Juni 4, 2014
Na James Magai, Mwananchi
Posted Jumatano,Juni4 2014 saa 24:0 AM
Posted Jumatano,Juni4 2014 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Wakili Hilla alidai vipande hivyo
vilivyokuwa na uzito wa kilo 1,889, mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Dar es Salaam. Wafanyabiashara wawili wakazi wa Dar es Salaam
wamepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Frank Moshi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jana na kusomewa mashtaka matatu ya kufanya biashara ya pembe za ndovu
zenye thamani ya zaidi ya Sh5.4 bilioni.
Washtakiwa hao, Salvius Matembo (39)
na Manase Philemon (39) walisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Pius
Hilla aliyedai kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 2014, washtakiwa hao
walisafirisha na kuuza vipande 706 vya pembe hizo.
Wakili Hilla alidai vipande hivyo
vilivyokuwa na uzito wa kilo 1,889, mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori. Shtaka la tatu ni la
kutoroka, linamhusu mshtakiwa wa pili aliyedaiwa kutoroka chini ya ulinzi wa
polisi.
Wakili huyo alisema upelelezi wa
kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Moshi aliahirisha kesi hiyo
hadi Juni 17, mwaka huu itakapotajwa na kuamuru washtakiwa warejeshwe mahabusu
hadi tarehe hiyo.
No comments:
Post a Comment