Na Charles Kayoka, Mwananchi
Posted Alhamisi,Marchi20 2014 saa 16:56 PM
Posted Alhamisi,Marchi20 2014 saa 16:56 PM
Kwa ufupi
Mji
kuwa wa kiutalii ni lazima uendelezaji wa maeneo, ujenzi wa majumba, barabara,
na matumizi ya maeneo ya mji (landscape management), uwe katika mazingira ya
kuwavutia watalii wa ndani na wa nje.
Nashukuru kwa simu chache nilizopata
kutokana na makala yangu ya wiki iliyopita ambayo ilizungumzia Mwanza ina uwezo
wa kuwa mji wa kiutalii, lakini mpaka sasa hakuna matangazo ya kutosha.
Ninaposema kuwa mji wa kitalii, au
utalii, nina maana kubwa sana, lakini la msingi ni serikali ya eneo husika
inapaswa kuwekeza vya kutosha sana katika miundombinu, utangazaji wa vivutio,
na utengenezaji wa matukio ambayo yenyewe yataufanya mji na matukio hayo kuwa
vivutio (destinations).
Mji kuwa wa kiutalii ni lazima
uendelezaji wa maeneo, ujenzi wa majumba, barabara, na matumizi ya maeneo ya mji
(landscape management), uwe katika mazingira ya kuwavutia watalii wa ndani na
wa nje. Mji wa Mwanza, kama ilivyo miji mingine nchini haiendelezwi kwa mtazamo
huo, na huwezi kuuangalia mji tu bali unapaswa kuwa na mtazamo wa kiutalii. Kwa
mfano kuwa na hoteli kubwa, hakuufanyi mji kuwa na sifa ya utalii. Watalii
hawaji kuona hoteli, wanataka kuona nini kipo ndani mji. Lakini pia wanataka
kuona namna gani wanaweza kufika sehemu mbalimbali za mjiji na namna gani
watafika huko kwa kuwa na mfumo wa barabara ya uhakika.
Mji unapaswa kuwa mfumo wa uongozaji
(navigation indications) ambao hautamlazimu mtalii kuuliza maswali mara kwa
mara bali kuwa na mfumo ambao utamsaidia mtalii kufika moja kwa moja kwenye
eneo husika la utalii. Mji unapaswa kuwa kivutio (destination) kwa sababu ndani
kuna maeneo au matukio ambayo yanasaidia kuwafanya watalii wauchague kama mji
wao wa kuutembelea. Mwanza kuna vivutio vingi sana, lakini havijaendelezwa ili
kuwavutia watalii na kuuchagua mji huo kuwa wa kitalii, hasa watalii wa nje.
Vivutio viilivyondani ni; ziwa na eneo
la utalii la Bujora ambavyo havijatangazwa. Kazi ya kuutangaza mji ni jambo
ambalo haliepukiki. a utalii. Kwa kweli kuutangaza utalii kunahitaji mikakati
ili kuwavutia watu. kushangaa.
Ckayoka28@yahoo.com, 0766959349
No comments:
Post a Comment