Na Daniel
Mjema, Mwananchi
Posted Jumapili,Marchi23 2014 saa 12:27 PM
Posted Jumapili,Marchi23 2014 saa 12:27 PM
Kwa
ufupi
Ni katika miamba ya Kilele cha
Mawenzi, ambapo eneo hilo haliruhusiwi kupandwa. Helkopta yatumwa kwa ajili ya
kuwaokoa.
Moshi. Mtalii mmoja raia wa Ujerumani, Jeane Traska (32) amenasa
katika miamba ya kilele cha Mawenzi cha Mlima Kilimanjaro baada ya kwenda
kinyemela eneo hilo ambalo haliruhusiwi kupandwa na watalii isipokuwa kwa
ruhusa maalumu.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro (Kinapa), Erastus Lufungilo, alilithibitishia gazeti hili jana
kuhusu kunasa kwa mtalii huyo pamoja na mwongoza watalii (Guide) aliyejulikana
kwa jina la Athman Juma kutoka Kampuni ya Nordic Tours.
“Ni kweli kuna tukio hilo na wote
wawili wamenasa huko tangu asubuhi na tunafanya kila jitihada kuokoa maisha
yao, lakini kimsingi walikwenda huko kinyemela kwa sababu wao walitakiwa kwenda
Kibo lakini wao wakaenda Mawenzi, alisema.
Meneja Uhusiano wa Shirika la
Hifadhi za Taifa Nchini (Tanapa), Paschal Shelutete, aliliambia gazeti hili
jana kuwa mtalii huyo pamoja na mwongozaji huyo wa watalii wamenasa katika
miamba ya kilele hicho baada ya kamba waliyokuwa wakiitumia kunasa kwenye
miamba.
Shelutete alisema mtalii huyo
alianza kupanda mlima huo Machi 18 mwaka huu kwa kutumia njia ya Rongai, safari
ambayo ingewachukua siku tano, lakini kwa sababu ambazo hazijulikani alibadili
njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo.
“Tanapa kwa kushirikiana na kampuni
yaNordic Tours tunaendelea na jitihada za kuwaokoa kwa kutumia askari wetu
wazoefu pamoja na helkopta itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa kutegemea hali ya
hewa itakavyotulia. Sasa hivi kuna mawingu mazito”alisema.
Kwa mujibu wa Shelutete, ili mtalii
aweze kuruhusiwa kupanda kilele hicho cha Mawenzi ambazo ni miamba, hutakiwa
kujaza fomu maalumu ili aweze kubeba dhamana yako mwenyewe endapo utapatwa na
matatizo katika kupanda kilele hicho.
No comments:
Post a Comment