Saturday, February 1, 2014

Wakamatwa na meno ya tembo


Jumamosi, Februari 01, 2014 09:20 Na Walter Mguluchuma, Katavi
WATU wawili  wakazi  wa  Mtaa wa Kawajense, Wilaya  ya  Mpanda, Mkoa  wa Katavi, wamekamatwa  kwa  tuhuma  za  kukutwa na  vipande   vitatu  vya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 24. Kamanda  wa Polisi Mkoa  wa Katavi, Dhahiri  Kidavashari, aliwataja  watuhumiwa hao kuwa ni Mateso Kayanda (35) na Damiani Kayanda (28).

Kamanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa jioni ya Januari  29, mwaka huu, nyumbani kwa watuhumiwa hao.

Kidavashari  alieleza kuwa watuhumiwa walikamatwa baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba watu hao wanajihusisha na biashara haramu na ndipo jeshi likaweka mtego kuwanasa.

Alieleza siku ya tukio watuhumiwa walikamatwa wakiwa na vipande vitatu vya meno ya tembo vya thamani iliyotajwa.

Alisema watuhumiwa hao pia walikutwa na mbao 53 aina ya kipilipili za thamani  ya Sh. 250.000, ambazo walikuwa wakizimiliki  isivyo halali.

Kamanda Kidavashari alieleza watumiwa wanatarajiwa kufikishwa  mahakamani  mara baada ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika.

Bottom of Form



No comments:

Post a Comment