Na Keku Lazaro, Mwananchi
Posted Jumatatu,Mei5 2014 saa 11:17 AM
Posted Jumatatu,Mei5 2014 saa 11:17 AM
Kwa ufupi
Imeelezwa kuwa hiyo inaonyesha
kwamba hali ya ujangili katika hifadhi mbalimbali nchini inaendelea na
kusababisha kupotea kwa wanyama hao.
Manyara. Tembo wanane katika Hifadhi
ya Tarangire mkoani hapa wameuawa katika kipindi cha Novemba 2013 hadi sasa
huku meno 17 ya tembo yakikamatwa katika operesheni inayoendelea kufanywa na
askari wa hifadhi hiyo.
Imeelezwa kuwa hiyo inaonyesha
kwamba hali ya ujangili katika hifadhi mbalimbali nchini inaendelea na
kusababisha kupotea kwa wanyama hao.
Mhifadhi mkuu wa Tarangire, Stefano
Qolli aliwaambia waandishi wa habari kuwa ujangili bado haujakoma.
Qolli alisema kuuawa kwa tembo hao
kunatokana na watu wanaodhaniwa kuwa ni majangili kutoka katika vijiji vya
jirani kuwawekea mitego mbalimbali tembo hao ikiwamo maboga yenye sumu na hali
hiyo imesababisha kupungua kwa idadi ya wanyama hao Tarangire.
Alitaja mbinu nyingine iliyoua tembo
hao wanane kuwa ni ile ya kuwatega kwa kamba.
Mbali na hayo alisema jumla ya meno
17 ya tembo yalikamatwa.
yalitokea katika vijiji vinne
ambavyo ni Kiteto,Kibao cha Manyara Ranch, Marangw, pamoja na Kondoa.
“Kupatikana kwa meno haya ya tembo
kunatokana na taarifa tulizopata kutoka kwa raia wema pamoja na askari wa
kikosi dhidi ya ujangili, lakini pia bado tunaendelea na jitihada za
kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika wanafikishwa katika vyombo vya dola,”
alisema mhifadhi huyo.
Kutokana na mauji hayo ya tembo
pamoja na meno yake jumla ya majangili 25 walikamatwa kwa kipindi cha November
2013 hadi sasa na tayari hatua za kisheria zimeshachukuliwa ikiwamo kufikishwa
mahakamani ingawaje kesi zao bado zinaendelea.
No comments:
Post a Comment