Thursday, March 27, 2014

Utalii wa chakula unaweza kuchangia maendeleo ya uchumi

Na Charles Kayoka, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Marchi27  2014  saa 13:59 PM
Kwa ufupi
Katika dunia ya utandawazi jamii hushindwa kuuza utamaduni wao, na chakula na upishi vikiwa moja ya tamaduni hizi.
Moja ya udhaifu mkubwa wa utangazaji wa utalii ni kukosa ushirikishwaji wa sekta mbalimbali za uchumi wa nchi.
Kwa walio wengi utalii unafikiriwa katika ufinyu wake wa kiasili wa kwenda mbuga za wanyama na kutembelea magofu tu.
Ili utalii ukamilike, kuna vipengele kadhaa ambavyo lazima viende sawa kama vile vivutio vyenyewe, usafiri na huduma za utalii, malazi na chakula.
Ukiangalia blogu na tovuti nyingi Tanzania utagundua kuwa zinatangaza vivutio vyenyewe tu, tena vile vya asili, kwa ukubwa zaidi, lakini chakula hakionekani kama kuwa ni sehemu muhimu sana ya utalii.
Licha ya kuwa watalii wengi kiasili hutembelea mahali kutaka kuona, karibu wote hupendelea kujaribisha ladha mpya ya vyakula na upishi wa asili katika maeneo wanayotembelea, na kwa hiyo ni muhimu kuanza kufikiria uimarishaji wa utalii wa upishi.
Faida inakuwa kubwa sana. Kwanza chakula ni kitu ambacho kila mgeni hulazimika kutumia, ingawa watu hawapendi kuacha asili, lakini kwa vile utalii ni pamoja na kujaribu na kutenda ambayo huna fursa nayo unakotoka, kula chakula na mapishi ya kigeni ni sehemu ya furaha ya utalii.
Kwa kweli watalii wengi hutaka kujua na kujaribu vyakula vya wenyeji wao, kwenda kwenye maeneo ambayo watapata chakula cha kiasili, na pengine kujifunza kukipika wao wenyewe.
Kwa njia hiyo utalii unaweza kutumika kutangaza chakula na mapishi ya nchi wanazokwenda, kiasi cha kuwezesha kujenga mfumo wa mafunzo nje na ndani ya nchi.
Chakula ni utamaduni wa jamii. Watalii kula na kujifunza mapishi ya wenyeji ni kuutangaza utamaduni, na njia hiyo utalii wa chakula unaweza pia kuwa ni kuuuza utamaduni kwa wageni au nje ya nchi.
Katika dunia ya utandawazi jamii hushindwa kuuza utamaduni wao, na chakula na upishi vikiwa moja ya tamaduni hizi. Tunapokula vitafunwa kama burger, sandwitch, hotdogs, cheese rolls, croissants, na kadhalika, tunakuwa tunanunua utamaduni wa wageni, na wanajipatia fedha nyingi kutokana na uuzaji huo kwani lazima watakuwa wanapata mahitaji makubwa kutoka kwetu.
Kwa kuwa tunaununua utamaduni huo, wanapata fedha za kuanzisha mafunzo, matangazo na hatimaye tunafikiria kuwa kula vyakula vya huko ni bora zaidi.
Kumbe basi tukirahisisha na kuboresha upishi na matangazo ya vyakula vyetu, tunaweza kutengeneza chanzo cha mapato kwa wananchi wetu.
1 |
Nchi kadhaa duniani huwa na matukio ya kitaifa yanayohusisha chakula na hatimaye yamekuwa ni vivutio vya utalii. Hapa kwetu tumebuni matukio kama ya Siku ya Nyama Choma, Siku ya Vipapatio vya Kuku, lakini hayako endelevu na hayaoanishwi na utalii.
Aidha matukio ya minada ya nyama choma kama kule Arusha, Morogoro na Dodoma, bado hayajafikia ukubwa wa kiutalii, hata hivyo tunaweza kuanzia hapo.
Waliotembelea nchi za Ulaya watakubaliana na mimi kuwa matunda yaliyovunwa na kuuzwa kwa kutoka shambani moja kwa moja huwa ni bidhaa ghali sana, na wageni wanapokuja hapa kwa kweli matunda huwa ni moja ya vyakula wanavyopenda kununua kwa sababu yametoka shamba.

Uchambuzi
Hivi kweli Serikali haiwezi kupambana na majangili?

Na Boniface Meena

Posted  Alhamisi,Marchi27  2014  saa 13:18 PM
Kwa ufupi
Haiwezekani majangili wakaua hata wale vifaru ambao Rais Kikwete aliwapata Afrika Kusini na kuwawekea ulinzi, halafu tukasema majangili ni watu wa kawaida.

Tuna vita mikononi mwetu hivyo ni muhimu tutumie kila tulichonacho kupambana na kushinda vita hiyo.
Vita hiyo ni ujangili ambao umekithiri nchini Tanzania, ambako vitisho vingi vimetolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali za Serikali, lakini ujangili bado unaendelea kukithiri.
Majangili ni watu wa aina gani au ni maroboti? Ni lazima tuanze kujiuliza kwa kuwa haiwezekani wakawa binadamu wa kawaida ambao wanaweza kuishinda nguvu ya Serikali ambayo ina kila kitu cha kuweza kupambana nao.
Ripoti ya Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) iliyotolewa hivi karibuni inaeleza kuwa mwaka jana Tanzania ndiyo ilikuwa kinara au kitovu cha biashara ya meno ya tembo katika nchi za Afrika Mashariki.
Imeeleza kuwa takribani tembo 30 huuawa kila siku nchini na kufanya tembo 10,000 kuuawa kwa mwaka. Yaani tembo 30 huuawa kila siku na Serikali imekaa kimya ikipiga kelele kuwa itapambana na majangili kwa njia yoyote ile ili kukomesha tatizo hilo.
Serikali ina jeshi, ina polisi ina usalama wa taifa bado tembo 30 wanauawa kila siku na majangili ambao wamejengewa dhana kuwa wanaizidi “nguvu Serikali” na kufanya mauaji ya tembo na vifaru wakati wowote ule wanaojisikia.
Kwa jinsi hali ilivyo na inavyoendelea, inatia wasiwasi kuwa huenda majangili hao ni viongozi walioko Serikalini ambao hawawezi kudhibitiwa kwa njia yoyote ile au ndio wanaowalinda majangili kwa masilahi yao binafsi na familia zao. Nasema hivyo kwa kuwa ni aibu kwa Serikali kwenda kupiga domo Ulaya kuwa inapambana na ujangili nchini kwa nguvu zake zote, halafu tembo 30 wakawa wanaendelea kuuawa kila siku.

Hapana! Hawa watu ni lazima watakuwa na mizizi mikubwa serikalini na kwenye vyombo vya usalama kiasi cha kuamua kufanya chochote, wakati wowote katika mbuga zetu za wanyama halafu kazi ya Serikali au wasimamizi wa mbuga iwe ni kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa majangili wameua tembo na kutoroka na meno yake.
Lazima kuna mkono wa mtu na ndiyo maana Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mabadiliko ya wakurugenzi hadi mawaziri, lakini bado ujangili unaendelea kukua kwa kasi badala ya kupungua.
Idadi ya tembo nchini imeendelea kupungua miaka ya karibuni hasa katika pori la akiba la Selous ambalo lilikuwa na kiasi cha tembo 70,000 mwaka 2006, lakini idadi hiyo imeendelea kupungua hadi tembo 39,000 mwaka 2009 na hivi sasa pori hilo linao tembo 13,084.
Iadi ya tembo katika mbuga ya Ruaha nako imepungua kwa asilimia 44 toka 2006 na hivi sasa inakadiriwa ina tembo 20, 090.

No comments:

Post a Comment