Mamlaka kamili Idara ya Wanyamapori yaanzishwa
na Asha
Bani-TANZANIA DAIMA
WADAU
na wanataaluma mbalimbali nchini wamekutana jijini Dar es Salaam na kujadili
kuanzishwa mamlaka kamili ya kusimamia Idara ya Wanyamapori.
Akifungua
mkutano huo jijini hapa mwishoni mwa wiki kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori,
Profesa Alexander Songolwa, alisema mamlaka hiyo inaanzishwa kuchukua baadhi
ya majukumu ya Idara ya Wanyamapori, hasa usimamizi wa rasilimali ya
wanyamapori.
Alisema
uanzishwaji wa mamlaka hiyo utasaidia kuokoa wanyamapori walioko hatarini
kutoweka kutokana na changamoto nyingi zinazotishia makazi na mazingira yao.
Prof.
Songolwa alisema mfumo uliopo hivi sasa hauiwezeshi serikali kukabiliana na
changamoto hizo, hivyo imeamua kubadilisha mfumo wa usimamizi na uendelezaji
wa sekta ndogo ya wanyamapori kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi pamoja na
matokeo yake.
Prof.
Songolwa alisema Idara ya Wanyamapori ya sasa inafanya kazi za urekebu,
uratibu na usimamizi wa rasilimali za wanyamapori. Hivyo uanzishwaji wa
mamlaka mpya unalenga kutenganisha majukumu hayo.
Alisema
katika utenganisho huo, Idara na Wizara kwa ujumla itabaki na majukumu mawili
ambayo ni urekebu na uratibu huku mamlaka ikichukua jukumu la usimamizi wa
rasilimali za wanyamapori.
|
No comments:
Post a Comment