Thursday, August 6, 2015

BREAKIN NEWZZ!!:- KUKAMATWA KWA MENO YA TEMBO USWISS WAZIRI NYALANDU AFUNGUKA LIKE NEVER BEFORE SOMA HAPA LIVE!!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirYSCVlbkt-CenVRznMnNyyX0KxjRAHUHfLR-v3dbiawwXZz_OCl0H_N0hV0ZPEs0Ybp3UvD37Xezrchc3ZjGs5feo7ADPOot4B5UrqqpNqvtA3wuxhK3JqlAtNjE3hMwVVlfLmzvIvHPJ/s1600/2B16A65B00000578-3185470-image-a-7_1438728714802.jpg

Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea taarifa kupitia Vyombo vya Habari inayohusu kukamatwa kwa nyara zinazojumuisha meno ya tembo yenye uzito wa kilo 262, kucha na meno ya simba vyenye uzito wa kilo moja(1). Tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea kwenye uwanja wa ndege wa Zurich nchini Uswisi tarehe 06 Julai, 2015. Kwa mujibu wa taarifa hizo, nyara hizo zilipatikana ndani ya masanduku manane (8) zikiwa njiani kwenda Beijing-China kutokea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kupitia Zurich.
Wizara inachukua nafasi hii kupongeza Uongozi wa uwanja wa ndege wa Zurich, na Serikali ya Uswisi na wote walioshiriki kubaini na kukamata nyara hizo. Wizara imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizi na kwamba nyara hizo zimesafirishwa kupitia uwanja wa ndege wa JN Dar es Salaam. Tukio hili linadhihirisha kuwa tatizo la ujangili bado linaendelea ndani na nje ya nchi yetu licha ya jitihada nyingi zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya za Kimataifa.
Wizara inapenda kuuhakikishia umma kuwa sisi kama nchi tunafanya na kutumia jitihada zote kupambana na vitendo vya ujangili unaotishia kutoweka kwa rasilimali za wanyamapori wetu.
Baada ya kupokea taarifa hizo, Wizara imeanza kufanya uchunguzi kwa kushirikisha mamlaka husika ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja kuwabaini wote waliohusika na kadhia hii. Wizara inapenda kutoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kufanya uchunguzi huu aziwasilishe kwenye mamlaka za Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na

Lazaro S. Nyalandu
Waziri wa Maliasili na Utalii.

No comments:

Post a Comment