Monday, December 30, 2013

TEMBO WAZIDI KUTEKETEA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII 
TAARIFA KWA UMMA
Itakumbukwa kuwa Serikali iliamua kuanzisha “Operesheni Tokomeza Ujangili” kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ujangili katika maeneo yote yaliyotengwa kisheria kama Mapori ya Akiba; Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Misitu katika miaka ya karibuni. Hata hivyo, Serikali iliamua kusitisha operesheni hiyo kwa muda.

Kufuatia kusitishwa kwa Operesheni Tokomeza, matukio ya uvunjaji wa sheria za hifadhi kama vile uingizaji holela wa mifugo katika maeneo ya hifadhi; ujangili wa tembo pamoja na uvunaji wa miti katika hifadhi za misitu yanaonekana kushamiri. Aidha, kumekuwa na ongezeko la kuvamiwa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na hata kuwasababisha madhara yakiwemo vifo na majeraha. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na:
·        Majangili kuua takriban tembo 60 katika Hifadhi/Mapori ya Selous, Rungwa, Burigi na Katavi na Ngorongoro. Hawa ni takriban tembo wawili kwa siku. Ikumbukwe kuwa wakati wa kipindi chote cha operesheni kilichodumu kwa mwezi mmoja ni tembo wawili tu waliokuwa wameuawa.  
·        Watumishi wa Pori la Akiba Mkungunero (Kondoa) waliokuwa doria kuvamiwa na kundi la watu wapatao 80 waliokuwa na mikuki na silaha nyingine za jadi  tarehe  24 Desemba, 2013.
·        Kuuawa kwa Askari mmoja wa wanyamapori aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Magengere (40) na mwingine, Bwana Yahaya Ramadhani (34), kujeruhiwa vibaya na Wafugaji walioingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Jumuiya (WMA) Ukutu (au JUKUMU) iliyoko Morogoro vijijini tarehe 6 Decemba, 2013.
·        Mtumishi mmoja wa wanyamapori, Sajidi Majidi, kujeruhiwa kwa kuchomwa mkuki kichwani na kuvunjwa mkono na wafugaji walioingiza ng’ombe katika Eneo la Ramsar la Kilombero tarehe 14 Novemba, 2013.
·        Kukamatwa kwa gari lililokuwa na mizoga 20 ya swala wilayani Simanjiro siku za karibuni
·        Kuanzishwa kwa kambi ya majangili katika Pori la Akiba Burigi ambapo vitendo vya ujangili vinaendeshwa. Majangili waliokuwa na silaha za moto walikimbia na kuacha nyuma nyani 30 waliokuwa wamewaua baada ya kukurupushwa na askari wa wanyamapori.
·        Kuongezeka wimbi la uvamizi na ufugaji wa mifugo ndani ya mapori ya akiba na hifadhi za misitu iliyopo magharibi mwa nchi yetu, hasa Burigi-Biharamulo-Kimisi, malagarasi-Moyowosi, Rukwa Lukwati, Luwanda, Ugalla, Ibanda-Rumanyika, Minziro na Katavi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 pamoja na Sheria zinazosimamia maeneo ya Hifadhi za Taifa na Misitu kuwa hairuhusiwi wananchi kuingia katika maeneo haya bila kibali ikiwa ni pamoja na uingizaji wa mifugo kwa ajili malisho. Aidha, bado vitendo vya ujangili haviruhusiwi chini ya sheria hizi. Kifungu cha 15 ni marufuku mtu yeyote kuingia kwenye pori la akiba bila kibali.  Aidha, Sheria hiyo inakataza kuwa na silaha yoyote ndani ya Pori la Akiba bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori [kifungu cha 17]; kuwinda, kuua, kukamata au kujeruhi mnyama [Kifungu cha 19] na kuchunga ng’ombe ndani ya Pori la Akiba [Kifungu cha 21].
Ikumbukwe kuwa matukio yaliyotokea bungeni Dodoma, hayajatengua Sheria yoyote ya Wanyamapori au Misitu.  Hamna maamuzi yoyote ya Bunge yaliyohalalisha ukiukwaji wa Sheria za Uhifadhi. Hivyo, wananchi wanatakiwa kutii na kufuata Sheria hizo kama zilivyo. Tahadhari inatolewa kuwa Serikali haitasita kumchukulia hatua kali yeyote atakayekiuka Sheria ya Wanyamapori kwa makusudi. Tunawaomba wananchi wasikubali kudanganywa na mtu yeyote yule kuvunja Sheria za nchi.

Aidha, nachukua nafasi hii kuwaagiza watumishi wote wa Wizara ya Maliasili na Utalii wahakikishe kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya ulinzi wa maeneo ya Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba na Misitu ya Hifadhi bila kutetereka. Sanjari na hilo wasisite kuchukua hatua stahiki dhidi ya mhalifu yeyote mradi tu wanazingatia Sheria, Kanuni na taratibu.  Utekelezaji huu wa sheria ufanyike bila kuathiri haki za msingi za binadamu.

Serikali ina maadili na miiko inayotawala utendaji kazi wa watumishi wake wote wakiwemo wale wa maliasili. Wizara ya Maliasili itaendelea kuwakumbusha watumishi wake juu ya maadili na miiko hii kupitia mafunzo ya mara kwa mara na mbinu nyingine. Aidha, Wizara itaendelea kuboresha miongozo inayohusu maadili na miiko hii ili iweze kuendana na wakati.

Mwisho, Serikali inasisitiza kuwa, kwa kutumia vyombo vyake, itaendelea kutekeleza majukumu yake na kusimamia ipasavyo Sheria ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayeshiriki moja kwa moja au kusaidia vitendo vya ujangili ili kunusuru rasilimali za Taifa. Jukumu la uhifadhi wa maliasili zetu liko pale pale, ni letu na lazima litekelezwe kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.

Imetolewa na:

Mh. Lazaro Nyalandu, MB.
NAIBU WAZIRI, MALIASILI NA UTALII
Desemba 29, 2013.

Mapigano wakulima, wafugaji yaua wanane

Na Augusta Njoji

30th December 2013

Hali si shwari katika Wilaya Kiteto mkoani Manyara kufuatia kuzuka kwa mapigano baina ya wakulima na wafugaji na kusababisha vifo na majeruhi.

Kufuatia hali hiyo, Chama cha Wakulima na Wafugaji wilayani Kiteto (Chawaki), jana kiliitisha mkutano kujadili mapigano hayo na kusaka suluhu.

Baada ya mkutano huo kuanza, zilizuka vurugu huku wafugaji jamii ya Kimasai wakiwapinga viongozi wa chama hicho na kumlazimu Mkuu wa Kituo cha Polisi wa wilaya hiyo, Foka Dinya, kuuvunja mkutano huo kwa madai kuwa kuna hali ya uvunjifu wa amani.

NIPASHE ilishuhudia vurugu hizo ambazo chanzo chake ni kugombea eneo la hifadhi ya Mbuga ya Embloi Murtangosi na polisi kufyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi hao pia walilalamikia kunyanyasika huku wakimtuhumu Mbunge wao, Benedict Ole Nangoro, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa madai kuwa amekuwa akichochea vurugu hizo kwa kuwabagua wakulima.

Walidai kuwa tangu Desemba 16, mwaka huu, vurugu hizo zimesababisha watu watano kupoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa.

Mmoja wakulima hao, Ramadhani Machaku, alidai kuwa wanasikitishwa kuwapo kwa vitendo hivyo na maisha yao yapo hatarini, lakini hakuna hata kiongozi mmoja ambaye amejitokeza kutafuta suluhu.

Alidai kuwa watu wanachinjwa kama kuku na kupoteza maisha yao na wafugaji kwa kuwavamia usiku wakiwa wamelala huku serikali mkoani humo ikiwataka wakulima kuondoka katika eneo la hifadhi, hatua ambayo alidai haiwatendei haki.

“Mpaka sasa hatuelewi hatma yetu licha ya uongozi wetu kuwapo hapa, hatuelewi wanafanya nini, lakini jambo moja nasema hivi hatutaondoka katika maeneo haya hadi kieleweke kwani kilimo ndicho kinachotusaidia kuishi,” alisema Machaku.

Naye dada wa mmoja wa marehemu ambaye aliuawa na katika mgogoro huo, Sada Ally, alisema kuwa mdogo wake alichomwa mkuki tumboni wakampeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, lakini alifariki dunia wakati akipata matibabu.

“Mgogoro huu ni wa wakulima na wafugaji, wafugaji wamekuwa hawataki wakulima walime, bali wao wachunge mifugo, hali hii imesababisha mdogo wangu apoteze maisha mpaka sasa,” alisema.

Aliongeza: “Serikali naomba itusaidie jamani wakulima wanateseka Kiteto, wakulima hawana mtu wa kuwaangalia, viongozi wao wote wa Kiteto ni Wamasai, hivyo wanakuwa upande wa wafugaji moja kwa moja na hawawasikilizi wakulima,” alidai Sada.

Msemaji wa Chawaki, Hassan Losioki, alisema kuwa tamko la chama hicho ni kuitaka Serikali irejeshe ardhi vijijini kwa mujibu wa Sheria namba nne na tano ya Mwaka 1999 ili wananchi wafanye maamuzi ya matumizi ya ardhi wao wenyewe.

Pia Losioki alimuomba Rais Jakaya Kikwete, aingilie kati mgogoro huo ambao ni wa muda mrefu takribani miaka minane sasa.

“Mgogoro huu umekuwa ni wa muda mrefu kwani umedumu kwa miaka minane sasa ambapo kila mwaka kumekuwapo na mauaji ya watu hasa unapofika msimu wa kilimo, “ alisema Hassan.
Hata hivyo, alisema kuwa vijiji vitano kati ya saba vilivyopo katika hifadhi hiyo vya Nati, Emaliti, Engusilisidani, Lotepesi na Kimana, vimejitoa katika hifadhi hiyo kupitia mikutano halali ya serikali za vijiji husika.
Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo, OCD Foka Dinya, alithibitisha kuwa hali si shwari Kiteto na kwamba wanawatafuta wanaohusika na mauaji.

“Mimi siwezi kuzungumzia mauaji yalitotokea kuanzia tarehe 16 mwezi huu nilikuwa likizo, ninachojua ni mfugaji mmoja aliyeuawa ambaye alizikwa jana nikiwa tayari nimerudi kazini,” alisema na kuongeza:

“Hata hivyo, sitazungumza sana kwani mimi si msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani kwetu…Leo (jana), kuna watu wawili ambao wamejeruhiwa katika vurugu hizi na wamepelekwa hospitali na polisi bado wanaendelea na doria kutokana na hali kutokuwa shwari.”

Akijibu tuhuma hizo, Ole Nangoro alisema kuwa hahusiki na uchochezi wa vurugu hizo na kufafanua kuwa hifadhi ya Embloi Murtangosi imesajiliwa kama hifadhi ya kijamii.

“Na ipo katika vijiji saba vya Wilaya ya Kiteto, wananchi wa eneo hilo walisema wataitumia ardhi hiyo watu 133,000 kwa ajili ya hifadhi ya jamii na baadaye eneo hilo lilivamiwa na watu wengi toka nje ya wilaya hiyo,” alisema.

“Kwa mwaka 2003, 2004 na 2006 waliondolewa, mwaka 2007 watu 50 walikwenda Kiteto Mahakama ya Ardhi kufungua kesi dhidi ya Halmashauri wakashinda na baadaye halmashauri ilikata rufaa na ikashinda, hivyo mahakama ikamteua `court broker' aliyesimamia uendeshaji wa kuwaondoa watu waliovamia katika eneo hilo,” alisema Naibu Waziri huyo.

Alibainisha kuwa mgogoro huo unachochewa na wale wanaopingana na sheria.
Kuhusu madai ya kuwapo kundi la Wamasai katika boma lake lililopo eneo la Olpopong’i ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji na wamekodiwa kutoka Kenya, Ole Nangoro alisema vyombo vya dola viende kuwatafuta nyumbani kwake na wawakamate lakini akasisitiza kuwa hakuna kitu kama hicho. 




KENYA NA TANZANIA KUSHIRIKIANA KUDHIBITI UJANGILI


Na Charles Ngereza
30th December 2013

Hifadhi Jamii ya Wanyama (WMA) la Enduimet, Wilayani Longido
 Wadau wa uhifadhi wanyama pori kati ya Tanzania na Kenya wameanzisha ushirikiano wa kudhibiti ujangili wa wanyama pori katika mpaka wa kaskazini mwa Tanzania.

Ushirikiano huo unahusisha kubadilishana taarifa za kihalifu, intelijensia na kufanya doria za pamoja katika mapito ya wanyama pori eneo hilo ambalo linaunganisha hifadhi za Arusha, Kilimanjaro na hifadhi ya Amboseli ya Kenya
Wakizungumza katika mkutano wa pamoja uliofanyika katika eneo la Hifadhi Jamii ya Wanyama (WMA) la Enduimet Wilayani Longido, walisema uwindaji wa tembo na simba katika eneo la mpaka limekuwa ni tatizo kubwa.

Mkuu wa usalama katika eneo la hifadhi jamii la Enduimet, Imanuel Bujiku, alisema wawindaji wamekuwa wakiwinda wanyama na kukimbilia nchi jirani kukimbia kukamatwa.
Bujiku alisema ushirikiano huo umehusisha idara zote za ulinzi usalama katika nchi zote zikiwemo polisi na vikosi vya kudhibiti ujangili.

“Lengo kuu la ushirikiano wetu ni wa kuhakikisha eneo la mapito ya wanyama kutoka Hifadhi ya Amboseli Kenya kuja Tanzania tunaweka ulinzi wa kutosha kuzuia mauaji ya wanyama,” alisema Bujiku.

Kuhusu hali ya ujangili katika eneo la Enduimet, alisema kuanzia Januari hadi Oktoba, ya majangili 16 walikamatwa pamoja na gari moja, baiskeli nane pikipiki tano na watuhumiwa kufikishwa mahakakani.

Mhifadhi jamii kutoka Hifadhi ya Amboseli Kenya, Francis Irungu, alisema ushirikiano huo utadhibiti ujangili na kuleta tija kubwa katka uhifadhi wanyama pori.

Samwel Ole Kaangi kutoka mfuko wa uhifadhi wa Big Life nchini Kenya, alisema ushirikiano huo umewafanya kuweka mpango kazi na utekelezaji kutokomeza ujangili katika eneo hilo.
CHANZO: NIPASHE

Sunday, December 29, 2013

Ushiriki wa umma unavyochochea utalii wa ndani


Na Mashaka Mgeta
29th December 2013

   Pia ni nyenzo ya kuhamasisha uhifadhi nchini
Ni safari ya takribani mwezi mmoja, ikinifikisha kwenye hifadhi za Tarangire, Kilimanjaro (Kinapa) na Serengeti (Senapa) ambazo zote zipo chini ya Hifadhi za Taifa (Tanapa).

Lakini katika kupata taarifa kwa upana zaidi kuhusu uhifadhi na utalii wa ndani,  ninapanua wigo wa vyanzo na kufika kwenye pori la akiba la Selou ambapo ninakutana na jamii zinazoishi kuzizunguka rasilimali hizo.

Yapo mafanikio kadhaa ya kijamii yanayotokana na uwekezaji wa mamlaka zinazoongoza maliasili hizo, kwa kugharamia huduma kadhaa za jamii ikiwa ni sehemu ya kuzifanya (jamii hizo) zinufaike na uwapo wa rasilimali hizo kwenye maeneo yao.

Kwa maana nyingine, kunufaika kunakotokana na uwapo wa maliasili hizo kunazifanya jamii zinazoishi maeneo yanayozizunguka, kuhisi umiliki wake na hivyo kuzilinda na kuziendeleza.

Miongoni mwa maeneo yanayozizunguka maliasili hizo kumefanyika ujenzi ama ukarabati wa nyumba ama ofisi zilizo katika sekta za afya, elimu na nyinginezo.

Mary Safari ni Mjumbe wa Kamati ya Mazingira na Uhifadhi ya kijiji cha Mamire wilayani Babati mkoa wa Manyara, kikiwa ni miongoni mwa maeneo jirani ya hifadhi ya Tarangire.

Anasema katika kipindi cha maisha ya zaidi ya miaka 34 akiwa kijijini hapo, hakuwahi kuwaona ‘uso kwa uso’ baadhi ya wanyamapori, zaidi ya kuwashuhudia kwenye picha za video.

Hata hivyo, anasema mapema mwaka huu, uongozi wa hifadhi ya Tarangire uliwaalika viongozi wa kata ya Mamire na yeye (Mary) akitokea kijiji cha Mamire, alishiriki ziara hiyo.

“Tulipoingia hifadhini nilishangaa kuwaona wanyama ambao sikuwahi kuwaona kabla na wengine nilikuwa ninawashuhudia kwenye picha za video,” anasema.

Mary ambaye ni mama wa watoto watatu, anasema baada ya ziara iliyofanyika Tarangire, amekuwa miongoni mwa watetezi wa uhifadhi na utangazaji wa utalii wa ndani.

“Zamani nilikuwa nafuata mkumbo kwa kuamini kwamba hifadhi kama ya Tarangire na wanyamapori waliomo ni adui zetu, lakini sasa hivi nipo mstari wa mbele kuzitetea,” anasema.

Anaongeza, “jamii ikishirikishwa kwa kina kuujua undani wa manufaa ya hifadhi ama mapori ya akiba tunayoishi karibu nayo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mabalozi wengi wa uhifadhi na utangazaji wa utalii wa ndani.”

Mary anasema ni ukweli usiopingika kwamba jamii zinazoishi karibu na hifadhi ama mapori ya akiba, zimekuwa zikiathirika kutokana na kuvamiwa na wanyamapori pori wanaoharibu mali hasa mazao yao.

“Utakuta mtu anamiliki eneo dogo lenye mazao ambayo yakiharibiwa na mnyamapori, basi hilo linakuwa jambo la uadui mkubwa,” anasema.

Si Mary pake yake, bali wananchi kadhaa wanaozizunguka hifadhi na mapori ya akiba, wanaielezea hali hiyo kuwa inachochea dhana kwamba hifadhi na wanyamapori ni adui wa binadamu.

Lakini Mary anasema pamoja na uhalisia huo, ushirikishwaji umma katika masuala ya hifadhi kunaweza kuwafanya watu wakatoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wa wanyamapori ili kudhibiti uharibifu unaotokana na wanyama hao.  

Anasema hata inapotokea kuwapo ushirikishwaji huo, jamii zinazozizunguka hifadhi na mapori ya akiba, zitajiepusha na vitendo vya uharibifu badala yake kuendeleza uhifadhi, kwa vile wanatambua umuhimu wake kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Mary anasema hali hiyo imedhihirika kwake binafsi ambapo sasa, anazungumzia umuhimu wa Tarangire katika hafla zinazofanyika ndani na nje ya wilaya ya Babati, kisha kuwashawishi watu kuitembelea.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mamire,  Juma Jumbe, anaungana na hoja za Mary, akisema uongozi wake uliotambua umuhimu wa kuishirikisha jamii hiyo iujue umuhimu wa Tarangire, hivyo kuwa mabalozi wa uhifadhi na kuutangaza utalii wa ndani.

Jumbe, anasema walipata mwaliko wa watu 18 wanaotoka kwenye maeneo yanayozunguka Tarangire, kwenda kuitembelea hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu ya kukuza ujirani mwema unaochochea uhifadhi na utalii wa ndani.

Walisema waliokuwamo kwenye ziara hiyo ni pamoja na wawakilishi wa vyama vya kimila, wazee, viongozi wa umma na dini na wajumbe wa kamati ya mazingira.

Jumbe anatoa mfano kuwa kutoishirikisha jamii katika kiwango kizuri kwenye uhifadhi wa Ziwa Babati lililo miongoni mwa vivutio vya utalii, kumeliweka katika hatari ya kutoweka.

“Si rahisi kuzungumzia uhifadhi na utalii wa ndani kama jamii zinazozunguka hifadhi na mapori ya akiba, hazitashirikishwa badala yake maliasili hizi zionekane kuwapo kwa ajili ya wageni kutoka nje hasa wazungu,” anasema.

Jumbe anasema kabla ya kuboreshwa kwa mpango wa ujirani mwema kati ya Tarangire na jamii zinazoishi kuizunguka, palikuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira na uuaji wa wanyamapori.

“Pamoja na changamoto zilizojitokeza hivi karibuni, lakini sasa hivi kuna mwamko unaoiwezesha jamii kuendeleza uhifadhi na kutangaza utalii wa ndani,” anasema.

Hassan Limbega ni Afisa Ardhi na Maliasili katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, anasema ushiriki wa jamii zinazolizunguka pori la akiba la Selou, umekuwa nyenzo muhimu katika uhifadhi wake.

Limbega, anasema ushiriki huo umeiwezesha jamii kutambua mambo ya msingi yakiwamo ya kisheria kama vile ilivyo kosa kuua mnyamapori.

“Baada ya kuwashirikisha wananchi sasa wamekuwa wasaidizi wa karibu wa idara yetu katika kukabiliana na changamoto za uhifadhi na kuwadhibiti wanyama wanaoharibu mali zao,” anasema.

Anasema, tofauti na ilivyokuwa awali, hivi sasa anapotokea mnyamapori kuingia eneo la makazi na kuharibu mali yakiwamo mazao, jamii zinazoishi pembezoni mwa Selou hazimuui, bali kuwasiliana na askari wa wanyamapori.

Limbega, anasema zaidi ya uhifadhi jamii hizo zinasaidia pia udhibiti wa ujangili hasa wa wanyamapori wadogo wanaowindwa na walio miongoni mwao.

Kwa mujibu wa Limbega, mpango wa ushirikishi wa jamii zinazoizunguka Selou wilayani humo, umefanikisha kuundwa kwa askari wa hifadhi kwenye ngazi za vijiji, wakiwa wanasimamiwa na asasi za kiraia (CBOs).

Hata hivyo, Limbega anapendekeza kwamba katika kukuza utalii wa ndani, ipo haja ya kutangaza vivutio vingine visivyojulikana, vikiwamo vinavyopatikana kuzunguka hifadhi na mapori ya akiba.

Pia anasema kwa vile uhifadhi na utalii wa ndani unahitaji rasilimali watu na fedha, ipo haja kwa mamlaka husika kufikiria namna bora ya kuziongeza ili zikidhi mahitaji kwa maeneo husika.

Meneja Uhusiano wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal Shelutete, anasema uwekezaji katika kuboresha huduma za jamii, ni moja ya ajenda zenye kipaumbele kwa mamlaka hiyo.

Shelutete, akizungumza ofisini kwake mjini Arusha, anasema mbali na kuwekeza katika huduma hizo, Tanapa kama ilivyo kwa mamlaka za maliasili nyingine, imekuwa ikisaidia shughuli za kijamii hususani kupitia asasi za kiraia zilizo kwenye sekta za umma na binafsi.

Hali hiyo inastahili kuwa miongoni mwa mafanikio yenye taswira chanya katika uhifadhi na uenezi (utangazaji) wa utalii kwa raia wa ndani.

Ingawa ni hivyo, yapo maeneo kadhaa ambayo yanapaswa kuboreshwa zaidi, ili azma ya uhifadhi na utangazaji wa utalii wa ndani, viwe endelevu kwa maslahi ya nchi na watu wake.

Kwa hali ilivyo sasa, wananchi wanaoishi maeneo ya kuzizunguka hifadhi za taifa, mamlaka za uhifadhi na mapori ya akiba, wanatoa ushauri unaolenga kuongeza kiwango cha ushiriki wao kwenye uhifadhi na utangazaji wa utalii wa ndani.

Tanzania kupitia taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, hususani Tanapa, imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jitihada kadha wa kadha zinafanyika katika kuendeleza uhifadhi na kutangaza utalii wa ndani.

Sekta ya utalii imekuwa moja ya vyanzo vya mapato, na kutokana na takwimu za mwaka jana zilizotolewa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ulichangia asilimia 17 ya pato ya taifa.

Ingawa ni hivyo, takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya Watanzania wanaoshiriki utalii wa ndani ni ndogo ikilinganishwa na wanaotoka nje ya nchi, hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuondokana na kasoro hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI 

Polisi yanasa meno ya tembo ya 25m/= kwenye treni


Na Moshi Lusonzo
29th December 2013


Kaimu kamanda wa kikosi cha polisi cha Tazara, (SSP) Inocent Mgaya (katikati) akiwa na OCD wa kituo hicho SP, Bakari Makuka (kushoto) na SP, Shaaban Hussein wakionesha meno ya tembo kwa waandishi wa habari.
Meno ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 25.5 yamekamatwa ndani ya treni ya Tazara katika stesheni ya Kisaki, Wilaya ya Morogoro Vijijini,  yakisafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam.

Meno hayo yalikamatwa Alhamisi wiki hii, ikiwa ni siku chache baada ya mawaziri wanne kuondolewa madarakani kutokana na kutosimamia vizuri zoezi la 'Operesheni tokomeza majangili '.

Akizungumza jana, Kaimu kamanda wa kikosi cha polisi cha Tazara, (SSP) Inocent Mgaya, alisema katika tukio hilo alikamatwa Ally Juma (26), maarufu Ngagari, fundi seremala  na mkazi wa Kisaki.

Kamanda Mgaya, alisema walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna mtu amebeba meno ya tembo ndani ya treni hiyo iliyokuwa ikitokea Zambia kwenda jijini Dar es Salaam.

Alisema baada ya kufanya upekuzi katika behewa namba M2, walifanikiwa kumkamata mtu huyo akiwa na mabegi mawili yakiwa yamehifadhiwa pembe 14 za tembo na kipande kimoja cha jino la kiboko.

"Tulipomkamata na kumfanyia upekuzi tuligundua begi la kwanza lilikuwa na vipande vinane vya pembe nane na la pili aliweka vipande saba," alisema Kamanda Mgaya.

Alisema kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, walibaini vipande hivyo vya pembe za tembo vina uzito wa kilo 29 vyenye  thamani ya Dola za Kimarekani 1950 (Sh. 25,520,000).

Jino la kiboko lilikutwa na uzito wa gramu 900 lenye thamani ya Sh. milioni 2.5.

"Nataka kuweka wazi kwamba usafiri wa treni ni kwa ajili ya watu kupata usafiri wa uhakika na sio vinginevyo, polisi wapo  makini kuhakikisha hakuna mtu anayetumia chombo hiki kwa uhalifu," alisema.

Aidha, kwenye tukio hilo polisi walikamata mifuko miwili ikiwa imepakiwa madawa ya kulevya aina ya bangi.

Hata hivyo, hakuna mtu aliyekamatwa kuhisika na mifuko hiyo yenye uzito wa kilo 19.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Habari Zaidi


Saturday, December 28, 2013

Poachers slaughter several precious Tanzania jumbos


By Lucas Liganga,The Citizen Reporter

Posted  Saturday, December 28   2013 at  09:02
In Summary
  • The tourism industry and conservationists are  concerned about  the rate of elephant killings which pose a threat to anti-poaching operations
 Dar es Salaam. Hardly a week in the whole of 2013  passed without wananchi reading a screaming banner headline about the poaching of elephants –not only in Tanzania’s electronic and print media but also in the international press.
To be precise, 2013 saw Tanzania turning into a killing field for elephants, a crisis that threatened to bring the jumbos to the brink of extinction.
During independence in 1961, Tanzania had 350,000 elephants; but poaching had resulted in the population of the jumbos going down to about 55,000 in 1989. Thanks to an anti-poaching operation christened Operation Uhai in 1989/90, the population rose to more than 100,000.
This operation was followed by another called Operation Kipepeo in 2009 headed by deputy commissioner of police (DCP), Venance Tossi. The outcome of this operation was not made public apart from the daily basis reporting of arrests of poachers and seizure of fire arms used in poaching.
As memories of these two anti-poaching operations were relegated to the archive, fresh reports emerged this year indicating that poachers kill an estimated 30 elephants every day, or about 850 every month. The number of elephants dropped from 130,000 in 2002 to 109,000 in 2009 and wildlife experts have warned that the entire population could be wiped out by 2020 if the trend continues.
This gloomy prediction forced the government to form another operation on September 5, 2013—the infamous Operesheni Tokomeza Ujangili.
To the dismay of wildlife conservationists this operation was suspended indefinitely due to claims of civilian abuse, torture, extortion and murder.
By the time it was suspended in the first week of November, 952 suspected poachers had already been arrested, 104 pieces of ivory seized, 631 firearms—including 13 military weapons—had been seized during the operation jointly conducted by the Tanzania People’s Defence Forces, Tanzania Police Force and Tanzania National Parks.
Addressing Parliament in Dodoma last month, the President Kikwete said the special anti-poaching operation which was suspended last month will soon continue, adding  that every thing should be done to ensure the project is running again as soon as possible. “The problem (poaching) is frightening. A lot of ivory has been impounded inside and outside the country. In total we are talking about 36 tonnes of tusks which equals to around 15,000 elephants,” said President Kikwete.




Friday, December 27, 2013

Utalii umeanza kunufaisha wazawa Z’bar


Na Theodatus Muchunguzi
27th December 2013

Hoteli ya Hideaway Nungwi Resort iliyoko katika ufukwe wa Nungwi, ambayo ni miongoni mwa hoteli zenye viwango vya juu duniani.
Baada ya uhasama wa kisiasa kuzuia maendeleo ya sekta mbalimbali visiwani Zanzibar, utalii umeanza kufufuka na mchango wake kwa uchumi wa visiwa vya Pemba na Unguja unaongezeka.

Inakadiriwa kuwa hivi sasa mchango wa sekta ya utalii kwa pato la Zanzibar umefikia asilimia 27 na kwamba asilimia 80 ya fedha zinazotokana na sekta hizo ni za kigeni.

Ongezeko la pato katika sekta hiyo linatokana na kuibuka kwa hoteli za kitalii, nyingi miongoni mwa hizo zimejengwa katika maeneo ya fukwe za bahari na wageni wanaofikia katika hoteli hizo idadi kubwa ni watalii kutoka mataifa tajiri duniani.

Unapotembelea maeneo hayo, kwa hakika huwezi kuamini kuwa upo Zanzibar, unaweza kufanya makosa kuamini kuwa siyo Pemba au Unguja kwa sababu ya uwingi wa wageni kutoka mataifa mbali mbali ya Ulaya na Marekani.

Kamisheni ya Utalii Zanzibar, inasema tangu kuanzishwa kwa sera ya kukaribisha vitega uchumi na sekta binafsi, asilimia 80 ya miradi iliyotekelezwa ni ya sekta ya hoteli na huduma za utalii za viwango mbalimbali.

Jumla ya hoteli 354, ikiwa ni pamoja na nyumba za kulaza wageni zenye vyumba 7,421 na vitanda 14,076 vimeshamiri visiwani Zanzibar, hasa katika maeneo ya pembezoni mwa miji zikiwa na uwezo wa kuhudumia wageni 169,223 mwa mwaka 2012.

Sekta hii hivi sasa imetoa mchango wa ajira za moja kwa moja kwa vijana 13,017 na zaidi ya ajira 45,000 kwa zile nafasi zisizo na uhusiano wa moja kwa moja. Matarajio ni kwamba zaidi ya asilimia 50 ya waajiriwa Zanzibar watatokana na sekta ya utalii ifikapo mwaka 2020.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Watembeza Watalii Zanzibar (Zato), Hassan Ali Mzee, anatofautiana na takwimu za Kamisheni ua Utalii kwa kusema kuwa sekta ya utalii inatoa ajira za moja kwa moja 15,000 na zisizo za moja kwa moja 60,000.

Anaongeza kusema kuwa watalii wanasaidia kuongeza pato kwa kuwa mtalii mmoja analazimika kulipa Dola 95 anapoingia nchini, Dola 50 kwa ajili ya viza na Dola 45 kwa ajili ya kodi ya matembezi, chakula na hoteli.

Viongozi wa hoteli nyingi zinazomilikiwa na wageni wanasema kwamba hoteli hizo zimeweza kutoa ajira kwa wananchi wengi, hususani Wazanzibari na baadhi kutoka Tanzania Bara.

Kwa mfano, hoteli ya Hideaway Nungwi Resort iliyoanzishwa miezi saba iliyopita na miongoni mwa hoteli zenye viwango vya juu duniani, ina wafanyakazi takribani 250 huku wafanyakazi 200 wakiwa ni wa kutoka Zanzibar na wengine 50 wanatoka Tanzania Bara.

Hoteli nyingine ya Diamond Dream of Zanzibar ambayo nayo inasema ina imeajiri zaidi ya wafanyakazi 250, wafanyakazi takribani 190 mwanatoka Zanzibar na wengine kati ya 50 na 60 ni kutoka Tanzania Bara.

Ujenzi wa hoteli hizo umewakomboa wananchi kwa kuwapatia ajira ambazo zinawapatia kipato cha kukidhi mahitaji yao muhimu kwa maisha ya maisha yao ya kila siku.

Hata hivyo, hakuna mazuri yasiyo na kasoro. Pamoja na Watanzania kunufaika na ajira hizo, yako malalamiko kuwa nafasi za juu katika hoteli za kitalii zinashikiliwa na wageni huku wenyeji wakiishia kufanya kazi ndogo ndogo za kupika, kufua, kusafisha vyumba na bustani.

Raia wengi wa kigeni ambao wanatajwa kuwa wameajiriwa katika hoteli hizo na kushika nafasi za juu na kulipwa zaidi ni wa kutoka Kenya.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa wazawa wa Zanzibar na Watanzania bara wanakwama kupata ajira katika hoteli za kitalii kwa kukosa uelewa wa lugha pamoja na kufanya kazi kwa mazoea.

Kutokana na hali hiyo, watalii wanajikuta wanashindwa kupata huduma kwa usahihi kutokana na tatizo la mawasiliano baina yao na wahudumu.

Meneja wa mauzo na masoko wa Hideaway Nungwi Resort, George Kiruku, anasema kuwa moja ya changamoto zinazoikabili hoteli hiyo ni wafanyakazi wenyeji kutokuwa na uwezo wa lugha za kigeni na kwamba kwa hali wanawasiliana kwa matatizo na watalii wanaotoka nje ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Kiruku ambaye ni raia wa Kenya, anasema watalii wanahitaji huduma za viwango na kwamba kwa sasa wakilalamika kuwa huduma wanazopewa na wenyeji kwamba haziridhishi.

“Wageni (watalii) wanalalamikia kutohudumiwa kwa wakati. Mgeni anaweza kuagiza chakula, lakini akacheleweshewa,” anasema Kiruku.

Hata hivyo, Kiruku anasisitiza kwamba wengi waliopata nafasi za ajira katika hoteli hiyo ni wa maeneo jirani huku akiahidi kwamba mpango wa kuwasaidia vijana na kinamama wa eneo la Nungwi unaandaliwa.

Kwa upande wake, Meneja wa hoteli ya Diamond Dream of Zanzibar, Allan Ochner, anapozungumzia changamoto ya lugha, hususan Kiingereza kwa wafanyakazi wenyeji, anasema huko nyuma kulikuwapo na malalamiko hayo, lakini kadri wanavyopatiwa mafunzo wanafanya vizuri.

Ochner ambaye anatoka Mombasa, Kenya, anasema kwamba wafanyakazi wanaosikiliza na kufuata maelekezo pamoja na kupenda kujiendeleza wanapandishwa vyeo, lengo ikiwa ni kuwapa motisha wa kijiendeleza zaidi.

“Tunapima utendaji wao na wanaobainika kufuata maelekezo wanapandishwa. Sasa baadhi ya idara wanaziongoza wafanyakazi wa Zanzibar,” anasema.
Omar Ibrahim, msimamizi wa shamba la viungo la Kizimbani, anawashauri vijana kujiendeleza na kuchangamkia ajira zilizoko katika sekta ya utalii.

Anasema baada ya kujiendeleza, yeye na wenzake sasa wamepata sifa ya kuwa wanawatembeza na kuwahudumia watalii wanaofika katika mashamba yao ya viungo.

“Tujitahidi kusoma hata kama tumeshindwa shule tujiendeleze katika kozi mbalimbali,” anasema Ibrahim ambaye shamba lake na wanakijiji wenzake linazalisha pilipili manga, vanilla, hiliki, alovera, mrangirangi, majani ya chai na mdarasini.

Afisa Mipango wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Miraji Ukuti Ussi, anakiri kwamba lugha ni changamoto miongoni mwa wafanyakazi katika hoteli za kitalii, lakini anasema hatua kadhaa zinachukuliwa kukabiliana nayo.

Dk. Ussi anasema kuwa moja ya hatua hizo ni kuboreshwa na kupanuliwa kwa Chuo cha Utalii cha Maruhubi ili kutoa huduma zinazohitajika za utalii.
Baadhi ya hoteli za kitalii zinalalamika kwamba hali ya hewa ya Zanzibar haitabiriki, kiasi kwamba wakati mwingine inabadilika ghafla na kusababisha usumbufu katika shughuli za uzalishaji wa mboga mboga zinazopendwa na watalii wengi.

Ochner wa Diamond Dream of Zanzibar, ambayo ina uwezo wa kuhudumia watalii 200 kwa siku na kulipa kodi hadi Dola za Marekani 500,000 kwa mwaka anasema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakwaza na kushindwa kuzalisha mboga hizo.

Hata hivyo, Kamisheni ya Utalii Zanzibar, kupitia kwa Ofisa wake wa Mipango, Dk. Miraji Ussi, anathibitisha kuwapo kwa malalamiko hayo, lakini anasema kuwa kuna mpango unaotekelezwa wa kuihamasisha Mamlaka ya Kutangaza Vitega Uchumi Zanzibar (Zipa) na wananchi kujihusisha na uzalishaji wa kilimo cha kisasa.

Anasema kuwa mpango huo ulianza baada ya baadhi ya hoteli kusema kuwa hali ya hewa wakati mwingine inakwaza uzalishaji wa baadhi ya mahitaji ya vyakula.

Mashamba ya viungo:
Uzalishaji wa viungo ni fursa nyingine muhimu kwa sekta ya utalii Unguja ambako kuna mashamba katika maeneo ya Kijichi na Kizimbani katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Shamba la Kijichi ambalo lina ukubwa wa ekari nne linamilikiwa na wanakijiji wapatao 300 na limewawezesha kuwapa ajira vijana kadhaa wanaolihudumia na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.

Omar Ibrahim, ni mmoja wa vijana hao anayesema watalii wengi wanapenda kutembelea shamba hilo kujionea na kununua aina kadhaa ya viungo kama pilipili manga, majani ya chai, binzari, vanilla, mdarasini, hiliki, mrangirangi na alovera na kuwaachia fedha.

“Tunapata fursa za kazi za vibarua na kupata fedha nyingine tunazoachiwa na watalii baada ya kuwapa huduma nzuri. Vijana wasio na ajira waje tushirikiane,” anasema Ibrahim ambaye hata hivyo anasita kueleza kiasi halisi cha fedha wanazopata kwa siku kutoka kwa watalii.


Hifadhi ya Jozani:
Hifadhi ya Taifa ya Jozani Chwaka Bay iliyoko katika wilaya za Kati na Kusini katika Mkoa wa Kusini Unguja, ni kivutio kingine kikubwa cha utalii Zanzibar.
Hifadhi hiyo ya miti ya asili yenye ukubwa wa hekta 5,000 ni sehemu inayovutia watalii wengi kwenda pamoja na watafiti kupita kufanya tafiti zao.

Kivutio kikubwa zaidi katika hifadhi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2004 ni kuwa na kima mwekundu pekee duniani, ambaye pia anafahamika kwa jina la Punju kutokana na sumu aliyonayo.

Inasemekana kwamba mbwa au mnyama yeyote akila nyama yake, ananyonyoka manyoya. Hifadhi hiyo pia inahifadhi paa nunga ambaye pia ni adimu.
Ali Ally Mwinyi, Ofisa wa Idara ya Misitu ambaye pia ni Meneja wa Uhifadhi Ghuba ya Chwaka, anasema kiasi cha Sh. milioni 180 zinalipwa na watalii takribani 24,000 kwa mwaka wanaoingia katika hifadhi hiyo.

Mwinyi anasema kuwa nusu ya mapato yatokanayo na hifadhi hiyo yanabakia katika jamii ya wanavijiji vinavyozungukwa na hifadhi na kiasi kinachobaki kinakwenda serikalini.
Rais Shein anasemaje kuhusu utalii?

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, anapozungumzia utalii, anasema Serikali ya awamu ya saba, iliingia madarakani ikiwa na dhamira kubwa ya kuimarisha sekta ya utalii na kwamba lengo ni kuibadilisha sura ya sekta hiyo ili iweze kuwa na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa taifa.

Dk Shein anasema angependa kuona utalii unakuwa sekta kiongozi ili iweze kuwa kichocheo cha sekta nyingine.

Anasema Kamati za Utalii kwa Wilaya za Unguja na Pemba tayari zimeundwa ili kuziimarisha huduma za utalii kwenye Wilaya, na kuwahamasisha wananchi kuendeleza miradi ya uzalishaji mali, hususan kilimo cha mboga mboga, matunda, biashara ndogo ndogo na kadhalika.

Chuo cha Maendeleo ya Utalii kilichoko Maruhubi hivi sasa kinaimarishwa ili kitekeleze kwa ufanisi zaidi lengo la kujenga rasilimali watu wenye ujuzi, utaalamu na stadi zinazohitajika.

“Lengo letu ni kukifanya chuo hicho kiendelee kutoa mafunzo ya utalii unaotilia maanani, mila, utamaduni na desturi zetu pamoja na hifadhi ya mazingira. Hivi sasa Serikali ishachukua hatua ya kuibua maeneo mapya ya vivutio vya utalii yakiwamo mapango, michezo ya asili, matamasha, maeneo ya hifadhi ya wanyama,” anasema na kuongeza:

“Hatua zinachukuliwa za kuimarisha utalii wa kumbukumbu za kihistoria kwa maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba, kuimarisha utalii wa kiutamaduni na kuuendeleza utalii wa ndani wenye kuyatunza mazingira.”

Rais Shein anasema juhudi za pamoja zinazochukuliwa na serikali na sekta binafsi zimepelekea kuongezeka kwa idadi ya watalii kututembelea Zanzibar. Katika mwaka 2011 Zanzibar ilipokea watalii wapatao 175,067 na mwaka 2012 watalii 169,223 walifika nchini.  
CHANZO: NIPASHE

Wednesday, December 25, 2013

Court rejects DPP`s objection to bail for Chinese nationals


By Karama Kenyunko

25th December 2013
The High Court in Dar es Salaam rejected an objection by the Director of Public Prosecution (DPP) to bail for three Chinese nationals charged with unlawful possession of elephant tusks.

The three were denied bail on Monday for their safety and public interest. Earlier, the DPP had filed a certificate objecting to the granting of bail to the accused under section 148(4) arguing that the court has no authority to hear the application as the case is premature.

The accused Chinese nationals are Huang Gin (50), Xu Fujie (22) and Chen Jinzhan (31).

Advocate Rweyongeza contended that the section quoted by the DPP was not proper. He said the DPP was supposed to file the certificate after the committal proceedings had taken place.

“Your honour, the certificate is premature and has been filed using the wrong provision,” he said.

For her part, prosecutor Faraja Nchimbi argued that the certificate was properly filed and covered all requirements of the law. She added that the court does not have the jurisdiction to hear the said bail application.

Making a ruling on the arguments Judge Teemba agreed with advocate Rweyongeza that the DPP’s certificate was improperly filed under a section of the Criminal Procedure Act (CPA) and therefore rejected the application.

The prosecution, led by State Attorney Biswalo Mganga, requested the court to give it seven days to file a counteraffidavit. 

Judge Teemba ruled that this should be made on January 3 and the defence should submit a rejoinder, if any, on January 10 when the case comes up for hearing.

It was earlier alleged that the accused committed the offence on November 2, this year, at Kifaru Street, Mikocheni B in Kinondoni District. 

It was further alleged that on the said date the accused, jointly and together, were found in unlawful possession of 706 pieces of elephant tusks. 

These weighed 1,889kgs, and were worth 5,435,865,000/-, property of the government. It was also alleged that the accused had no permit from the director of wildlife and the tusks represented the slaughter of about 400 elephants. 

It was claimed that the tusks were found in sacks of garlic at the house of the Chinese nationals.
All the accused were remanded in custody.
SOURCE: THE GUARDIAN

Barrick to pay abused Tarime women


 

Barrick Gold has also been embroiled in controversy over a series of gang rapes by security guards at its Porgera gold mine in Papua New Guinea.PHOTO|FILE 
By Citizen Reporter and Agencies

Posted  Wednesday, December 25  2013 at  11:27
In Summary
The incidents occurred over a period of several years before their public disclosure in a company statement in May 2011.
African Barrick Gold (ABG) this week announced that it would give cash payments and other compensation to 14 women who were sexually assaulted by police and security guards at its North Mara gold mine in Tanzania. Quoting the company’s statement, Canadian newspaper Mail & Globe reported that ABG, a subsidiary of Toronto-based Barrick Gold Corp, said it spent two years questioning more than 200 people in an independent investigation of the sexual assault allegations, which were first disclosed by Barrick in 2011.
“Fourteen women are presently receiving remediation packages,” the company said in a statement to the newspaper on Thursday.
“Although the exact components of each package depends on the individual claimant, they have included cash compensation, sponsored employment to provide job training, financial and entrepreneurial training, education expenses for claimants’ children, relocation expenses, home improvements, health insurance for claimants and their families and counselling services.” ABG described the 14 women as “victims” of sexual assault, not just complainants.
The case began when about 10 women alleged that they were arrested at the North Mara mine site and sexually assaulted by company security guards or police. The incidents occurred over a period of several years before their public disclosure in a company statement in May 2011. The women told investigators that they were taken to holding cells and threatened with imprisonment if they refused to have sex with the police or guards.
According to the Mail & Globe, the company said it found the complaints “credible” and “highly disturbing”. It launched its own investigation by a team of experienced experts, and it turned over its findings to the Tanzanian police, although last week it was unable to say whether the police will lay criminal charges against the perpetrators.
Barrick Gold has also been embroiled in controversy over a series of gang rapes by security guards at its Porgera gold mine in Papua New Guinea. An investigation by Human Rights Watch concluded that the attacks were “brutal” and “extreme.” As many as 170 women were raped at the Porgera mine, activists say.
Ms Catherine Coumans, a researcher at Mining Watch Canada, an Ottawa-based non-profit organisation, said ABG had kept “too much secrecy” over the North Mara sexual assault cases.
The ABG statement is its first disclosure about the investigation since 2011, but it fails to disclose key details of the investigation and the compensation, she said.
A British court recently criticised ABG for launching a “pre-emptive strike” against a group of Tanzanian villagers who had filed a lawsuit against the company after six of their relatives were killed by police at the North Mara gold mine and several others were injured. The lawsuit alleges that the company is responsible for the deaths because the police are an “integral part” of the mine’s security and operate under an agreement with the company.
The ruling by the British High Court, issued earlier this month, said the company had acted in haste by launching a legal tactic the court described as “a Tanzanian torpedo” to force the lawsuit to be heard in a Tanzanian court, rather than a British court.
Leigh Day, the British law firm representing the Tanzanian villagers, said the villagers were served with legal papers “out of the blue” after the mining company quietly launched a court case in Tanzania seeking to declare that it cannot be held responsible for the actions of the police.
“These papers demanded that our clients, who do not have Tanzanian lawyers, promptly appear before a court that is some 1,200 kilometres and a two-day bus ride away from where they live,” the law firm said.
he firm obtained an injunction to prevent the company from proceeding with its Tanzanian case against the villagers, and later the company dropped the Tanzanian case.
In its statement issued last week, the company said it had “no intent to make a pre-emptive strike.” It also noted that the British courts had criticised some aspects of the original lawsuit against the company by the villagers.