Thursday, September 5, 2013

TAARIFA KWA UMMA


HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
USAHIHI WA TAARIFA ZA MGENI ALIYEUWAWA NA TEMBO NJE
YA HIFADHI YA TARANGIRE
Baadhi ya vyombo vya habari nchini jana na leo vimekuwa vikiripoti juu
ya tukio la kuuwawa na tembo kwa mgeni kutoka Marekani
anayefahamika kama Thomas Vardon Macfee (58) tarehe 31.08.2013 katika
Hifadhi ya Taifa Tarangire.
Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kuweka usahihi wa taarifa
zilizoripotiwa kama ifutavyo:-
Tukio la mgeni husika lilitokea nje ya Hifadhi ya Tarangire katika kijiji cha
Kakoi kambi ya Tarangire River Camp, wakiwa wanafanya utalii wa
kutembea kwa miguu “Walking Safari”. Baada ya kuvamiwa na
kuumizwa, mgeni huyu alifikishwa katika zahanati ya Hifadhi ya
Tarangire na watumishi wa kambi aliyofikia iliyo nje ya hifadhi kwa ajili
ya matibabu ya huduma ya kwanza na alipofikishwa, alifariki dunia.
Hivyo basi, Shirika linapenda kusahihisha kuwa tukio lililopelekea kifo
cha mgeni lilitokea nje ya Hifadhi ya Tarangire na si ndani kama
ilivyoripotiwa.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO
HIFADHI ZA TAIFA
S.L.P 3134
ARUSHA
05/09/

No comments:

Post a Comment