Thursday, November 14, 2013

Multi-million dollar jumbo tusks seized



By Mwinyi Sadallah ,The Citizen 

Posted  Thursday, November 14   2013 
In Summary
For about two months before the operation was called off, the police, military and wildlife officials carried out a joint operation against poachers amid a surge of killings of elephants and rhinos.
Zanzibar. A 40-foot container filled with elephant tusks hidden in plastic bags was seized here yesterday. The ivory haul was reported to be destined for China. This development comes just a few days after some 797 tusks were seized in three raids. This means about 400 elephants were slaughtered for their tusks.
Details made available to The Citizen indicate that the container was seized at Malindi Port by police, the Zanzibar Anti-Smuggling Unit and the Tanzania Intelligence Service after a tip-off.
Zanzibar Police Commissioner Musa Ali Musa told The Citizen the tusks were packed in 50-kilogramme plastic bags. To conceal their load, the smugglers packed sea shells in some plastic bags and placed them carefully at the main entrance to the container.
According to Mr Musa, the container was brought to Malindi port ready for export by a clearing and forwarding agent. He declined to name the agent. Police have reportedly launched an investigation to identify the owner of the cargo and the ship that ferried the cargo.
Police in Zanzibar did not give the street value of the consignment, saying an investigation was underway to establish the owners of the seized cargo.
Mr Musa said police and other government officials were unloading the cargo to determine the number of tusks. He added: “All I can tell you is that we have launched investigations, but I can’t go into details such as revealing the name of the agent (clearing and forwarding). In doing so, I might interfere with the investigation process.”
Tourism and Natural Resources Minister Khamis Kagasheki urged those who have information on the smuggling network to come forward and tell the authorities what they know in order to curb the illegal trade.
Zanzibar’s Minister in the President’s office (Special Forces), Mr Haji Omar Omar Kheir, said the Zanzibar government would consult with the Mainland team on the trial of the culprits.
“We don’t have a Natural Resource Act so we will sit with our counterparts on the mainland to decide whether the trials will take place there or in the Isles using the anti-economic sabotage laws,” Mr Kheir added.
The seizure of the container comes a few days after the government suspended the anti-poaching campaign amid reports of human rights violations by officers engaged in the campaign.
For about two months before the operation was called off, the police, military and wildlife officials carried out a joint operation against poachers amid a surge of killings of elephants and rhinos.
Last year, Parliament was told poaching was out of control with an average of 30 elephants being killed for their ivory every day. In August 2011, Tanzanian authorities seized more than 1,000 elephant tusks hidden in sacks of dried fish at Zanzibar port that were destined for Malaysia.
Last year, more than 150 Chinese citizens were arrested across Africa—from Kenya to Nigeria—for smuggling ivory. There is growing evidence that poaching rises in elephant-rich areas where Chinese construction workers are building roads.
Most of the illegal ivory—experts say as much as 70 percent—is destined for China. The Chinese have coveted ivory for centuries but never before have so many of them been able to afford it. China’s economic boom has created a vast middle class, pushing the price of ivory to a stratospheric $1,000 per pound on the streets of Beijing.



Kontena la meno ya tembo lakamatwa Zbar


Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi


Posted  Alhamisi,Novemba14  2013 
Kwa ufupi
Limekamatwa Zanzibar ambako hakuna sheria inayohusu wanyamapori, bali watuhumiwa wanaweza kushtakiwa kwa uhujumu uchumi
Zanzibar.Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, vimekamata kontena la futi 40 likiwa limepakia meno ya tembo yaliyohifadhiwa kwenye mifuko ya nailoni yenye ujazo wa kilo 50, yakisafirishwa nje ya nchi.
Meno hayo yalikamatwa Bandari ya Malindi majira ya alasiri jana na polisi, Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM), Maofisa wa Usalama wa Taifa na raia wema waliotoa taarifa kuhusiana na mpango huo.
Akizungumza mjini hapa jana, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema uchunguzi wa tukio hilo umeanza ikiwamo kuwasaka wamiliki wa mzigo huo kupitia Kampuni ya Wakala wa Kusafirisha Mzigo, iliyopewa kazi hiyo.
Kamishna Mussa alisema kazi ya kupakua mzigo na kuchana gunia moja baada ya jingine tayari imeanza chini ya ulinzi mkali wa askari ili kujua idadi ya meno na thamani yake. Alisema mzigo huo ulikamatwa kupitia taarifa za siri zilizofanikisha kugundua kontena hilo lililokuwa na meno hayo yaliyochanganywa na kuwekwa katikati ya makombe (sea shells).
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema wakati umefika kwa Watanzania kushiriki na kuvikabili vitendo vya ujangili vyenye lengo la kuangamiza wanyamapori hasa Tembo na Faru.
Balozi Kagasheki alisema kazi inayofanywa na askari ni sehemu ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, huku akiwapongeza askari kwa kufanikisha jukumu lao.
Naye Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais (Idara Maalumu na Vikosi vya SMZ) Haji Omar Kheir alisema hakuna sheria za nyara za Serikali kutokana na visiwa hivyo kutokuwa na wanyamapori wa aina hiyo, lakini wahusika wanaweza kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi ya Zanzibar iliopitishwa mwaka huu.

Unafiki wa wabunge hawa aibu kwa taifa


Makala
Toleo la 325  Raia Mwema
13 Nov 2013
  • Balozi Kagasheki aachwe achape kazi
KATIKA kipindi cha miaka mitatu iliyopita kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa wabunge, wanaharakati, vyombo vya habari na wananchi wa kulaani mauaji ya tembo. Mbali na kuulani huko, wamekuwa wakiilaumu serikali kwa kutokuchukua hatua muafaka kumaliza tatizo hili.
Wengine wamedai hali ni mbaya, wakitaka sheria itungwe ili majangili wapigwe risasi, wapo waliotaka waziri mwenye dhamana ajiuzulu huku wengine wakilalamika na kutaka tumwachie Mungu!
Ni kweli hali ya ujangili dhidi ya tembo nchini imekithiri na hakuna mbadala zaidi ya kuchukua hatua muafaka. Waziri mwenye dhamana, Balozi Khamisi Kagasheki, akiweka wazi hili katika Bunge la bajeti lililopita alihadharisha kuwa inaandaliwa operesheni maalumu.
Kwamba ‘Operesheni Uhai’ iliyofanyika mwishoni mwa miaka ya 1980 ingekuwa ndogo kulinganisha na hiyo iliyokuwa ikiandaliwa.
Katika utatuzi wa tatizo lolote kuna mbinu kuu tatu. Mbinu za kawaida ambazo ni endelevu (proactive), mbinu zinazolenga kuzuia tatizo (preventive au deterrent) na mbinu za kujibu mapigo (reactive).
Wakati mbinu mbili za kwanza zinatoa muda mrefu wa kujipanga na aghalabu huwa shirikishi, mbinu ya tatu ni ya haraka na inachukua sura ya udharura na pengine haitoi fursa kwa demokrasia.
Kwa mfano, kinapozuka kipindupindu mahali au nyumba inapoungua huwezi kuahirisha hatua ili kungoja ridhaa ya kikao au kuandaa semina kuelimisha watu namna ya kukabili tatizo.
Ni kweli kwamba mbinu mbili zilizotajwa hapo juu (proactive na preventive) zimekuwa zinatumiwa na mamlaka husika kupambana na tatizo la mauaji ya tembo. Hata hivyo, sababu kadhaa zimegeuza ujangili wa tembo kuwa janga na hivyo kufanya njia hizi mbili zisiwe ‘toshelevu’.
Tembo wengi wanauawa kutokana na kukua kwa soko katika nchi za mashariki ya mbali. Aidha, ongezeko la wageni kutoka katika nchi hizi; ongezeko la wahamiaji haramu na urahisi wa wahalifu kupata silaha za kivita; kushuka kwa maadili na uzalendo miongoni mwa Watanzania watumishi na wasio watumishi; kuimarika kwa miundombinu (barabara) na njia za mawasiliano (simu za mikononi) na jiografia yetu (kupakana na Bahari ya Hindi) ni mambo yanayochangia ongezeko la mauaji ya tembo na biashara haramu ya meno yake.
Katika hali ambayo tembo wengi wanakufa kila siku kiasi cha kutishia uwepo wake katika miaka michache ijayo, hakuna njia nyingine yoyote ya kukabili tatizo hili zaidi ya kuchukua hatua za dharura na haraka (reactive measures). Na hili ndilo lililofanywa na serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana ambaye alitangaza ‘Operesheni Tokomeza’.
Naamini hatua hii ni ya kupongezwa. Waziri Kagasheki amethubutu na nina hakika akisaidiwa na kuungwa mkono ataweza. Kuna wanaodai operesheni hii si suluhisho. Kwa bahati mbaya Watanzania tumekuwa wepesi kukosoa bila kutoa suluhisho mbadala. Ni vema wale wanaokosoa wakatuambia dawa mujarabu ya kumaliza tatizo hili ni ipi.
Wakati matunda ya operesheni hii yameanza kuonekana, inashangaza wanapojitokeza wanasiasa na ‘wanaojiita wanaharakati’ kumshambulia waziri ambaye wengi wanaomfahamu hawajawahi kutilia shaka uadilifu na utendaji wake kwa umma.
Kimsingi, wanasiasa na wanaharakati hawajamtendea haki Kagasheki, hawajazitendea haki maliasili zetu na hawajaitendea haki nchi hii. Ninachokiona hapa ni baadhi ya wanasiasa kutumia mbinu chafu kujijenga kisiasa. Lakini pia kuna uwezekano kuwa wapinzani wa vita hii wana maslahi kutokana na wao binafsi au jamaa zao kuhusika katika dhambi hii kubwa ya kuangamiza tembo.
Ama nyingi ya asasi (NGOs) zinazodai kutetea haki za binadamu inaeleweka kuwa nyingi zipo, si kwa maslahi hasa ya Watanzania, lakini ni mashine za watu za kuvuna pesa. Asasi hizi, mara nyingi zimekuwa zikiunda hoja hasi dhidi ya serikali ili kujenga uhalali wa kupata pesa kutoka kwa wafadhili wao na ndio maana watendaji wake wana utajiri wa kutisha.
Wangekuwa wakweli wangeonesha pia kusikitishwa na vifo vya askari waliokufa kwa kuuawa na majangili. Inakuwaje mtu kulalamikia ng’ombe kukamatwa ndani ya hifadhi lakini asiguswe na vifo vya binadamu vinavyosababishwa na majangili? Huo uzalendo uko wapi? Ni vema asasi hizi zikaendelea kuwepo na kutengeneza pesa, lakini si kwa mbinu chafu kama hizo.
Kauli ya mbunge mmoja kuwa eti “..watu waliokamatwa ndani ya hifadhi wamepigwa na kuumizwa wakati majangili wa tembo wameachwa” si kwamba tu inakatisha tamaa, bali pia inaonesha ni aina gani ya wabunge tulinao.
Mbunge angewasaidia Watanzania kama angetuambia waliokamatwa ndani ya hifadhi walifuata nini na kwa sheria gani. Aidha, alitakiwa kutusaidia kuwa majangili wa tembo wanaohusika ni kina nani hasa! Ieleweke kuwa hii vita si ya Kagasheki peke yake.
Hivyo hao wanaowajua majangili wamsaidie ili sheria ichukue mkondo wake. Sasa mbunge aliyekula kiapo cha kuilinda katiba na kutumikia umma anapojua wahujumu kama hao halafu akakaa kimya mpaka Kagasheki aje awajue, anatoa matumaini gani kwa Watanzania?
Kwa tafsiri yangu, mbunge wa namna hii ni msaliti wa nchi yetu. Mwingine, tena waziri analalamikia msaidizi wake kukamatwa. Hivi msaidizi wako akituhumiwa kwa uhalifu ana kinga gani ya kutokukamatwa na kuhojiwa?
Operesheni yoyote ile duniani kote inapotokea huwa kuna kasoro za hapa na pale. Hata nchi zilizoendelea zimejikuta zikifanya makosa katika operesheni kama hizi na pengine hata kusababisha watu wake kupoteza maisha (rejea Marekani na vita ya magaidi).
Lakini pia hata kwenye sayansi za tiba karibu dawa zote huwa na madhara ya kando (side effects) lakini baadaye hupatikana tiba ya kudumu. Labda wanasiasa na wanaharakati wetu wangetusaidia sana kama wangetupa mfano wa operesheni yoyote ile ambayo haikuwahi kuwa na kasoro.
Hata hivyo, kama wote tunakubali kuwa mapambano dhidi ya ujangili wa tembo ni vita ya lazima, hivi kukijitokeza kasoro unaamua kuachana na hiyo vita? Inapotokea unasafiri kwa gari ikapata pancha, unaamua kuachana na safari na kumfukuza dereva?
Binafsi sitaki kuamini wale wanaomshambulia Waziri Kagasheki wana uchungu na nia ya dhati na maisha ya Watanzania wenzao. Ninachoamini ni kwamba kuna ajenda iliyojificha. Nashawishika kuamini hivyo kwa kuwa ni wabunge hawa hawa waliokuwa wanapiga kelele kwamba tembo wanakwisha, sasa wamemgeuka Balozi Kagasheki.
Leo Balozi Kagasheki anapofanya kweli wabunge hao hao wanadai ajiuzulu kwa kuvunja haki za binadamu! Hivi huu unafiki wa wabunge wetu utaisha lini? Hivi maslahi gani ya nchi wanayopigania?
Pale Kagasheki alipotangaza kusitisha ‘Operesheni Tokomeza’ (tangazo ambalo nahisi pengine hata yeye hakulifanya kwa ridhaa yake), sikutarajia wabunge wangekubaliana nalo. Cha ajabu, wengi waliochangia tamko hili la wizara walijielekeza kwenye lawama dhidi yake na wahusika wengine kwenye operesheni hii na kuonyesha kuguswa kwa masikitiko na kitendo cha ng’ombe pamoja na watu kukamatwa.
Katika michango yote, wabunge wengi wakiwemo wale wanaopenda kujipambanua kama wazalendo hawakuonyesha kukerwa na mauaji ya tembo! Hili linazua maswali. Je, kelele zote walizokuwa wakipiga dhidi ya ujangili zililenga kukejeli wananchi kwamba wana uchungu na rasilimali za taifa?
Je, katika hali kama hii ambapo wanaonyesha wazi kupinga operesheni, ni kitu gani kitasababisha tusiwaunganishe na mtandao wa ujangili? Je, kwa nini tusiamini kuwa lawama zote na chuki zinazoelekezwa kwa Balozi Kagasheki zimejificha kwenye maslahi ya kisiasa zaidi?
Nawasihi Watanzania wote wenye nia njema na hatima ya maliasili zetu kuendelea kuunga mkono kwa nguvu zote juhudi za kupambana dhidi ya janga la ujangili wa tembo na rasilimali nyingine za taifa. Tuwe makini na wanasiasa wanafiki wanaotumia shida, misiba na majanga yetu kujinufaisha kisiasa.
Namsihi Waziri Kagasheki na watendaji wengine wote wenye mtazamo chanya kwa taifa letu wasikatishwe tamaa. Ieleweke kuwa, katika hali ambayo watu wameingia kwenye siasa kwa mbinu chafu, si rahisi kwa watu waadilifu, makini na wenye viwango vya hali ya juu vya utendaji kama Balozi Kagasheki kukubalika.
Watapigwa vita na kuchafuliwa bila sababu za msingi. Imani kubwa iko kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ndiye aliyempa dhamana Waziri Kagasheki.
Hotuba yake aliyotoa bungeni, inatoa matumaini kwamba fitna na chuki zinazoelekezwa kwa Balozi Kagasheki na wasioitakia mema nchi yetu kwa kivuli cha uzalendo na kutetea haki za binadamu zitashindwa.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mwandishi wa makala hii anaitwa Elifuraha Mchangila


Monday, November 4, 2013

Wachina meno ya tembo wachunguzwa



Na Fidelis Butahe, Mwananchi
  Jumatatu,Novemba4  2013 
  
Kwa ufupi
Wakati Feleshi akieleza hayo, Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, huku akisisitiza kuwa atalitolea ufafanuzi leo kama akipata kibali cha kufanya hivyo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya raia wa China kukamatwa na vipande 706 vya meno ya tembo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) Eliezer Feleshi amesema wanasubiri uchunguzi wa suala hilo kukamilika.


Wakati Feleshi akieleza hayo, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, huku akisisitiza kuwa atalitolea ufafanuzi leo kama akipata kibali cha kufanya hivyo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

“Unajua ile ni ‘task force’ iliyoanzishwa na waziri mwenyewe, na amelizungumzia, sasa mimi siwezi kusema kilichokwishazungumzwa na waziri,” alisema Kamanda Kova. 

Juzi Kagasheki aliongoza operesheni ya kuwasaka watu wanaojihusisha na ujangili katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni sambamba na polisi na maofisa usalama na kufanikiwa kuwakamata raia watatu wa China, Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wakiwa na meno hayo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Feleshi alisema kazi yake ni kupambana na uhalifu na kufafanua kuwa uchunguzi ukikamilika, taratibu za kufikishwa mahakamani zitafanyika.

“Tunasubiri uchunguzi ukamilike kwanza, kisha taratibu zingne zitafuta kwa mujibu wa sheria,” alisema Feleshi.

Meno hiyo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini.

Saturday, November 2, 2013

Ujangili ukiendelea kuchekewa utamaliza wanyama

                         Munubhi Munubhi


WAZO binafsi ni kuamini kuwa kama kuna utatu mtakatifu, mfano wa ule wa mbinguni, basi utatu huo mtakatifu kwetu Tanzania ni Ikulu, Mahakama na Bunge tukufu, mahali ambapo hakika panasimamia na kuwakilisha mamlaka, haki na usawa ili kudumisha amani nchini.

Wakati tukiwa na taasisi hizo ‘takatifu’ hususan Bunge, tena moja, lenye wajibu muhimu wa kutunga sheria na kuisimamia Serikali katika kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kumezuka minong’ono kwamba baadhi ya wawakilishi wetu hao wamegeuka kuwa ‘watetezi’ wa watuhumiwa mbalimbali likiwamo hili la ujangili tena ndani ya chombo cha kutunga sheria!

Zipo taarifa mbalimbali zinazonukuliwa na vyombo vya habari kama vile: ‘Ujangili kulitesa Bunge’ na kadhalika; na wabunge kukinzana vikali huku suala la ujangili likifahamika wazi wazi miongoni mwa Watanzania kuwa ni moja ya tuhuma za makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria zetu hizo hizo zilizotungwa na kupitishwa na Bunge letu.

Kama hivi ndivyo, ni kwa vipi sasa katika suala hili la ujangili ambalo ni tuhuma nzito ya uhalifu linazusha kuwepo kwa pande mbili kinzani bungeni, moja ikiwa mtetezi mkuu na kwa kauli za hisia kali hasa baada ya upande mwingine kutoa taarifa na hata ushahidi wa awali kwa wahusika wanaojihusisha wakiwamo wale walionaswa.

Wazo jepesi na mtazamo wangu ni kuwa hawa ‘watetezi’ wanaotumia kauli kubwa, nzito na za hisia kali kuwatetea hata baadhi ya watuhumiwa walionaswa na vyombo vingine vya dola katika ujangili hakika hawawatendei haki Watanzania na vyombo vingine husika vya dola na wala utetezi huo haujengwi kwa kuzingatia msingi wa utawala bora, kwani zipo mahakama ambapo ni mahali mahususi kwa utetezi  kama huo kwa wahusika.

Pasipo shaka utetezi kama huo ambao huenda hauzingatii misingi ya utawala bora, yaani wa kuzingatia mifumo ya sheria unaweza kutengeneza na kuzusha hisia miongoni mwetu wananchi tunaowakilishwa kwamba pengine watetezi hao wana masilahi binafsi katika suala la ujangili na si bure.

Kwa mantiki hiyo, ndiyo sababu kwa sasa kuna kushutumiana kwa hali ya juu kuhusu majangili ni kina nani, wakati wanajulikana na hata kufikia hatua ya kuomba kutajana kwa majina kwa wahusika humo humo bungeni.

Lililo dhahiri na la kujiuliza ni kuwa: Je, ni kweli  kwamba uhalifu wa ujangili umepiga hodi bungeni kwa baadhi ya wabunge kujihusisha na uhalifu huo tena kwa kutumia kofia za heshima na utukufu wa Bunge letu?

Hapa sinuii kamwe kusema kuwa waheshimiwa wabunge au baadhi yao wanajihusisha na uhalifu wa ujangili nchini, la hasha, lakini kinachosemwa na wao wanachosema, wakiwa pia ni wananchi wana ndugu na marafiki zao ambao kuwatetea hao juu ya ujangili kunazusha shaka kuwa utetezi huo si bure, bali huenda ni utetezi wa kimasilahi.

Ndiyo sababu habari zinazonukuliwa na vyombo vya habari ambazo hazijakanushwa pia zinasema: ‘Ujangili kulitesa Bunge’, ndipo najiuliza kulitesa kwa vipi? Hivi majangili wamo bungeni?

Jibu la swali la maoni haya laweza kuwa jepesi au gumu kwa kuwa yawezekana likajibiwa ‘ndiyo’ au likajibiwa ‘hapana’ pasipo kutaka kuzingatia takwimu za waliosema ndiyo au hapana. Lipo tatizo.

La muhimu kuzingatia hapa ni kuwa, hakika hatuna budi kuwa makini sana kwani Watanzania walio wengi kwa sasa si wale wa miaka ya 47, wanao upeo wa juu wa uelewa na wenye ufahamu wa kutosha kabisa, hivyo watambuzi na wadadisi wa kufahamu na kutambua mambo yao muhimu ya kitaifa na hali mbalimbali zenye mushkeli na zinazopelekwa kimzaha na kwa mazoea.

Ni mtazamo wangu kuwa huenda katika suala la ujangili ambalo ni moja ya tuhuma za makosa ya jinai linapobainika na kutolewa taarifa hususan hata kuwepo watuhumiwa waliokamatwa haipendezi kuona na kusikia utetezi mkubwa na mzito namna ile bungeni huku hata wabunge wenyewe wakianza kutuhumiana hadharani kuwafahamu wahusika.

Ni bora tukapingana na tukaparaganyika ovyo katika masuala ya itikadi za vyama kwa ngazi yake husika, lakini inapofika kwenye ngazi ya masuala ya masilahi ya kitaifa hatuna budi kuachana na tofauti zetu za itikadi za vyama na kuwa kitu kimoja (Bunge moja) kwa masilahi ya taifa.

Hakika ujangili ni janga kwa utalii wetu na ukichezewa chezewa kimzaha na kimazoea hivi hivi hakuna mnyama atakayesalimika nchini kwani mifano ipo mingi.


Maoni: 0758 999 777.



Shehena pembe za ndovu zakamatwa Dar es Salaam



Na Goodluck Eliona, Mwananchi

Posted  Jumapili,Novemba3  2013 

Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.
Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.
Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung .
Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.
Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.
Mbali ya kushuhudia shehena ya pembe hizo, alionyeshwa gari maalumu aina ya Toyota Noah ambalo watuhumiwa hao hulitumia kutoa pembe porini na kuyaingiza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika eneo la tukio mara baada ya kuwakamata alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na matokeo ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imesitishwa na Serikali juzi baada ya wabunge kuilalamikia.
Waziri Kagasheki alisema kwamba katika harakati za kutaka kuwakamata watuhumiwa hao walitoa Sh30 milioni kwa ajili ya kujaribu kuwahonga askari.
“Walitaka kuwahonga askari ili wasikamatwe,” alisema huku akionyesha noti za fedha hizo.
Alisema wabunge wanaomtaka ajiuzulu kwa madai kwamba Operesheni Tokomeza Ujangili imesababisha mauaji ya watu na mifugo wanapoteza muda kwa kuwa mwenye mamlaka ya kumtoa ni Rais Jakaya Kikwete pekee.
“Sasa mimi nasema kunitoa haitakuwa rahisi anayeweza kunitoa ni yule aliyeniweka,” alisema.
Alisema ipo mikakati inayofanywa na baadhi ya wabunge kutaka kuwang’oa baadhi ya mawaziri kwa masilahi binafsi ya kisiasa.
Itakuwa ni jambo la ajabu kwamba kila mtu akiingia madarakani wanataka atoke, watatolewa wangapi?” alihoji na kuongeza kuwa operesheni hiyo ni muhimu kwa ajili ya kunusuru tembo wasiishe.
Alisema kwamba ni kweli kuna baadhi ya dosari zimejitokeza kwenye operesheni ikiwamo kuuawa kwa baadhi ya mifugo, lakini siyo kwamba zoezi zima halina manufaa.
Kagasheki alisema kama kasi hii ya kuuawa kwa tembo itaachiwa iendelee baada ya miaka 10 tembo wote watakuwa wameisha nchini.
Alisema hataki kuona utawala wa Rais Kikwete ukiondoka madarakani ukiwa na lawama ya kuachia majangili wawamalize tembo.
Mmoja wa watuhumiwa hao, Huang Qin alisema shehena yote ya pembe za ndovu iliyokamatwa nyumbani kwake ilikuwa ikiletwa kidogo kidogo na rafiki yake ambaye hakumtaja jina.
Akiongea kwa Kiswahili Qin alisema: “Mimi hii si yangu, kichwa yangu mbovu. Rafiki yangu alileta hii (pembe) kidogo kidogo.”
Januari mwaka huu, Gazeti La Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba Serikali ya Kenya imekamata shehena ya vipande 638 vya pembe za ndovu ambavyo ni sawa tembo 320 waliouawa.
Mzigo huo wa tani mbili ulikuwa kwenye kontena la mawe ya urembo (marumaru) kutoka Tanzania.
Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa tani nne za pembe za ndovu zenye thamani ya Dola za Marekani 3.4 milioni sawa na takriban Sh5.4 bilioni zilikamatwa Hong Kong Oktoba 20, mwaka jana, huku ikielezwa kuwa meno hayo yalikamatwa yakisafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.
Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na pembe za ndovu yenye thamani ya Sh18.4 milioni yaliyotengenezwa kama bangili tayari kusafirisha kwenda nje ya nchi.

Kijiji kilichoonja chungu ya kutokomeza ujangili



Charles Ndagulla-Tanzania daima

OKTOBA 13, mwaka huu ni siku iliyovuruga mwenendo wa maisha ya kila siku ya wananchi wa Kijiji cha Minziro kilichopo Kata ya Minziro, Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera baada ya kundi la wanajeshi wanaoendesha Operesheni Tokomeza Ujangili kuvamia kijiji hicho.
Kabla ya mkasa huo, siku hiyo ilikuwa tulivu. Waumini wa madhehebu mbalimbali waliamka asubuhi na mapema kwenda kumwabudu muumba wao kama ilivyo ada kila Jumapili.
Wakati waumini hawa wakirejea majumbani baada ya kutoka kwenye ibada, walikutana na upepo mbaya, na huu si ule unaoezua mapaa ya nyumba wala kung’oa miti, bali ni wa kipigo kutoka kwa walinda amani wetu.
Kila mmoja alikimbia kivyake kuokoa nafsi yake, na wale walioshindwa kuhimili mikiki ya mbio waliangukia mikononi mwa wapiganaji wetu, na hapo ndipo vipigo vilianza bila kuangalia sehemu ya kupiga.
Makamanda hawa hawakuishia kutembeza vichapo kwa raia wema tu, bali walienda mbali kwa kuchoma moto  baadhi ya nyumba za wananchi hao. Hakika Minziro iligeuka uwanja wa vita.
Wananchi hawa hadi sasa wamejawa na hofu, hawamwamini mtu yeyote wasiyemfahamu, na kila wamuonapo wanajificha kwenye mashamba ya migomba na baadhi yao vichakani wakitafakari kitakachotokea tena kwa siku hiyo.
Ni wachache waliothubutu kuwasogelea wanahabari waliotinga kijijini hapo kupata taarifa sahihi juu ya mkasa huo, lakini bado walikuwa wamejawa na hofu hadi hapo walipotolewa hofu hiyo na wenyeji walioambatana na wageni hao.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mulungu A, Boniface Ponsian, ambaye ni mmoja wa wahanga wa tukio hilo baada ya kukamatwa na kushitakiwa kwa madai ya kumiliki mazao ya misitu bila kibali, anasema hali bado ni tete kijijini hapo.
Anasema hadi sasa wananchi wengi wameyahama makazi yao na kukimbilia mafichoni, huku wakiwaacha watoto wadogo wakiwa hawana msaada wa wazazi wao.
Katika tukio hilo, wanajeshi hao wanadaiwa kuwafunga kamba wananchi na kuwaning’iniza kwenye magari yao wakiwa wamewainamisha vichwa chini, huku baadhi yao wanadaiwa kutapika kutokana na mtikisiko wa magari.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, zaidi ya wananchi 20 wa Kijiji cha Minziro waliumizwa vibaya na askari hao wanaodaiwa kuwapa mateso ya kila aina wakiwahusisha na wahamiaji haramu kutoka nchi za Burundi, Rwanda na Uganda na uvunaji wa mazao ya misitu kutoka msitu wa hifadhi ya taifa wa Minziro.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo wa kitongoji, wanajeshi hao baada ya kutembeza kipigo kwa wananchi kwa siku mbili mfululizo, walichoma moto nyumba yakiwamo maduka na kubomoa baadhi ya milango ya nyumba hizo.
Mwenyekiti huyo amewataja baadhi ya wahanga walioshambuliwa na askari hao kuwa ni Josephat Joseph, Edwin George, Didas Domisheni, Steven Serapioni, Sonko Yoronimu, Mkasa Mathias na Josephat Emmanuel.
Wanajeshi hao walichoma moto duka la mfanyabiashara Joseph Jovin wa Kijiji cha Minziro ambaye amekimbia makazi yake sanjari na Edward Mgowa ambaye alibomolewa milango ya nyumba yake na mwenyewe amekimbilia kusikojulikana yeye na mkewe na kuacha watoto wao watano wakiwa wapweke.
Katika tukio hilo, askari hao walimuumiza Josephat Emmanuel baada ya kupewa adhabu ya kutembelea magoti kwa umbali mrefu.
Pamoja na ukweli kwamba vyombo vya ulinzi na usalama Wilaya ya Misenyi vinafahamu operesheni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali mstaafu Issa Njiku, anadai hana taarifa yoyote juu ya tukio hilo.
Kwa mtu wa kawaida, anaweza akahisi  mkuu hyo wa wilaya haelewi wajibu wake, lakini ukweli ni kwamba anaficha uoza uliofanywa na walinzi hao wa amani ama kwa makusudi ama kwa kutokufahamu.
Si mkuu wa wilaya pekee, hata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Phillp Kalangi naye usemi wake ni huo huo wa DC Njiku, kwamba hana taarifa kutoka kwa OCD wake wa Misenyi, Yusuf Mtatifikolo, juu ya tukio hilo ikiwa ni wiki tatu zimepita tangu litokee.
Tukio hilo halikuishia siku moja, liliendelea siku ya pili ya Oktoba 14, ambako viongozi wa serikali ya kijiji hicho walikamatwa na kuwekwa mahabusu polisi kwa siku tano kabla ya kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa ndani ya siku mbili.
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Minziro, John Sali Kilibwa, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mulungu A, Ponsian na Anastazia Nestory ambao walihukumiwa Oktoba 22, mwaka huu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya sh milioni moja kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki mazao ya misitu bila kibali. Walilipa faini.
Wakati viongozi hao wakinusurika kwenda gerezani kutumikia kifungo, mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Minziro, yeye alikwenda gerezani baada ya kujikuta akikamatwa muda mfupi tu baada ya kuwatolea ushahidi viongozi hao wa kijiji. Amefunguliwa mashitaka matatu; kuvuna mazao ya misitu bila kibali, kusafrisha mazao ya misitu bila kibali na kumiliki mazao ya misitu kinyuume cha sheria. Kesi yake bado inaendelea.
Kwa muundo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa, Kanali mstaafu Massawe, ndiye mwenyekiti wake na katibu ni Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Mkoa (RSO). Ndivyo hivyo na wilayani ambako DC Njiku ni mwenyekiti wa kamati na katibu wake ni DSO.
Mbali na wanajeshi, wengine waliokuwa wakitekeleza operesheni ya kuwashambulia wananchi wa Kijiji cha Minziro na vitongoji vyake wanatoka  kwenye Idara ya Usalama wa Taifa, polisi na maofisa kutoka Idara ya Misitu ambayo kwa sasa inaitwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.
Swali ni je, nani atawaondolea hofu na mashaka wananchi hao wa Kijiji cha Minziro na vitongji vyake pamoja na vijiji jirani? Kwani hadi naandika makala hii, wanajeshi hao wangali wakivinjari kijijini hapo wakiwasaka watu waliowaumiza wenyewe kwa sababu wanazozifahamu wenyewe.
ndagullacharles@yahoo.com 078