Marchi 29, 2014
Kitaifa
“Mwaka 1997 kulikuwa na
wanyamapori 7,000 katika hifadhi hiyo na kwamba kutokana na usimamizi mzuri
mwaka 2010 wanyama waliongezeka hadi kufikia 32,000 tembo
wakiwamo,”.PICHA|MAKTABA
Posted Marchi29 2014 saa 9:39 AM
Kwa ufupi
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida askari huyo anakiri kuwa wanasiasa ni tatizo kubwa
kwenye eneo hilo, wamefikia hatua ya kufungua matawi ya vyama vyao ndani ya
hifadhi kwa kuwa kuna watu wamevamia na kufanya makazi.
Dar
es Salaam.
Wanyamapori wakiwamo tembo katika Hifadhi ya Wami Mbiki wapo hatarini kutoweka,
kutokana na kasi ya vitendo vya ujangili.
Mbali ya ujangili wa
wanyamapori, pia ukataji miti kwa ajili ya uchomaji mkaa, na ufugaji wa mifugo
ndani ya eneo hilo, ni vitendo vinavyozidi kuongezeka na kutishia kutoweka kwa
hifadhi hiyo.
Eneo hilo linaundwa na
vijiji 24, wilaya tatu za mikoa ya Morogoro na Pwani, ambapo vijiji vitatu viko
Wilaya ya Morogoro, Mvomero vijiji(8), 13 ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, liko
kati ya Morogoro, Chalinze, Mbewe, Kanga, Turiani na Wami Dakawa.
Wilaya ya Morogoro,
Mvomero vijiji(8), 13 ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, liko kati ya Morogoro,
Chalinze, Mbewe, Kanga, Turiani na Wami Dakawa.
Uchunguzi wetu unaonyesha
kuwa ujangili wa wanyama katika hifadhi hiyo huendeshwa kwa kutumia magari,
pikipiki, mbwa, mitego ambayo husambazwa eneo kubwa, huku bunduki aina ya
gobori na za kivita zikitumiwa kwa ajili kuua wanyama wakubwa kama vile tembo.
Gazeti hili limebaini
kuwa wanyama kama simba, chui na mbwa mwitu huuawa kwa sumu ili kukinga mifugo
iliyohamishiwa ndani ya eneo hilo isiliwe, huku tembo wakiuawa kwa bunduki na
sumu ili kupata meno yake.
Kutokana na kuwapo kasi
kubwa ya ujangili na uharibifu wa mazingira katika hifadhi hiyo, idadi ya
wanyama inapungua kwa kasi.
Taarifa ya watafiti ya
mwaka jana kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Teps, inaeleza kuwa hali
hiyo ilianza kuwa mbaya zaidi kwa kipindi cha 2010-2013 baada ya kukosa
ufadhili kutoka nje na kwamba hata mikataba ya wafanyakazi wa hifadhi hiyo
iliisha mwaka 2010 na kukosekana kwa doria.
Pamoja na malori kusomba
tani za mkaa kutoka ndani ya pori hilo, hakuna hatua zinazochukuliwa na uongozi
wa halmashauri na wizara husika.
Inakadiriwa wanyama zaidi
ya 15,000 wamehama ama kuwindwa kwa kipindi cha miaka miwili na eneo limegeuzwa
kuwa ranchi ya mifugo na kulimwa ekari za maelfu ya mazao ya mahindi na mpunga
ndani ya hifadhi.
Dk. Alfred Kikoti
Dk. Alfred Kikoti ambaye
alishiriki katika utafiti huo aliliambia gazeti hili kuwa tangu mwaka 1997
kulikuwa na wanyama 7,000, na waliongezeka hadi kufikia 32,000 mwaka 2010.
“Mwaka 1997 kulikuwa na
wanyamapori 7,000 katika hifadhi hiyo na kwamba kutokana na usimamizi mzuri
mwaka 2010 wanyama waliongezeka hadi kufikia 32,000 tembo wakiwamo,”alisema.
Dk. Kikoti alisema hadi
kufikia mwaka 2010-2013, tembo katika hifadhi hiyo wamebaki 150 kati ya 350 na
wengi wanahama kutokana na kukosa mazingira rafiki.
Alisema eneo hilo ni
muhimu kiikolojia kwa kuwa huwaunganisha wanyama kutoka Sadani, Mikumi na Selou
kwa kuwa maji hayakauki, kuliacha mikononi mwa majangili ni kuua uhifadhi hapa
nchini.
“Eneo hili ni kubwa sana
na huwezi kupata eneo ambalo linaunganisha maeneo makubwa ya nchi kama ilivyo
kwa mikoa hiyo, wanyama kama tembo wanakwisha na wengine kwa kuwa wizara
imejiweka pembeni,” alisema.
Mtafiti huyo alisema
Wizara ya Maliasili na Utalii ni chanzo cha maliasili hizo kutoweka kwa kuwa kuna
wawekezaji walioomba kuweka faru ndani ya eneo hilo, hatua ambayo ingeimarisha
ulinzi, lakini hawajawahi kujibu na wako kimya, huku wanyama, magogo na samaki
wakiisha.
“Wizara haina mwitikio,
ripoti zote za utafiti wanazo, hakuna asiyejua kuwa Wami Mbiki inakwisha, watu
hawataki kuchukua majukumu yao,” alisema.
Mkuu wa askari
Furaha Mbwilo mkuu wa
askari wa wanyamapori katika hifadhi hiyo, alisema ujangili umekuwa mkubwa
ndani ya pori hilo ukifanywa na wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wakiwemo
baadhi ya viongozi wa serikali.
Alisema: “Wizara ya
Maliasili haisaidii kwa suala la ulinzi, ingawa awali walikuwa wanakuja mara
moja, sasa humu kumekuwa ni shamba la bibi, maana majangili, wafugaji, wapasua
mbao na wachoma mkaa wanajua kuwa hatuna gari, hatuwezi kufanya doria kwa mguu,
wanavuna maliasili za taifa watakavyo.”
Mbwilo alisema kuwa
kujitoa kwenye ufadhili kwa Shirika la Kimataifa la Danish Hunter
Association(DHA), tangu mwaka 2011 ndiyo kumeongeza kasi ya ujangili.
Naibu Waziri aomba muda
Akizungumza na gazeti
hili kwa njia ya simu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamod Mgimwa
alisema hana taarifa na kuomba apewe siku mbili hadi tatu atakuwa amejua nini
kinaendelea Wami Mbiki.
“Nashukuru sana kwa
taarifa hii...naomba siku mbili, tatu nitakuwa na jibu...naomba muendelee
kutusaidia kwenye sekta hii,”anasema
No comments:
Post a Comment