Tuesday, September 24, 2013

MAMLAKA YA WANYAMAPORI


       Mamlaka kamili Idara ya Wanyamapori yaanzishwa
  na Asha Bani-TANZANIA DAIMA
     
WADAU na wanataaluma mbalimbali nchini wamekutana jijini Dar es Salaam na kujadili kuanzishwa mamlaka kamili ya kusimamia Idara ya Wanyamapori.
Akifungua mkutano huo jijini hapa mwishoni mwa wiki kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songolwa, alisema mamlaka hiyo inaanzishwa kuchukua baadhi ya majukumu ya Idara ya Wanyamapori, hasa usimamizi wa rasilimali ya wanyamapori.
Alisema uanzishwaji wa mamlaka hiyo utasaidia kuokoa wanyamapori walioko hatarini kutoweka kutokana na changamoto nyingi zinazotishia makazi na mazingira yao.
Prof. Songolwa alisema mfumo uliopo hivi sasa hauiwezeshi serikali kukabiliana na changamoto hizo, hivyo imeamua kubadilisha mfumo wa usimamizi na uendelezaji wa sekta ndogo ya wanyamapori kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi pamoja na matokeo yake.
Prof. Songolwa alisema Idara ya Wanyamapori ya sasa inafanya kazi za urekebu, uratibu na usimamizi wa rasilimali za wanyamapori. Hivyo uanzishwaji wa mamlaka mpya unalenga kutenganisha majukumu hayo.
Alisema katika utenganisho huo, Idara na Wizara kwa ujumla itabaki na majukumu mawili ambayo ni urekebu na uratibu huku mamlaka ikichukua jukumu la usimamizi wa rasilimali za wanyamapori.



No comments:

Post a Comment