Na Fidelis
Butahe, Mwananchi
Jumatatu,Novemba4 2013
Jumatatu,Novemba4 2013
Kwa ufupi
Wakati Feleshi akieleza hayo, Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, huku
akisisitiza kuwa atalitolea ufafanuzi leo kama akipata kibali cha kufanya hivyo
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
Dar es Salaam. Siku moja baada ya raia wa China kukamatwa na vipande 706 vya meno ya tembo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) Eliezer Feleshi amesema wanasubiri uchunguzi wa suala hilo kukamilika.
Wakati
Feleshi akieleza hayo, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova alisema uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, huku akisisitiza
kuwa atalitolea ufafanuzi leo kama akipata kibali cha kufanya hivyo na Waziri
wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
“Unajua
ile ni ‘task force’ iliyoanzishwa na waziri mwenyewe, na amelizungumzia, sasa
mimi siwezi kusema kilichokwishazungumzwa na waziri,” alisema Kamanda Kova.
Juzi Kagasheki aliongoza operesheni ya kuwasaka watu wanaojihusisha na ujangili
katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni sambamba na polisi na
maofisa usalama na kufanikiwa kuwakamata raia watatu wa China, Xu Fujie, Chen
Jinzha na Huang Qin wakiwa na meno hayo.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Feleshi alisema kazi yake ni kupambana na uhalifu na
kufafanua kuwa uchunguzi ukikamilika, taratibu za kufikishwa mahakamani
zitafanyika.
“Tunasubiri
uchunguzi ukamilike kwanza, kisha taratibu zingne zitafuta kwa mujibu wa
sheria,” alisema Feleshi.
Meno
hiyo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori
mbalimbali hapa nchini.
No comments:
Post a Comment