Saturday, September 28, 2013

JWTZ KUSAKA MAJANGILI WATEMBO NA FARU

                     
               Na Mwandishi wetu


RAIS Jakaya Kikwete ametangaza kuwa ataliamrisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuongoza mapambano dhidi ya ujangili wa tembo na faru na ukataji haramu wa miti kwa shughuli za biashara ambao umefikia kiwango kikubwa nchini.
Alisema kuwa sekta ya utalii nchini sasa imeanza kutishiwa na uvunaji wa wanyama hao na biashara haramu ya meno ya tembo na faru, na kwamba tishio hilo ni kubwa kwa sababu sekta hiyo inachangia kiasi cha asilimia 17 katika mapato ya taifa na inaajiri watu 300,000.
Rais Kikwete alitangaza uamuzi huo juzi wakati alipozungumza kwenye mkutano wa viongozi wa nchi na serikali kuhusu biashara haramu ya wanyama na bidhaa zake pamoja na biashara haramu ya bidhaa za miti na mbao jijini New York, Marekani.
Aliuambia mkutano huo, ulioandaliwa na Rais Ali Omar Bongo Ondimba wa Gabon na Serikali ya Ujerumani kwenye Makao Makao ya Umoja wa Mataifa kuwa mwaka 1960, Tanzania ilikuwa na tembo 350,000 lakini kutokana na ujangili idadi hiyo ilishuka hadi 110,000 ilipofika mwaka 2009.
Kuhusu faru, Rais Kikwete alisema kuwa mwaka 1974 walikuwepo 700 na sasa wako chini ya 100 kwa sababu ya vitendo vya kijangili.
“Katika miaka ya 1980 na 1990 wakati wa kilele cha ujangili katika mikonga ya wanyama, tulilazimika kutumia jeshi kutuliza hali hiyo. Tuliona matokeo mazuri na tulikuwa na utulivu wa aina fulani.
“Lakini katika miaka minne iliyopita, tumeshuhudia kuongezeka kwa vitendo vya ujangili kwa ari na kasi mpya. Kwa mfano kati ya mwaka 2010 na Julai, 2013, zaidi ya tembo 1,386 waliuawa nchini,” alisema.
Rais Kikwete aliongeza kuwa wamechukua hatua kali za kupambana na ujangili ikiwa ni pamoja na kurekebisha sera, sheria na kanuni.
Aliongeza kuwa wamesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa ya kupambana na ujangili huu.
“Vile vile, tumechukua hatua za kukamata majangili na hata kukamata silaha zinazotumika katika ujangili. Kati ya mwaka 2010 hadi katikati ya mwaka huu, majangili 5,189 wametiwa mbaroni na silaha 1,952 zimekamatwa.
“Isitoshe vipande 3,788 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 10,756 vilikamatwa nchini. Nimeamuru JWTZ kukabiliana na hali hiyo na naamini kuwa tutapata mafanikio makubwa zaidi katika operesheni inayoandaliwa,” alisema.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alisema kuwa mifuko ya hifadhi nchini itaendelea kuchangia maendeleo kwa kugharamia miradi mbalimbali, lakini kwa namna ya kuilinda ili serikali isije kuua ‘bata wa dhahabu anayetaga mayai ya dhahabu’.
Rais alisema kuwa misaada inayotolewa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani (MCC) ni ya aina yake duniani kwa sababu wanufaika wakubwa wanapewa uhuru wa kuamua ni miradi gani ndani ya nchi igharamiwe na misaada hiyo.
Vile vile, Rais Kikwete alizitaja sekta kubwa ambako wawekezaji kutoka Marekani wanaweza kuwekeza mitaji yao kama njia ya kuongeza uwekezaji wao katika Tanzania, na hivyo kusaidia kukuza kwa kasi zaidi uchumi wake.

Thursday, September 26, 2013

Tuesday, September 24, 2013

UJANGILI UDHIBITIWE


Tanzania ikomeshe ujangili’
                 na Lucy Ngowi -Tanzania Daima

UCHUMI wa Tanzania kwa kiasi kikubwa unategemea utalii wa wanyamapori, hivyo juhudi zinahitajika kukomesha ujangili.

Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songolwa, alisema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Tembo kitaifa alipokuwa akimwakilisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Alisema juhudi za haraka zinahitajika kuhakikisha ujangili unakoma.

“Nchi yetu kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea utalii, madini yakichimbwa wanaondoka nayo tunabaki na mashimo, tembo wakitunzwa vizuri wakazaliana wanabaki. Uchumi wetu umebebwa na wanyamapori, juhudi za makusudi zinahitajika kuokoa wanyama hao,” alisema.

Alisema ujangili unaoendelea hivi sasa nchini unasababishwa na wachache wenye uroho, hivyo Watanzania waikatae hali hii kwa kuipinga vikali.

Kwa mujibu wa Songolwa, kuna nchi zilizokuwa na tembo barani Afrika lakini hivi sasa hawana, hivyo Tanzania ikicheza muda si mrefu watatoweka.

Alizitaja nchi hizo kuwa ni Gambia, Swaziland, Burundi na Mauritania. Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na tembo wengi, inayoongoza ni Botswana.

MAMLAKA YA WANYAMAPORI


       Mamlaka kamili Idara ya Wanyamapori yaanzishwa
  na Asha Bani-TANZANIA DAIMA
     
WADAU na wanataaluma mbalimbali nchini wamekutana jijini Dar es Salaam na kujadili kuanzishwa mamlaka kamili ya kusimamia Idara ya Wanyamapori.
Akifungua mkutano huo jijini hapa mwishoni mwa wiki kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songolwa, alisema mamlaka hiyo inaanzishwa kuchukua baadhi ya majukumu ya Idara ya Wanyamapori, hasa usimamizi wa rasilimali ya wanyamapori.
Alisema uanzishwaji wa mamlaka hiyo utasaidia kuokoa wanyamapori walioko hatarini kutoweka kutokana na changamoto nyingi zinazotishia makazi na mazingira yao.
Prof. Songolwa alisema mfumo uliopo hivi sasa hauiwezeshi serikali kukabiliana na changamoto hizo, hivyo imeamua kubadilisha mfumo wa usimamizi na uendelezaji wa sekta ndogo ya wanyamapori kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi pamoja na matokeo yake.
Prof. Songolwa alisema Idara ya Wanyamapori ya sasa inafanya kazi za urekebu, uratibu na usimamizi wa rasilimali za wanyamapori. Hivyo uanzishwaji wa mamlaka mpya unalenga kutenganisha majukumu hayo.
Alisema katika utenganisho huo, Idara na Wizara kwa ujumla itabaki na majukumu mawili ambayo ni urekebu na uratibu huku mamlaka ikichukua jukumu la usimamizi wa rasilimali za wanyamapori.



Monday, September 23, 2013

WATUMISHI TANAPA KUCHUNGUZWA


Tanapa kuchunguza tuhuma za ujangili
Na Daniel Mjema na Ibrahim Yamola, Mwananchi

Kwa ufupi
  • Shelutete alisema kutokana na majangili kubuni mbinu mpya kila siku, shirika limeunda kikosi maalumu (Rapid  Response Team) kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu kwa haraka zaidi.
Arusha/Dar es Salaam. Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (Tanapa), limeanzisha uchunguzi dhidi ya baadhi ya watumishi wake wanaotajwa kuwapo katika mitandao ya ujangili wa wanyama wakiwamo tembo.

Meneja Uhusiano wa Tanapa, Paschal Shelutete aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, wale watakaothibitika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

“Tumepokea tuhuma dhidi ya baadhi ya watumishi wetu kujihusisha na mitandao ya ujangili na uchunguzi dhidi yao umeanza ukishirikisha vyombo vya kiuchunguzi,” alisema Shelutete.

Shelutete alisema, tatizo la ujangili ni la kimtandao ukishirikisha majangili wa kimataifa wanaotumia ushawishi wa fedha na silaha za kisasa katika kuua tembo kwa lengo la kujipatia vipusa. “Wapo watumishi wamejikuta wakishawishiwa kujiunga na mitandao ya ujangili jambo ambalo ni kinyume kabisa na maadili ya kazi na hawa wakibainika kwa kweli hatuna msalie mtume,” alisema.

Shelutete alisema kutokana na majangili kubuni mbinu mpya kila siku, shirika limeunda kikosi maalum (Rapid  Response Team) kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu kwa haraka zaidi.

Alisema uanzishwaji wa kikosi hiki umeonyesha mafanikio makubwa na kutoa mfano katika kipindi cha miezi sita iliyopita hakuna tembo aliyeuawa ndani ya Hifadhi za Manyara na Tarangire.

Shelutete alisema kwa miezi sita, majangili 1,116 walikamatwa katika hifadhi mbalimbali huku Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Senapa) pekee ikikamata majangili 248. 
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Tembo nchini yaliyoandaliwa na UDSM kitengo cha Taasisi ya Kutathimini Rasilimali, Profesa Alexander Songorwa alisema wananchi ni wadau muhimu katika kampeni ya kupambana na ujangili.

MAGEUZI TANAPA YAJA


HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA

TANAPA KUENDESHA MAFUNZO MAALUM KWA ASKARI WAKE

Jumla ya Askari mia moja (100) waliofuzu usaili wa awali wa ajira ya uaskari wanatarajiwa kuanza rasmi mafunzo maalum ya mbinu za medani kwa miezi mitatu katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu.
Askari watakaofuzu vema mafunzo hayo ndio watakaoajiriwa na shirika katika utaratibu mpya ulioanzishwa na shirika wa kuandaa mafunzo hayo kwa askari hawa waliopitia mafunzo ya uaskari katika Jeshi la Kujenga Taifa na Chuo cha Wanyamapori Pasiansi Mwanza.
Aidha, shirika linaendelea kuchunguza na kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na vitendo vya ujangili kwa kushirikisha vyombo vya dola. Uchunguzi bado unaendelea kufanyika kwa baadhi ya wafanyakazi na utakapopatikana ushahidi wa kisheria kwa wote wanaojihusisha na mitandao ya ujangili hatua kali za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa.
Mafanikio kadhaa yameweza kufikiwa na shirika katika kukabili ujangili ambapo uimarishwaji wa doria za magari na miguu pamoja na matumizi ya mbwa katika hifadhi nchini umepunguza kwa kiwango kikubwa vitendo hivi ambapo katika kipindi cha miezi sita iliyopita ujangili uliokuwa umeshika kasi katika Hifadhi za Tarangire na Ziwa Manyara uliweza kudhibitiwa kwa asilimia 100 ambapo hakuna tembo aliyeuawa ndani ya hifadhi hizo tangu

Thursday, September 19, 2013

INTEREJENSIA TANAPA YAOKOA TEMBO




Taarifa za kiitelijensia zinavyookoa tembo
Kwa ufupi
  • 419 Idadi ya tembo waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini.
  • 1,645Mbao zilizokamatwa baada ya kuibwa katika hifadhi  nchini
  • Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema-Moshi. 
Kinapa inatakiwa kutoaelimu zaidi ya ujasiriamali kwa jamii ili kuwapa uwezo wa kuanzisha miradi.
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa) ni moja ya hifadhi 16 nchini ambayo imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ujangili wa tembo ambao wamekuwa wakiuawa na wahalifu wanaotafuta vipusa.
Takwimu zilizotolewa na Mhifadhi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (Tanapa), Mtango Mtahiko zinaonyesha kati ya 2009 hadi 2012, wanyamapori 15,227 waliuawa ndani ya hifadhi hizo.
Kati ya wanyamapori hao, 419 ni tembo waliouawa katika hifadhi mbalimbali huku hifadhi ya Ruaha ikiongoza kwa tembo 131 kuuawa ikifuatiwa na Serengeti 92, Tarangire 53, Katavi 36 na Mikumi 30.
Mkuu wa Idara ya Ulinzi na Uokoaji Kinapa, Sebastian Gambares anasema ujangili wa tembo umepungua kwani mwaka 2012/2013 hakukuwa na tukio la kuuawa kwa tembo ndani ya hifadhi hiyo.
“Hata matukio ya nyuma ya kuuawa kwa tembo yalihusisha matukio ya kuuawa nje ya hifadhi, Kinapa tumekuwa makini sana katika kudhibiti Majangili,”anabainisha mhifadhi huyo.
Anasema wanapobaini kuwapo kwa tembo katika eneo fulani hasa tembo wanaotoka Hifadhi ya Amboseli nchini Kenya, basi kikosi cha kupambana na ujangili kinakuwapo karibu na maeneo hayo.
Naye Mkuu wa Hifadhi ya Kinapa, Kanda ya Kaskazini Magharibi, Imani Kikoti anasema moja ya mikakati iliyosaidia udhibiti wa ujangili ni kubadilishana taarifa za kiitelejensia kwenye maeneo ya mipakani.
Kikoti anasema Kinapa imeamua kudhibiti ujangili wa tembo kwa kuwa wanaweza kutoweka kama udhibiti makini hautakuwapo katika maeneo waliopo.
Kwa mujibu wa Kikoti, katika kipindi  cha 2009 hadi 2012, idadi ya majangili wanaokamatwa imekuwa ikipungua kutoka 320 mwaka 2009 hadi majangili 278 mwaka 2012/2013.
Anasema mikakati ya kukabiliana na ujangili inahusisha pia ujangili wa mazao ya misitu, kuwasha moto kwenye hifadhi na uingizaji mifugo kwenye maeneo ya hifadhi kwa uharibifu huo unaathiri  vyanzo vya maji.
Kikoti anasema kushuka kwa idadi ya mbao na nguzo zinazokamatwa ni dalili tosha kwamba vitendo vya ujangili wa mazao ya misitu ndani ya hifadhi vimekuwa vikidhibitiwa kwa kiasi kikubwa.
Mathalani, mwaka 2009/2010 mbao zilizokamatwa zilikuwa 1,645 na nguzo 229, lakini mwaka 2012/2013 idadi hiyo ilishuka hadi mbao 636 na nguzo 198.
“Mlima Kilimanjaro ni chanzo muhimu cha maji kwa hiyo mifugo ikikanyaga maeneo hayo vyanzo hivyo vinakauka na kuathiri mikoa mbalimbali inayotegemea vyanzo hivi,”anabainisha Kikoti.
Mkuu wa Idara ya Ujirani mwema ya Kinapa, Theodora Aloyce, anasema kipindi cha 2007/2008 hadi 2012/2013, Kinapa imefadhili miradi ya wananchi yenye thamani ya sh1.29 bilioni ikiwamo ujenzi wa madarasa na madawati.
Miradi hiyo imetekelezwa katika wilaya tano zinazozunguka mlima huo ambazo ni Hai, Siha, Rombo, Moshi na Longido.
Theodora anasema miradi mingine iliyofadhiliwa na Kinapa kwa kuchangia asilimia 70 huku wananchi wakichangia asilimia 30 ni ujenzi wa shule za walimu, hosteli za wanafunzi, maabara na miradi ya maji.
Theodora anasema katika miaka ya karibuni, kumekuwapo na vikundi kadhaa vinavyoendesha miradi ya kihifadhi kama kuanzishwa kwa vitalu vya miti ya asili na kufuga Nyuki.
Moja ya shule zinazonufaika ni amabazo ziko jirani na Mlima Kilimanjaro ni Shule ya Sekondari,  Uru Kishumundu, Wilaya ya Moshi vijijini ambayo Kinapa imefadhili ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike.“Tuishukuru sana Kinapa kwa kwa kutujengea jengo la ghorofa tatu,”anasema Philip Nzao ambaye ni Makamu Mkuu wa shule.

Sunday, September 15, 2013

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI







HOTUBA YA MHE. LAZARO NYALANDU, NAIBU WAZIRI WA MALIASI NA UTALII KATIKA MAPOKEZI YA MATEMBEZI YA HIARI YALIYOANDALIWA NA ‘AFRICAN WILDLIFE TRUST’ TAREHE 12/09/2013 ENEO LA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM

• Bw. Patric Patel, Mkurugenzi, African Wildlife Trust
• Washiriki wa Matembezi,
• Wageni waalikwa,
• Mabibi na Mabwana,

Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kwa niaba yangu mwenyewe, ninapenda kuwapa pole ninyi nyote mliotembea kwa hiyari yenu kutoka Arusha hadi hapa Dar es Salaam. Aidha, ninawapongeza African Wildlife Trust kwa kubuni matembezi haya ambayo yamebeba ujumbe mkubwa kuhusu kupiga vita ujangili nchini. Ninawapongeza pia wageni mliofika kwenye halfa hii ya kupokea matembezi haya.

Ndugu Wananchi,
Matembezi haya ya kupiga vita ujangili nchini yamefanyika wakati ambapo kuna ongezeko kubwa la ujangili, nchini hususan ujangili wa tembo. Ujangili huu unasababishwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na:
1. Kuongezeka kwa bei ya meno ya tembo katika masoko haramu huko Mashariki ya Kati na Asia;
2. Kuimarika na kuongezeka kwa magenge ya ujangili (poaching syndicates) pamoja na ubora wa mawasiliano;
3. Kudorora kwa uchumi na kuongezeka kwa umasikini katika jamii, hivyo kufanya watu wengi kujiingiza kwenye ujangili cha uhalifu mwingine;
4. Uroho wa kutaka utajiri wa haraka haraka ambao umewafanya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo na watumishi wa umma kujiingiza katika ujangili; na
5. Rushwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa jumla.

Ujangili umechangia sana katika kupungua idadi ya tembo nchini kutoka 350,000 miaka ya 1960 hadi 110,000 mwaka 2009. Idadi ya tembo wanaouawa na majangili inazidi kuongezeka kila mwaka. Kwa mfano, kwa kipindi cha miaka mitatu (2010 – 2012) tembo waliouawa na majangili ni kama ifuatavyo:
Mwaka 2010 - 259
Mwaka 2011 - 276
Mwaka 2012 - 473
Kati ya Januari na Julai 2013 tembo 378 pia walikuwa wameuawa na majangili.

Ndugu Wananchi,
Serikali, kupitia Wizara ya Maliasi na Utalii, imekuwa ikipambana na majangili hawa ndani na nje ya hifadhi za taifa. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, (2010 – 2012) jumla ya majangili 4,066 walikamatwa na bunduki 1,899 kukamatwa na kutaifishwa. Serikali inaendelea na mikakati na mbinu mbalimbali za kukabiliana na majangili.

Serikali inajenga uwezo wa kukabiliana na majangili porini na matajiri waliopo mijin,i ambao wanafadhili ujangili. Baadhi ya wafanyabiashara wanasiasa na watumishi wa umma wanajihusisha na ujangili. Ninatoa wito na onyo kwao kwamba waache kabisa uovu huu, vinginevyo watajikuta wamenaswa na vyombo vya dola ambapo, mbali na kufikishwa mahakamani, watatangazwa kwenye vyombo vya habari ili umma na wananchi wote Tanzania wajue watu wanaohuJumu rasilimali zao. Dawa ya majangili imekwishachemshwa na inapelekwa mezani wakati wowote. Ole wake atakayenyweshwa na dawa hiyo.

Ndugu Wananchi,
Ninatoa wito kwa wananchi wote waendelee kushirikiana na serikali kupiga vita ujangili kwa kuwafichua majangili popote wanapowaona. Aidha, taasisi zote za umma zishirikiane kupambana na ujangili ili kuutokomeza kabisa.

Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi na mashirika ya kimataifa katika kuukabili ujangili unaovuka mipaka. Wakati huo huo serikali itajengea watumishi wa sekta ya wanyamapori uwezo wa kuutokomeza ujangili.

Ni matumaini yangu kuwa Africa Wildlife Trust haitaishia kwenye matembezi haya bali itaendelea na juhudi nyingine za kupambana na ujangili ikiwa ni pamoja na kutoa fedha na vifaa kwa Sekta ya Wanyamapori ili kuunga mkono kikamilifu juhudi za serikali katika mapambano haya.

Ningependa kuona kwamba kwa kipindi cha muda mfupi ujao, ‘African Wildlife Trust’ inaandaa hafla ya kukabidhi vifaa na/au fedha za kusaidia kupambana na ujangili. Vivyo hivyo, ninatoa wito na changamoto kwa Kampuni za umma na binafsi pamoja na mtu mmoja mmoja kutoa fedha na vifaa kwa ajili ya kuzuia ujangili nchi nzima.

PICHANI:

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) (watano kutoka kushoto msitari wa mbele) akiwa anandamana pamoja na waandamanaji wanaopinga ujangili wa tembo ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’ mara baada ya kuwapokea leo, Ubungo jijini Dar es Salaam asubuhi. Maandamano hayo yamechukua muda wa siku 19 na waandamanaji wametembea kilomita 650, kutoka Jijini Arusha.

Thursday, September 12, 2013

UROHO WA UTAJIRI CHANZO CHA UJANGILI WA TEMBO



na Zawadi Chogogwe

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema kuwa kuongezeka kwa umaskini katika jamii nchini, kunasababishwa na baadhi ya watu wenye uroho wa kutaka utajiri wa haraka.
Nyarandu alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika mapokezi ya matembezi ya hiari yaliyoandaliwa na ‘African Wildlife Trust’.
“Uroho wa kutaka utajiri wa haraka umewafanya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na watumishi wa umma kujiingiza katika ujangili,” alisema.
Aliongeza kuwa ujangili umechangia kupungua kwa idadi ya tembo kutoka 350,000 miaka ya 1960 hadi 110,000 mwaka 2009 ambapo idadi hiyo inaongezeka kila mwaka.
Alitoa mfano kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2010 -2012) jumla ya tembo waliouawa ni 1008 ambapo mwaka 2010 (259), mwaka 2011 (276) na mwaka 2012 (473).
“Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikipambana na majangili hao ndani na nje ya hifadhi za taifa ambapo kwa kipindi hicho wamewakamata majangili 4,066 wakiwa na bunduki 1,899 ambazo zilitaifishwa,” alisema.
Nyalandu alitoa wito kwa wanojihusisha na uovu huo kuacha mara moja vinginevyo watajikuta wamenaswa na vyombo vya dola na kufikishwa mahakamani.
Matembezi hayo yalikuwa ni ya kupiga vita ujangili unaofanywa nchini, ambayo yamefanyika siku 19 kutoka jijini Arusha hadi Dar es Salaam kwa kuwashirikisha watu 1,000.
Naye Mkurugenzi wa African Wildlife Trust, Patric Patel, alisema kuwa Desemba watu 150 watatoka Arusha kuja Dar es Saalam kwa kutumia baiskeli lengo lao likiwa ni kutunza hifadhi za taifa na kupambana na ujangili.




UTALII SADANI


Ngiri kuishi na watu Sadani ni kawaidal


Baadhi ya ngiri wakiwa Mbuga ya Sadani. Picha ya Maktaba. 
Na Charles Kayoka, Mwananchi





Kwa ufupi
  • Mafanikio katika utunzaji wa hifadhi hii umesababisha wanyama kama ngiri (warthogs) kuwa wengi na kuingia katika makazi ya wananchi na kula kila wanachoweza kula bila kuogopa. 
  •  
  • Ni  jambo la kawaida. Kuna habari za hao ngiri kuishi na binadamu katika nyumba moja, ngiri wakitumia makazi ya binadamu kuzaana.
Baada ya makala yangu ya wiki iliyopita baadhi ya wasomaji walitaka kujua kama wangetembelea Sadani wangeona nini.

 Katika Kijiji cha Sadani wananchi hawajaamka usingizini na kuitumia mbuga ya wanyama kama fursa ya kiuchumi.
Awali nilidokeza kwamba kijiji hicho kina historia ndefu, kama wananchi wangeamka basi utalii wa utamaduni na kihistoria ungekuwa kivutio kikubwa sana kwa wageni ambao wangetaka kujifunza historia hiyo.

Wageni wengi katika miaka iliyopita walifika Sadani wakiwamo wachungaji wa Kijerumani Rebman na Krapf, na mpelelezi na mwanajeshi mashuhuru, Sir Francis Burton, na safari za mwanzo za waendeza dini ya Ukristo Tanzania Bara zilianzia Sadani, Pangani na hadi Ubondei (Halle) na Kilimanjaro. Ushahidi huu utaupata kwenye vitabu vyao wenyewe.

 Lakini ukifika Sadani utaona makaburi ya wageni waliofika kutoka katikati hadi mwishoni mwa miaka ya 1800. Utaona ngome kubwa iliyotumika kama soko la watumwa.

Lakini Kijiji cha Sadani kimezungukwa na mbuga ya wanyama ya Sadani yenye kila aina ya wanyama. Mafanikio katika utunzaji wa hifadhi hii umesababisha wanyama kama ngiri (warthogs) kuwa wengi na kuingia katika makazi ya wananchi na kula kila wanachoweza kula bila kuogopa.

 Ni  jambo la kawaida. Kuna habari za hao ngiri kuishi na binadamu katika nyumba moja, ngiri wakitumia makazi ya binadamu kuzaana.
Lakini cha ajabu mbuga ya wanyama ya Sadani ni ya pekee. Hii ni mbuga ya kwanza katika Tanzania ambayo imetoka bara hadi baharini.

Kasa hao huzaliwa hapo na kusambaa maeneo ya mbali, hasa Australia. Lakini wakati wa kuzaana huja tena hapohapo bila kupotea. Hiki ni kivutio cha aina yake. 

Sadani ilianzishwa miaka ya 1950 kama ranchi ya serikali ya mkoloni wakati huo kwa ajili ya ng’ombe. Na ukifika kijijini Mkwaja Ranchi utaona ushahidi huo wa kihistoria. 

Kuna mengi ya kuona ingawa maelezo katika maandishi hakuna.
Ckayoka28@yahoo.com, 0766959349



Tuesday, September 10, 2013

JENERALI ULIMWENGU KUONGOZA BODI


JENERALI ULIMWENGU MWENYEKITI WA BODI 
 
The General Public is hereby informed that pursuant to the powers conferred upon him by section 18(2) (b) of the Tourism Act No. 29 of 2008, the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Sued Kagasheki has appointed the following as members of the Tanzania Tourism Licensing Board (TTLB), for a period of three years effective from 1st July, 2013.
1. Jenerali Ulimwengu - Chairman
2. Abdullal Khamis Abdullah (Assistant Commissioner - Boarder Management-Immigration Services Department)
1. Willy N. Mlulu (Assistant Commissioner of Police)
2. Ms. Leonela Kishebuka (Registrar of Companies, BRELA)
3. Dr. Ezekiel A. Dembe (TANAPA)
4. Patrick N. Kassera (Commissioner for Domestic Revenue – TRA),
5. Ms. Monica L. Mwamunyange (Commissioner for Budget, Ministry of Finance),
6. Ms. Mary Kalikawe, (Chairperson of AWOTTA)
7. Zuher Hassanali Fazal, (TATO)
8. Richard Rugimbana, (Executive Secretary, Tanzania Confederation of Tourism -TCT)
9. Michel Mantheakis, (CEO, Mantheakis Safaris Ltd)
10. Ms. Scholastica Ponera, (CEO, Pongo Safaris Ltd.)

Ibrahim A. Mussa
ACTING PERMANENT SECRETARY

Saturday, September 7, 2013

BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA KUFANYIKA SEPTEMBA 8,2013


 KATIBU WA TASWA  MKOA WA ARUSHA MUSSA JUMA KAIKATI AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI UKUMBI WA PALACE HOTEL JIJINI ARUSHA KUHUSU BONANZA LA WAANDISHI WA MIKOA YA DAR,ARUSHA NA MANYARA LITALOFANYIKA SEPT,8,2013 VIWANJA VYA GENERAL TYRE

 MAANDALIZI YA BONANZA
WAANDISHI WAKIFUATILIA MAELEZO KUTOKA KWA KATIBU WA TASWA ARUSHA KUHUSIANA NA BONANZA

Friday, September 6, 2013

FURSA ZA UTALII

 FURSA ZA UTALII JIJINI ARUSHA
 VINYAGO
 WAGENI WENGI HUNUNUA VINYAGO HAPA
 WAGENI HUNUNUA VINYAGO HAPA CULTURAL HERITAGE



Thursday, September 5, 2013

WANYAMA KIVUTIO CHA WATALII

 BWAWALA VIBOKO HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
 TWIGA AKISAKA CHAKULA HIFADHI YA MAMLAKA YA NGORONGORO
 VIBOKO
TWIGA

TAARIFA KWA UMMA


HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
USAHIHI WA TAARIFA ZA MGENI ALIYEUWAWA NA TEMBO NJE
YA HIFADHI YA TARANGIRE
Baadhi ya vyombo vya habari nchini jana na leo vimekuwa vikiripoti juu
ya tukio la kuuwawa na tembo kwa mgeni kutoka Marekani
anayefahamika kama Thomas Vardon Macfee (58) tarehe 31.08.2013 katika
Hifadhi ya Taifa Tarangire.
Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kuweka usahihi wa taarifa
zilizoripotiwa kama ifutavyo:-
Tukio la mgeni husika lilitokea nje ya Hifadhi ya Tarangire katika kijiji cha
Kakoi kambi ya Tarangire River Camp, wakiwa wanafanya utalii wa
kutembea kwa miguu “Walking Safari”. Baada ya kuvamiwa na
kuumizwa, mgeni huyu alifikishwa katika zahanati ya Hifadhi ya
Tarangire na watumishi wa kambi aliyofikia iliyo nje ya hifadhi kwa ajili
ya matibabu ya huduma ya kwanza na alipofikishwa, alifariki dunia.
Hivyo basi, Shirika linapenda kusahihisha kuwa tukio lililopelekea kifo
cha mgeni lilitokea nje ya Hifadhi ya Tarangire na si ndani kama
ilivyoripotiwa.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO
HIFADHI ZA TAIFA
S.L.P 3134
ARUSHA
05/09/

Sunday, September 1, 2013

TANAPA YAZIDI KUONGEZA KIKOSI CHA KUKABILIANA NA UJANGILI

 MKURUGENZI MKUU WA TANAPA ALLAN KIJAZI MWENYE NGUO NYEUPE AKIWA NA MAKAMANDA WALIOFUZU MAFUNZO HUKO KATAVI IKIWA NI MKAKATI WA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA UJANGILI NCHINI.
 MIONGONI MWA VIVUTIO VIKUBWA NDANI YA HIFADHI ZA TAIFA NI TEMBO
 MMOJA WA WATALII AKINGIA HOTELI YA KITALII SERONERA ,ILIYOKO NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

 WAGENI WAKIWA LANGO LA NGORONGORO TAYARI KWA KUINGIA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.