi kufikia mwaka 2010-2013, tembo katika hifadhi hiyo wamebaki 150 kati ya 350 na wengi wanahama kutokana na kukosa mazingira rafiki.
Alisema eneo hilo ni muhimu kiikolojia kwa kuwa huwaunganisha wanyama kutoka Sadani, Mikumi na Selou kwa kuwa maji hayakauki, kuliacha mikononi mwa majangili ni kuua uhifadhi hapa nchini.
“Eneo hili ni kubwa sana na huwezi kupata eneo ambalo linaunganisha maeneo makubwa ya nchi kama ilivyo kwa mikoa hiyo, wanyama kama tembo wanakwisha na wengine kwa kuwa wizara imejiweka pembeni,” alisema.
Mtafiti huyo alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ni chanzo cha maliasili hizo kutoweka kwa kuwa kuna wawekezaji walioomba kuweka faru ndani ya eneo hilo, hatua ambayo ingeimarisha ulinzi, lakini hawajawahi kujibu na wako kimya, huku wanyama, magogo na samaki wakiisha.
“Wizara haina mwitikio, ripoti zote za utafiti wanazo, hakuna asiyejua kuwa Wami Mbiki inakwisha, watu hawataki kuchukua majukumu yao,” alisema.
Mkuu wa askari
Furaha Mbwilo mkuu wa askari wa wanyamapori katika hifadhi hiyo, alisema ujangili umekuwa mkubwa ndani ya pori hilo ukifanywa na wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wakiwemo baadhi ya viongozi wa serikali.
Alisema: “Wizara ya Maliasili haisaidii kwa suala la ulinzi, ingawa awali walikuwa wanakuja mara moja, sasa humu kumekuwa ni shamba la bibi, maana majangili, wafugaji, wapasua mbao na wachoma mkaa wanajua kuwa hatuna gari, hatuwezi kufanya doria kwa mguu, wanavuna maliasili za taifa watakavyo.”
Mbwilo alisema kuwa kujitoa kwenye ufadhili kwa Shirika la Kimataifa la Danish Hunter Association(DHA), tangu mwaka 2011 ndiyo kumeongeza kasi ya ujangili.
Top of Form

Naibu Waziri aomba muda
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamod Mgimwa alisema hana taarifa na kuomba apewe siku mbili hadi tatu atakuwa amejua nini kinaendelea Wami Mbiki.
“Nashukuru sana kwa taarifa hii...naomba siku mbili, tatu nitakuwa na jibu...naomba muendelee kutusaidia kwenye sekta hii,”anasema



Friday, March 28, 2014

Mshtakiwa meno ya tembo ajidhamini mahakamani



Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Jumatano,Marchi26  2014  saa 11:9 AM
Kwa ufupi
  • Rebeca Julius Mwita (32) anakabiliwa na mashtaka matatu ya kukutwa na nyara hizo za Serikali zenye uzito wa kilo 46 zikiwa na thamani ya Sh39.5 milioni aliruhusiwa kujidhamini mwenyewe kinyume cha kifungu cha  148 (5)(c) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Mtuhumiwa anayeshtakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti kwa makosa ya kukutwa na meno ya tembo, ameruhusiwa kujidhamini mwenyewe, Mwananchi limebaini.
Rebeca Julius Mwita (32) anakabiliwa na mashtaka matatu ya kukutwa na nyara hizo za Serikali zenye uzito wa kilo 46 zikiwa na thamani ya Sh39.5 milioni aliruhusiwa kujidhamini mwenyewe kinyume cha kifungu cha  148 (5)(c) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.  Mwita alikamatwa Januari 17, 2013 na alifikishwa mahakamani siku nne baadaye, Januari 23 ambako alifunguliwa mashtaka manne ya kukutwa na meno ya tembo mawili na vipande vinne vya meno hayo, kinyume cha sheria.
 Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Amon Kahimba, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Anesius Kainunura alidai kuwa makosa yanayomkabili mshtakiwa ni kinyume cha Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya 2009 kifungu cha 4(d) jedwali la 1 na Kifungu cha 57 (1) na 60 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi iliyofanyiwa marekebisho 2002.
 Baada ya kusomewa mashtaka, mtuhumiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana hivyo alirejeshwa rumande hadi Februari 4, 2013 wakati kesi yake ilipotajwa kwa mara ya pili.    Masharti aliyopewa ni kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya maneno ya Sh1 milioni, kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja alipaswa kuweka bondi Sh2 milioni na sharti la tatu lilikuwa ni mdhamini mmojawapo kuwasilisha fedha taslimu Sh18 milioni.
Kesi hiyo iliendelea kutajwa bila mtuhumiwa kupata dhamana hadi Julai 9 na 23, 2013 wakati  wadhamini wawili ,akiwamo mume wake walijitokeza kumdhamini, lakini walishindwa licha ya kwamba wakati huo masharti yalikuwa yamelegezwa.
 Tofauti na masharti ya awali, kila mdhamini alitakiwa kutoa ahadi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh2 milioni pia mshtakiwa kujidhamini kwa fedha ya maandishi Sh500,000.
 Hakimu Kahimba aliwakataa wadhamini hao kwa maelezo kwamba hawakuwa na sifa, hivyo kuamuru mtuhumiwa arejeshwe rumande hadi Agosti 14, mwaka jana na kesi hiyo namba Eco.03/2013, ingetajwa kisha kusomwa kwa maelezo ya awali.
Dhamana ya ghafla
Katika hali isiyo ya kawaida, Julai 23, wakati waendesha mashtaka, karani na yeye (hakimu) akiwa ameshaandika tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo,  aliamuru shauri la mshtakiwa huyo lisomwe upya mahakamani.
 Uchunguzi umebaini kuwa baada ya shauri hilo kusomwa upya, Hakimu Kahimba aliruhusu Mwita ajidhamini mwenyewe kwa ahadi ya maandishi ya Sh500,000 na kuamriwa kufika mahakamani Agosti 14, 2013.
 Akizungumza na gazeti hili, Hakimu Kahimba alisema alitumia busara zaidi katika uamuzi wake, kutokana na mshtakiwa kukaa mahabusu kwa muda mrefu kwa kukosa wadhamini.
 “Mshtakiwa pamoja na kuomba alegezewe masharti ya dhamana...Bado alishindwa, kutokana na kukaa muda mrefu na uhakika wa kumpata upo....Wakati mwingine tunatumia hekima zaidi,” alisema Kahimba.
Hata hivyo, hakimu huyo alikiri kuwapo kwa matukio kadhaa ya watuhumiwa wanaoruka dhamana, huku chanzo kikubwa kikiwa ni kuwapa masharti nafuu yanayokinzana na hitaji la sheria kwa kesi za uhujumu uchumi.
 Mwendesha Mashtaka Mwandamizi Mkoa wa Mara, Lusekelo Samwel alisema uamuzi huo umekiuka kifungu cha 148 (5)(c) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA) 1985 (RE:2002) ambayo  inabainisha wazi masharti ya dhamana kwa makosa hayo.
 “Kwa kosa ambalo mshtakiwa atashtakiwa nalo likiwa na thamani inayozidi Sh10 milioni...mshtakiwa anatakiwa pamoja na masharti mengine kutoa fedha taslimu ambazo ni sawa na nusu ya thamani ya kiasi anachoshtakiwa nacho ama thamani ya mali isiyohamishika kama dhamana kwa mshtakiwa,” alisema Samuel.
 Naye Wakili Juma Thomas alisema: “Hakimu hawezi kulegeza masharti ya dhamana eti kwa sababu mshtakiwa ameomba, maana kwa haya makosa dhamana yake inaongozwa na sheria, hali ilivyo inatia shaka,” alisema Thomas.  Jana gazeti hili lilikuwa na habari inayohusu mahakama hiyo kutoa hukumu ambazo zinakiuka sheria, huku hakimu akidai kuwa wanazingatia haki za watu ambao huwa wamekaa mahabusu kwa muda mrefu.



Thursday, March 27, 2014

Utalii wa chakula unaweza kuchangia maendeleo ya uchumi



Na Charles Kayoka, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Marchi27  2014  saa 13:59 PM
Kwa ufupi
Katika dunia ya utandawazi jamii hushindwa kuuza utamaduni wao, na chakula na upishi vikiwa moja ya tamaduni hizi.
Moja ya udhaifu mkubwa wa utangazaji wa utalii ni kukosa ushirikishwaji wa sekta mbalimbali za uchumi wa nchi.
Kwa walio wengi utalii unafikiriwa katika ufinyu wake wa kiasili wa kwenda mbuga za wanyama na kutembelea magofu tu.
Ili utalii ukamilike, kuna vipengele kadhaa ambavyo lazima viende sawa kama vile vivutio vyenyewe, usafiri na huduma za utalii, malazi na chakula.
Ukiangalia blogu na tovuti nyingi Tanzania utagundua kuwa zinatangaza vivutio vyenyewe tu, tena vile vya asili, kwa ukubwa zaidi, lakini chakula hakionekani kama kuwa ni sehemu muhimu sana ya utalii.
Licha ya kuwa watalii wengi kiasili hutembelea mahali kutaka kuona, karibu wote hupendelea kujaribisha ladha mpya ya vyakula na upishi wa asili katika maeneo wanayotembelea, na kwa hiyo ni muhimu kuanza kufikiria uimarishaji wa utalii wa upishi.
Faida inakuwa kubwa sana. Kwanza chakula ni kitu ambacho kila mgeni hulazimika kutumia, ingawa watu hawapendi kuacha asili, lakini kwa vile utalii ni pamoja na kujaribu na kutenda ambayo huna fursa nayo unakotoka, kula chakula na mapishi ya kigeni ni sehemu ya furaha ya utalii.
Kwa kweli watalii wengi hutaka kujua na kujaribu vyakula vya wenyeji wao, kwenda kwenye maeneo ambayo watapata chakula cha kiasili, na pengine kujifunza kukipika wao wenyewe.
Kwa njia hiyo utalii unaweza kutumika kutangaza chakula na mapishi ya nchi wanazokwenda, kiasi cha kuwezesha kujenga mfumo wa mafunzo nje na ndani ya nchi.
Chakula ni utamaduni wa jamii. Watalii kula na kujifunza mapishi ya wenyeji ni kuutangaza utamaduni, na njia hiyo utalii wa chakula unaweza pia kuwa ni kuuuza utamaduni kwa wageni au nje ya nchi.
Katika dunia ya utandawazi jamii hushindwa kuuza utamaduni wao, na chakula na upishi vikiwa moja ya tamaduni hizi. Tunapokula vitafunwa kama burger, sandwitch, hotdogs, cheese rolls, croissants, na kadhalika, tunakuwa tunanunua utamaduni wa wageni, na wanajipatia fedha nyingi kutokana na uuzaji huo kwani lazima watakuwa wanapata mahitaji makubwa kutoka kwetu.
Kwa kuwa tunaununua utamaduni huo, wanapata fedha za kuanzisha mafunzo, matangazo na hatimaye tunafikiria kuwa kula vyakula vya huko ni bora zaidi.
Kumbe basi tukirahisisha na kuboresha upishi na matangazo ya vyakula vyetu, tunaweza kutengeneza chanzo cha mapato kwa wananchi wetu.
1 |
Nchi kadhaa duniani huwa na matukio ya kitaifa yanayohusisha chakula na hatimaye yamekuwa ni vivutio vya utalii. Hapa kwetu tumebuni matukio kama ya Siku ya Nyama Choma, Siku ya Vipapatio vya Kuku, lakini hayako endelevu na hayaoanishwi na utalii.
Aidha matukio ya minada ya nyama choma kama kule Arusha, Morogoro na Dodoma, bado hayajafikia ukubwa wa kiutalii, hata hivyo tunaweza kuanzia hapo.
Waliotembelea nchi za Ulaya watakubaliana na mimi kuwa matunda yaliyovunwa na kuuzwa kwa kutoka shambani moja kwa moja huwa ni bidhaa ghali sana, na wageni wanapokuja hapa kwa kweli matunda huwa ni moja ya vyakula wanavyopenda kununua kwa sababu yametoka shamba.

Uchambuzi
Hivi kweli Serikali haiwezi kupambana na majangili?

Na Boniface Meena

Posted  Alhamisi,Marchi27  2014  saa 13:18 PM
Kwa ufupi
Haiwezekani majangili wakaua hata wale vifaru ambao Rais Kikwete aliwapata Afrika Kusini na kuwawekea ulinzi, halafu tukasema majangili ni watu wa kawaida.

Tuna vita mikononi mwetu hivyo ni muhimu tutumie kila tulichonacho kupambana na kushinda vita hiyo.
Vita hiyo ni ujangili ambao umekithiri nchini Tanzania, ambako vitisho vingi vimetolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali za Serikali, lakini ujangili bado unaendelea kukithiri.
Majangili ni watu wa aina gani au ni maroboti? Ni lazima tuanze kujiuliza kwa kuwa haiwezekani wakawa binadamu wa kawaida ambao wanaweza kuishinda nguvu ya Serikali ambayo ina kila kitu cha kuweza kupambana nao.
Ripoti ya Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) iliyotolewa hivi karibuni inaeleza kuwa mwaka jana Tanzania ndiyo ilikuwa kinara au kitovu cha biashara ya meno ya tembo katika nchi za Afrika Mashariki.
Imeeleza kuwa takribani tembo 30 huuawa kila siku nchini na kufanya tembo 10,000 kuuawa kwa mwaka. Yaani tembo 30 huuawa kila siku na Serikali imekaa kimya ikipiga kelele kuwa itapambana na majangili kwa njia yoyote ile ili kukomesha tatizo hilo.
Serikali ina jeshi, ina polisi ina usalama wa taifa bado tembo 30 wanauawa kila siku na majangili ambao wamejengewa dhana kuwa wanaizidi “nguvu Serikali” na kufanya mauaji ya tembo na vifaru wakati wowote ule wanaojisikia.
Kwa jinsi hali ilivyo na inavyoendelea, inatia wasiwasi kuwa huenda majangili hao ni viongozi walioko Serikalini ambao hawawezi kudhibitiwa kwa njia yoyote ile au ndio wanaowalinda majangili kwa masilahi yao binafsi na familia zao. Nasema hivyo kwa kuwa ni aibu kwa Serikali kwenda kupiga domo Ulaya kuwa inapambana na ujangili nchini kwa nguvu zake zote, halafu tembo 30 wakawa wanaendelea kuuawa kila siku.
Haiwezekani majangili wakaua hata wale vifaru ambao Rais Kikwete aliwapata Afrika Kusini na kuwawekea ulinzi, halafu tukasema majangili ni watu wa kawaida.
Hapana! Hawa watu ni lazima watakuwa na mizizi mikubwa serikalini na kwenye vyombo vya usalama kiasi cha kuamua kufanya chochote, wakati wowote katika mbuga zetu za wanyama halafu kazi ya Serikali au wasimamizi wa mbuga iwe ni kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa majangili wameua tembo na kutoroka na meno yake.
Lazima kuna mkono wa mtu na ndiyo maana Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mabadiliko ya wakurugenzi hadi mawaziri, lakini bado ujangili unaendelea kukua kwa kasi badala ya kupungua.
Idadi ya tembo nchini imeendelea kupungua miaka ya karibuni hasa katika pori la akiba la Selous ambalo lilikuwa na kiasi cha tembo 70,000 mwaka 2006, lakini idadi hiyo imeendelea kupungua hadi tembo 39,000 mwaka 2009 na hivi sasa pori hilo linao tembo 13,084.
Iadi ya tembo katika mbuga ya Ruaha nako imepungua kwa asilimia 44 toka 2006 na hivi sasa inakadiriwa ina tembo 20, 090.
Tuna vita mikononi mwetu hivyo ni muhimu tutumie kila tulichonacho kupambana na kushinda vita hiyo.
Vita hiyo ni ujangili ambao umekithiri nchini Tanzania, ambako vitisho vingi vimetolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali za Serikali, lakini ujangili bado unaendelea kukithiri.
Majangili ni watu wa aina gani au ni maroboti? Ni lazima tuanze kujiuliza kwa kuwa haiwezekani wakawa binadamu wa kawaida ambao wanaweza kuishinda nguvu ya Serikali ambayo ina kila kitu cha kuweza kupambana nao.
Ripoti ya Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) iliyotolewa hivi karibuni inaeleza kuwa mwaka jana Tanzania ndiyo ilikuwa kinara au kitovu cha biashara ya meno ya tembo katika nchi za Afrika Mashariki.
Imeeleza kuwa takribani tembo 30 huuawa kila siku nchini na kufanya tembo 10,000 kuuawa kwa mwaka. Yaani tembo 30 huuawa kila siku na Serikali imekaa kimya ikipiga kelele kuwa itapambana na majangili kwa njia yoyote ile ili kukomesha tatizo hilo.
Serikali ina jeshi, ina polisi ina usalama wa taifa bado tembo 30 wanauawa kila siku na majangili ambao wamejengewa dhana kuwa wanaizidi “nguvu Serikali” na kufanya mauaji ya tembo na vifaru wakati wowote ule wanaojisikia.
Kwa jinsi hali ilivyo na inavyoendelea, inatia wasiwasi kuwa huenda majangili hao ni viongozi walioko Serikalini ambao hawawezi kudhibitiwa kwa njia yoyote ile au ndio wanaowalinda majangili kwa masilahi yao binafsi na familia zao. Nasema hivyo kwa kuwa ni aibu kwa Serikali kwenda kupiga domo Ulaya kuwa inapambana na ujangili nchini kwa nguvu zake zote, halafu tembo 30 wakawa wanaendelea kuuawa kila siku.
Haiwezekani majangili wakaua hata wale vifaru ambao Rais Kikwete aliwapata Afrika Kusini na kuwawekea ulinzi, halafu tukasema majangili ni watu wa kawaida.
Hapana! Hawa watu ni lazima watakuwa na mizizi mikubwa serikalini na kwenye vyombo vya usalama kiasi cha kuamua kufanya chochote, wakati wowote katika mbuga zetu za wanyama halafu kazi ya Serikali au wasimamizi wa mbuga iwe ni kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa majangili wameua tembo na kutoroka na meno yake.
Lazima kuna mkono wa mtu na ndiyo maana Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mabadiliko ya wakurugenzi hadi mawaziri, lakini bado ujangili unaendelea kukua kwa kasi badala ya kupungua.
Idadi ya tembo nchini imeendelea kupungua miaka ya karibuni hasa katika pori la akiba la Selous ambalo lilikuwa na kiasi cha tembo 70,000 mwaka 2006, lakini idadi hiyo imeendelea kupungua hadi tembo 39,000 mwaka 2009 na hivi sasa pori hilo linao tembo 13,084.
Iadi ya tembo katika mbuga ya Ruaha nako imepungua kwa asilimia 44 toka 2006 na hivi sasa inakadiriwa ina tembo 20, 090.