Thursday, September 12, 2013

UTALII SADANI


Ngiri kuishi na watu Sadani ni kawaidal


Baadhi ya ngiri wakiwa Mbuga ya Sadani. Picha ya Maktaba. 
Na Charles Kayoka, Mwananchi





Kwa ufupi
  • Mafanikio katika utunzaji wa hifadhi hii umesababisha wanyama kama ngiri (warthogs) kuwa wengi na kuingia katika makazi ya wananchi na kula kila wanachoweza kula bila kuogopa. 
  •  
  • Ni  jambo la kawaida. Kuna habari za hao ngiri kuishi na binadamu katika nyumba moja, ngiri wakitumia makazi ya binadamu kuzaana.
Baada ya makala yangu ya wiki iliyopita baadhi ya wasomaji walitaka kujua kama wangetembelea Sadani wangeona nini.

 Katika Kijiji cha Sadani wananchi hawajaamka usingizini na kuitumia mbuga ya wanyama kama fursa ya kiuchumi.
Awali nilidokeza kwamba kijiji hicho kina historia ndefu, kama wananchi wangeamka basi utalii wa utamaduni na kihistoria ungekuwa kivutio kikubwa sana kwa wageni ambao wangetaka kujifunza historia hiyo.

Wageni wengi katika miaka iliyopita walifika Sadani wakiwamo wachungaji wa Kijerumani Rebman na Krapf, na mpelelezi na mwanajeshi mashuhuru, Sir Francis Burton, na safari za mwanzo za waendeza dini ya Ukristo Tanzania Bara zilianzia Sadani, Pangani na hadi Ubondei (Halle) na Kilimanjaro. Ushahidi huu utaupata kwenye vitabu vyao wenyewe.

 Lakini ukifika Sadani utaona makaburi ya wageni waliofika kutoka katikati hadi mwishoni mwa miaka ya 1800. Utaona ngome kubwa iliyotumika kama soko la watumwa.

Lakini Kijiji cha Sadani kimezungukwa na mbuga ya wanyama ya Sadani yenye kila aina ya wanyama. Mafanikio katika utunzaji wa hifadhi hii umesababisha wanyama kama ngiri (warthogs) kuwa wengi na kuingia katika makazi ya wananchi na kula kila wanachoweza kula bila kuogopa.

 Ni  jambo la kawaida. Kuna habari za hao ngiri kuishi na binadamu katika nyumba moja, ngiri wakitumia makazi ya binadamu kuzaana.
Lakini cha ajabu mbuga ya wanyama ya Sadani ni ya pekee. Hii ni mbuga ya kwanza katika Tanzania ambayo imetoka bara hadi baharini.

Kasa hao huzaliwa hapo na kusambaa maeneo ya mbali, hasa Australia. Lakini wakati wa kuzaana huja tena hapohapo bila kupotea. Hiki ni kivutio cha aina yake. 

Sadani ilianzishwa miaka ya 1950 kama ranchi ya serikali ya mkoloni wakati huo kwa ajili ya ng’ombe. Na ukifika kijijini Mkwaja Ranchi utaona ushahidi huo wa kihistoria. 

Kuna mengi ya kuona ingawa maelezo katika maandishi hakuna.
Ckayoka28@yahoo.com, 0766959349



No comments:

Post a Comment