Lazaro Nyalandu
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Posted Ijumaa,Mei2 2014 saa 24:0 AM
Posted Ijumaa,Mei2 2014 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Alipoulizwa kuhusu suala hilo,
Nyalandu alikiri kumzuia Songorwa kujitambulisha: “Kwanza sikujua kama
angekuwapo katika kikao kile, maana suala lake bado hatujalizungumza ofisini.
Dar es Salaam. Hatua ya kurejeshwa kazini Mkurugenzi wa Wanyamapori,
Profesa Alexander Songorwa baada ya kutimuliwa kazi na Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu imeibua mapya baada ya mkurugenzi huyo kutimuliwa
katika Kamati ya Bunge jana.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira walikubaliana na pendekezo la Nyalandu kutaka Profesa
Songorwa asijitambulishe katika kikao cha kamati hiyo kwa kuwa hakuwa
anatambulika.
Sakata hilo lilitokea wakati kigogo
huyo na watendaji wengine walipokuwa wakijitambulisha kabla ya kuanza kwa kikao
cha kamati hiyo kilichokuwa kikijadili Bajeti ya Serikali mwaka 2014/15.
Februari mwaka huu, Profesa Songorwa
na Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Jafari Kidegesho
walisimamishwa kazi na Nyalandu akisema ni utekelezaji wa azimio la Bunge
katika Ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili.
Hata hivyo, watendaji hao,
walirejeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho
zilieleza kwamba baada ya Nyalandu kukataa kumtambua, wajumbe walimuunga mkono
wakisema nao hawamtambui kwa sababu hatua aliyochukuliwa ilitokana na uamuzi
uliofikiwa na Kamati ya Operesheni Tokomeza, ambayo ni sehemu ya Kamati hiyo ya
Bunge.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo,
Nyalandu alikiri kumzuia Songorwa kujitambulisha: “Kwanza sikujua kama
angekuwapo katika kikao kile, maana suala lake bado hatujalizungumza ofisini.
Sikuona sababu ya yeye kujitambulisha. Tukirejea ofisini tutalizungumza na kazi
zitaendelea kama kawaida, ila azimio la Bunge dhidi yake lipo wazi. Uamuzi
haurudi nyuma na itabidi apangiwe kazi nyingine.”
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James
Lembeli alishindwa kukiri wala kukataa kutokea kwa jambo hilo zaidi ya kusema
jambo hilo iulizwe Wizara ya Maliasili na Utalii.
Profesa Songorwa hakupatikana jana
kuzungumzia suala hilo na simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu.
No comments:
Post a Comment