Wageni wakipata chakula ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Na Hakimu Mwafongo, Mwananchi
Posted Jumanne,Juni10 2014 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Licha ya kuwa na mikakati mingi,
idadi ya watalii wamekuwa ni wachache
Iringa. Licha ya Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na wadau
wengine kutumia fedha nyingi kuimarisha miundombinu na kuboresha huduma kwenye
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Runapa), bado inapokea wageni wachache.
Akigungumza na waandishi wa habari
katika ofisi za hifadhi hiyo, ofisa mwandamizi wa utalii wa hifadhi hiyo, Eva
Pwele alisema licha ya mikakati mbalimbali inayofanywa, watalii wanaoongezeka ni
wastani wa asilimia 0.2 tu kwa mwaka, kiasi ambacho ni kidogo mno.
Alisema idadi ya watalii wa nje
imeongezeka kutoka 19,081 mwaka 2008/9 hadi 24,293 huku wa ndani wakiwa
wameongezeka kutoka 8,151 hadi kufikia 9,994 mwaka 2013.
Alisema idadi ya wageni wa ndani
imekuwa ikiongezeka kidogo wakati kwa wageni kutoka nje inaongezeka kwa kiwango
cha juu kidogo.
Hifadhi hiyo inafikika wakati wote,
barabara za ndani ya hifadhi zimetengenezwa na kuwawezesha watalii kutembea
hata wakati wa masika na kiangazi.
Kuna huduma ya malazi na mawasiliano
yameimairishwa ili kuhakikisha wageni wanapata fursa nzuri ya kutembelea
hifadhi hiyo. Hata hivyo tatizo ni namna watalii wanavyopatikana kwa kiasi
kidogo.
Mpango wa hifadhi hiyo ni kufungua
njia nyingine za barabara ili kuunganisha na Mkoa wa Mbeya kupitia wilaya ya
Chunya ili wageni wanaotumia uwanja wa kimataifa wa Songwe wasitembee umbali
mrefu kupitia Iringa; badala yake wawe wanapitia Wilaya ya Chunya na kuingia
Ruaha.
No comments:
Post a Comment