Sunday, March 16, 2014

SIKU YA TAIFA YA KUTUNDIKA MIZINGA TAREHE 18 MACHI 2014 WILAYANI MLELE


Siku ya Taifa ya Kutundika Mizinga itaadhimishwa kitaifa mkoani Katavi katika wilayani Mlele tarehe 18 Machi 2014. Aidha, siku hiyo mikoa mingine itaadhimisha kimkoa katika wilaya na vijiji vilivyochaguliwa. Kauli Mbiu ya mwaka huu ni:“Boresha Ufugaji Nyuki, Linda Ubora wa Mazao Yake”.

Madhumini ya siku hii ni kuendeleza Ufugaji Nyuki unaolenga kuongeza idadi ya wafuga nyuki, usimamizi bora wa makundi ya nyuki na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kw akuzingatia ubora na teknolojia za kisasa. Aidha, siku hii inatumika kuhamasisha uhifadhi endelevu wa raslimali za misitu na nyuki.

Siku hii itakuwa chachu ya kuwahamasisha wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kwa wingi katika ufugaju nyuki wa kisasa.

Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), ambaye atashiriki kutundika mizinga katika msitu wa Mlele Kusini eneo la Kanembela na baadaye kuhutubia wananchi.

Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa wito kwa wadau na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kufanikisha siku hii kwenye maeneo yaliyopangwa na maeneo binafsi.


No comments:

Post a Comment