Rais Jakaya Kikwete, akipokea mfano
wa helikopta kutoka kwa mtoto wa bilionea wa pili duniani, Warren Buffett,
Howard ambaye familia yake kupitia Mfuko wa Warren Buffett Foundation watatoa
helikopta moja itakayotumika kupambana na ujangili katika Pori la Akiba la
Selous. Picha ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Na Mpoki Bukuku, Mwananchi
Posted Ijumaa,Marchi14 2014 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Akikabidhi mfano wa helkopta kwa
Rais Kikwete, Buffett alisema amevutiwa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali
ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili hususan wa tembo na faru.
Dar es Salaam. Familia ya bilionea namba mbili nchini Marekani, Warren
Buffett imeunga mkono juhudi za kupambana na ujangili nchini kwa kuchangia
helikopta moja.
Familia ya Warren Buffett imeamua
kutoa msaada huo kupitia Mfuko wa Howard Buffett Foundation, baada ya
kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali.
Helikopta hiyo itatumika kwa ajili
ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili katika hifadhi za taifa na mapori ya
akiba nchini.
Msaada huo ulikabidhiwa juzi kwa
Rais Jakaya Kikwete na mtoto wa bilionea huyo, Howard Buffett, ambaye yuko
nchini kwa mapumziko ya kitalii.
Akikabidhi mfano wa helkopta kwa
Rais Kikwete, Buffett alisema amevutiwa na kazi nzuri inayofanywa na Serikali
ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili hususan wa tembo na faru.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu alisema wamepokea kwa furaha ufadhili huo, ambapo utahusisha
mafunzo kwa marubani wawili nchini Marekani ama Afrika Kusini kutokana na
matakwa ya wizara.
“Wametuambia pesa ipo tayari ila ni
jukumu letu sisi kama Serikali kuchagua aina ya helikopta tunayoitaka. Itakuwa
na uwezo wa kubeba watu sita na kwa sasa tunaangalia kama tuchukue Bell ama
Ecopter, wataalamu wanashughulikia,” alisema.
No comments:
Post a Comment