Meno ya Tembo yanayosakwa na
wafanyabiashara wakubwa huku soko lake likitajwa kuwa nchini China. Picha na
Maktaba
Na Waandishi wetu, Mwananchi
Posted Jumapili,Februari16 2014 saa 3:0 AM
Posted Jumapili,Februari16 2014 saa 3:0 AM
Kwa ufupi
Yalikuwa yakisafirishwa na
watuhumiwa watatu kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser kutoka Mtwara kwenda
Dar es Salaam.
Singida/Mtwara. Ikiwa ni muda mfupi
baada ya Rais Jakaya Kikwete kukiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu
linaloielemea Tanzania, Jeshi la Polisi mkoani Mtwara na Singida linawashikilia
watu wanne kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha nyara za Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Kaimu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga alisema kuwa jeshi
hilo limewakamata watu watatu wakiwa na meno ya tembo 58 yenye uzito wa
kilogramu 130.6 yenye thamani ya Sh700.3 milioni.
Kamanda alieleza kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa saa 11:00 alfajiri katika Kijiji cha Chungu Kata ya Nanyumbu,
Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakiwa katika kizuizi cha barabara ya
Mtambaswala – Mangaka wakielekea jijini Dar es Salaama.
“Tunawashikilia watu watatu kwa
tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali ambazo ni meno ya tembo 58 yenye
uzito wa kilogramu 130.6 na thamani ya 700.3 milioni, ambapo ni sawa na tembo
29 waliouawa yakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser,” alisema Kamanda
Manganga.
Alisema mbinu waliyotumia watuhumiwa
hao ni kukata sakafu ya gari ya chini ya kiti cha nyuma ya dereva na
kutengeneza tanki la bandia na kuweka meno hayo kisha kuweka kapeti juu yake.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Hamidu Ngunde (40) dereva, Geraldat Lukas (36) dereva na Boniphace Kosan (29)
wote wakazi wa jijini Dar es Salaam na kusema kuwa gari iliyotumika kusafirisha
meno hayo ni mali ya Hilali Rashid.
Wakati huo huo, Kamanda wa polisi
Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alisema wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa
mmoja, Februari 13 mwaka huu saa 2.30 asubuhi katika kizuizi cha Mazaoa ya
Misitu na Chakula kilichopo katika Kijiji cha Ukimbu Kata ya Mgandu, tarafa ya
Itigi, Wilaya ya Manyoni.
Alisema mtuhumiwa huyo alikuwa
akitumia gari aina ya Toyota lenye namba T.797 CQL kusafirisha nyara za
Serikali kutoka Kijiji cha Mwamangembe kwenda Itigi Mjini.
“Nyara alizokamatwa nazo mtuhumiwa
zilikuwa zimewekwa kwenye mabegi mbalimbali ya nguo,” alifafanua. Kamwela
alisema uchunguzi wa awali, umeonyesha kuwa vipande hivyo 21 vinakadiriwa kuwa
vya tembo wanne, vina uzito wa kilogramu 49 na thamani ya Sh43.1 milioni.
Kuvamiwa watalii kwatia doa Zanzibar
Na Herieth
Makwetta, Mwananchi
Posted Jumapili,Februari16 2014 saa 3:0 AM
Posted Jumapili,Februari16 2014 saa 3:0 AM
Kwa ufupi
- Akizungumza na Mwananchi Jumapili Mjini Zanzibar, Ferouz alisema mashambulizi hayo yalikuwa mabaya na yalichafua mfumo mzuri uliojengwa kwa kipindi kirefu katika visiwa hivyo, na kwamba yamerudisha nyuma juhudi za tume ya kukuza utalii ndani ya Visiwa vya Zanzibar.
Zanzibar. Katibu Mkuu wa Tume ya Utalii Zanzibar, Salehe Ramadhani Ferouz, amesema mashambulizi ya baadhi ya watalii waliowahi kutembelea visiwa vya Zanzibar, yameifanya picha ya kisiwa hicho cha amani kubadilika.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Mjini Zanzibar, Ferouz alisema mashambulizi hayo yalikuwa mabaya na yalichafua mfumo mzuri uliojengwa kwa kipindi kirefu katika visiwa hivyo, na kwamba yamerudisha nyuma juhudi za tume ya kukuza utalii ndani ya Visiwa vya Zanzibar.
“Kama tume, tuna wakati mgumu sana kwa sasa, japokuwa wageni katika tamasha hili la Sauti za Busara wamekuwa ni wengi, lakini tuna imani mwaka huu idadi ingekuwa kubwa zaidi, vitendo hivi ndivyo vinatukwamisha,” alisema.
Kwa mujibu wa ofisa huyo wa utalii wa Zanzibar, amesema kuwa wamekuwa wakikusanya wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani, tangu kuanzisha kwa tamasha hilo kwa mara ya kwanza miaka 11 iliyopita.
“Tunapata ahueni kubwa ya watalii wakati wa tamasha hili linalochukua muda wa siku nne, hoteli zote hapa mjini zimejaa, hii yote ni katika utalii wa muziki kwani wengi zaidi wanapendelea kuja msimu huu kushuhudia tamasha la muziki wa asili,” alisema Ferouz.
Kwa mujibu wa Ferouz, utalii ni sekta inayoongoza katika kukuza uchumi Zanzibar kwnai inachangia asiliamia 25 ya Pato la Taifa (GDP) na asilimia 80 ya ukusanyaji wa kodi za serikali.
Mwishoni mwa mwaka jana , Zanzibar ilikuwa inakabiliwa na mashambulizi ya tindikali, ambayo wanawake wawili kutoka Uingereza Katie Gee na Kirstie Trup, wote wakiwa na umri wa miaka 18, wakati wakitembea katika njia ya sehemu ya zamani ya mji mkuu wa Zanzibar, walimwagiwa tindikali na watu wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki.
Mashambulizi ya hivi karibuni yakiwamo ya upotevu wa wanandoa wa Kifaransa ambao wanaaminiwa kwamba waliuawa na kutupwa katika kisilinalozunguka nyumba yao.
Francois Cherer Robert Daniel na Brigette Mery walionekana kwa mara ya mwisho mwaka jana. Taarifa kwamba wamepotea zilianza kutangazwa Desemba 27 mwaka jana.
Govt defends Serengeti road
By Zephania Ubwani, The Citizen
Bureau Chief
Posted Sunday, February 16 2014 at 04:00
Posted Sunday, February 16 2014 at 04:00
In Summary
- Government Counsel Gabriel Malata told the East African Court of Justice that the highway would ease the movement of tourists to and from the area.
Arusha. The government has defended
the proposed highway across the Serengeti National Park, saying constructing it
will neither violate the East African Community (EAC) Treaty nor harm the
ecosystem.
Government Counsel Gabriel Malata
told the East African Court of Justice that the highway would ease the movement
of tourists to and from the area.
When the case was filed in December
2010, he explained, the government had not decided on whether to build a tarmac
or gravel road. After a feasibility study, Mr Malata said, the gravel road came
out on top--essentially because it would have no effect on the Serengeti
eco-system.
Mr Malata, the principal state
attorney, asked the court to dismiss the case filed by the Nairobi-based Africa
Network of Animal Welfare (ANAW) with costs. He argued that supporting ANAW
would frustrate the tourism sector in the entire region “because the road is
there to facilitate the movement of tourists”.
The EAC partner states were yet to
ratify the Protocol on Environment and Natural Resources, he added, making the
case premature.
ANAW argues that construction of the
road will be hazardous to the environment and animals in particular. The
group’s lawyer, Saitabao Kanchory Mbalelo told the court that construction of
the road across the national park infringes Articles 5 and 3 of the EAC Treaty.
London wildlife summit moves to choke off ivory
markets
Posted Saturday, February 15 2014 at 10:00
In Summary
- The London Declaration urges practical steps to end the illegal trade in rhino horn, tiger parts and elephant tusks that contribute to criminal activity worth more than $19 billion (14 billion euros) each year.
Related Stories
London. More than 40 countries including China and African states
have signed a declaration aimed at stamping out the illegal trade in wildlife,
in a move broadly welcomed by conservation groups.
The London Declaration urges
practical steps to end the illegal trade in rhino horn, tiger parts and
elephant tusks that contribute to criminal activity worth more than $19 billion
(14 billion euros) each year.
British Foreign Secretary William
Hague, who hosted Thursday’s meeting, said: “I believe the measures we have agreed
can mark a crucial turning point.”
Hague highlighted the attendance of
China and Vietnam, two major consumers of the banned products. Beijing sent
Forestry Vice minister Zhang Jianlong.
“I do welcome the involvement of
China (and) the constructive approach from their minister and from other Asian
countries, but there will be more work to do,” Hague said. He highlighted the
progress that China had made in reducing the number of sharks killed to make
shark fin soup, a traditional Chinese delicacy.
“The conference wants to follow this
example in other areas,” he said. Conservation groups gave the declaration a
largely positive reception, but said it did not go far enough.
Ms Mary Rice of the London-based
Environmental Investigation Agency said: “This has been an unprecedented
gathering, the first indication that many of the world’s governments are really
serious about combating organised wildlife crime.
“We would have liked them to go
further and, specifically with regard to ivory and tigers, close down legal
domestic markets.”
Tanzania, Chad, Gabon, Ethiopia and
Botswana announced a separate action plan to protect elephants of which 25,000
are killed each year by poachers, according to official estimates.
Botswana will organise a conference
in 2015 to evaluate progress on the initiative.
Opening the meeting, British heir to
the throne Prince Charles , said that while it was important to tackle
poachers, the key thing was to “attack demand” for rare creatures which are
used to produce traditional medicines and other products.
Charles said the declaration would
“address what is the most significant problem in my view -- that of demand for
and consumption of specific products from critically endangered wildlife. Most
recently, demand from Asia -- particularly China -- has fuelled the trade, but
we also know that the US and Europe are contributing to it.”
While estimates of the value of the illegal
trade in wildlife vary -- London’s Chatham House think-tank puts it at $10
billion -- all the participants agree that poaching is accelerating at an
alarming rate. (AFP)The conference heard that 1,000 rhinos were killed in South Africa last year compared with just 13 in 2007, and the number of tigers living wild in Asia has plunged from 100,000 to just 3,200 in the space of 10 years.
Martial arts film star Jackie Chan attended the conference to call for urgent action. He told AFP: “I don’t want my grandchildren to look in a book and say ‘what is that, rhino?’.
“We have already destroyed the earth enoughl
Wabunge watahadharisha ujangili kudhoofisha uchumi
Na Mwandishi
maalum
15th
February 2014
Sambamba na hilo, umetoa angalizo kwa serikali juu ya mikataba inayoingia na nchi za jirani hususani zile zinazohusika na ujenzi wa barabara kwasababu wimbi hilo linatumia mwanya huo kama sehemu mahususi ya biashara yao.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Umoja huo, ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Riziki Lulida, alisema ongezeko la wageni nchini, ambao wanaishi muda mrefu bila sababu maalumu limechangia kwa kasi kupotea au kuuawa kwa wanyamapori.
“Suala la kusimamia ujangili ni letu sote hivyo tuache malumbano pasipo sababu, tushikamane kwa pamoja kwa sababu hali ni tete ukilinganisha kundi hili limebebwa na watu wakubwa wanaotumia njia mbalimbali za kuangamiza rasilimali ya nchi.”
Alitoa mfano kuwa "awali tulishtushwa na taarifa za kuuliwa kwa wanyamapori sehemu za Kilindi mkoani Lindi, ambapo tulikutana na uongozi wa kijiji, lakini wahusika walidai hali ngumu ya maisha imechangia kuua wanyamapori hao” alisema Riziki.
Kwa upande wake mbunge wa Dole Zanzibar, Sylivester Mabumba (CCM), alisema miaka 10 ya nyuma taifa lilikuwa na idadi ya wanyamapori wengi ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya, Burundi, Rwanda, China, lakini kwa sasa wageni hao wameligeukia taifa.
Naye mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), alisema, umoja huo umesikitishwa na kauli ya mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa, juu ya Rais Jakaya Kikwete kuhusika na hujuma za ujangili huo, badala yake umesema kama ni pungufu ni wakawaida kwa kila kiongozi.
“Siasa iwe na mipaka yake jamani, kwanza tuna wasiwasi na kauli aliyoitoa Mchungaji Msigwa kwa sababu inaweza kuleta madhara makubwa ndani na nje ya nchi siku za usoni” alisisitiza Beatrice.
CHANZO:
NIPASHE
Sunday Feb
16, 2014
Atoboa baada ya
kutinga CNN, BBC
Wamo vigogo 40, baba lao liko Arusha
Wamo vigogo 40, baba lao liko Arusha
Rais Jakaya
Kikwete, amesema mtandao wa majangili unajulikana na jitihada za serikali
zimefanikiwa kukamata vigogo 40 walio kwenye mtandao mkubwa wa biashara ya
nyara hizo za serikali.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya BBC , jana asubuhi alisema watuhumiwa hao wamebainika kuwa wanajihusisha na mtandao kwenye ukanda wa Kaskazini na kwamba tajiri mkuu wa biashara hiyo naye amefahamika na kwamba anapatikana mkoani Arusha .
Akizungumza katika kipindi cha Amka na BBC , alikozungumzia ujangili, alieleza kuwa mtandao umefahamika na kwamba unahusisha matajiri na miongoni mwa watu hao 40 yupo tajiri huyo wa Arusha ambaye hakutaka kumtaja jina redioni.
“Tumeutambua mtandao huo hadi wakubwa zao ni matajari pale Arusha kuna mmoja mkubwa ambaye sitaki kumtaja jina alikuwa akiendesha biashara hiyo naye yupo kwenye kundi hili la watu 40 kazi iliyokuwa ikifanyika ni kuutambua huo mtandao kwa upana,” alisema.
Awali alisema Tanzania ilikuwa na tembo wengi barani Afrika na hata duniani wakati huo baada ya Uhuru walikuwa 350,000 na ilipofikia mwaka 1987 walipungua hadi 55,000.
Alisema hapo ndipo serikali ilipofanya maamuzi ya kuingiza jeshi katika mapambano ya kupambana na ujangili jambo lililosaidia kwa kiasi kupunguza tatizo.
Hata hivyo, alisema ilipofikia mwaka 1989 shirika linaloshughulikia haki za wanyama walioko hatarini kutoweka (CITES) ilifanya maamuzi ya kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu duniani.
Rais Kikwete alisema kwa mambo hayo mawili ikiwamo nguvu ya jeshi kuingilia kupambana na ujangili pamoja na biashara hiyo kupigwa marufuku duniani ilisaidia kupungua ujangili na tembo kuanza kuonekana.
Alisema ilipofika mwaka 2009 hesabu ilikuwa kubwa ambapo idadi ya tembo iliongezeka na kufikia 110,000.
Alipohojiwa juu ya gazeti moja la Uingereza la Daily Maili kumuandika kuwa hajafanya jitihada za kutosha kupambana na ujangili, alisema gazeti hilo limeandika uongo na kwamba serikali imejitahidi kufanya mikakati mbalimbali kuokoa maisha ya tembo na kupunguza ujangili.
Pembe hizo za ndovu wanaouliwa Afrika soko lake lipo katika nchi za Asia ikiwamo China.
Kikwete alisema jitihada mbalimbali zimefanywa ndiyo maana mtandao huo ambao unajihusisha na biashara ya meno ya tembo umegundulika.
Wakati Rais akiwa kwenye mkutano nchini Uingereza uliokuwa ukijadili ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na pembe za faru, polisi mkoani Singida wamemkamata George James na vipande 21 vya meno hayo.
Polisi ilisema meno hayo yenye thamani ya Sh. milioni 43 yana uzito wa kilo 49.
MAHOJIANO NA CNN
Wakati huo huo, ujangili umemfikisha Rais Kikwete, kwenye televisheni ya CNN ya Marekani, alikohojiwa akitakiwa kueleza vita dhidi ya majangili inayofanyika nchini.
Akihojiwa na CNN jijini London juzi, alisema Tanzania imefanya operesheni nyingi dhidi ya majangili na kuhimiza haja ya mataifa makubwa kusaidia juhudi za kupambana na ujangili huo.
Akijibu maswali ya Christiane Amanpour wa CNN, Rais alitaka dunia kuungana kusimamisha biashara ya pembe za ndovu.
Alieleza kuwa hatua hiyo itaondoa kichocheo cha mtu kuwaua wanyama hao
Alieleza kuwa wakati wa uhuru walikuwepo tembo 350,000 kabla ya kuibuka wimbi la ujangili mkubwa ulioiachia nchi tembo 13,000 pekee.
AHADI YA MSAADA
Akijibu swali kama kuna ahadi yoyote aliipata katika mkutano juu ya ulinzi wa wanyama pori uliofanyika London juzi, Rais Kikwete aliitaja Canada kuwa imeahidi kutoa Dola milioni mbili, wakati serikali ya Uingereza imeahidi kutoa msaada.
ALICHOTARAJIA
Alieleza kuwa kitu muhimu kwake na viongozi wa Afrika ni kufahamisha kuwa ili kuupiga vita ujangili kunahitajika rasilimali watu, kuwajengea uwezo askari wa wanyama pori wa kulinda wanyama.
Rais alisema alikuwa anategemea nchi zilizoendelea hasa Uingereza na Marekani kusaidia upande wa mafunzo ya askari wa wanyama pori na pia kuwapatia vifaa.
Alitaja silaha, magari na vyombo vyenye uwezo wa kufanya uchunguzi na kwamba ndicho alichotegemea kutoka kwenye mkutano huo na kwamba amepata ahadi za msaada.
AKIBA YA MENO
Rais Kikwete alisema Tanzania ina karibu tani 112 za pembe za ndovu ambazo haijajua itazifanya nini kwa sababu nchi ilizoea kuomba idhini ya kuziuza hatua ambayo inahitaji kuangaliwa upya.
UMASKINI
Akijibu swali kuhusu kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa kulinganisha na nchi nyingine katika kipindi cha miaka michache iliyopita lakini nchi ikiwa na maskini wanaoishi kwenye ufukara, alisema “uchumi unakua kwa asilimia 70 lakini umasikini unapungua kwa asilimia 2.0” akiongeza kuwa mchango huo wa ukuaji wa asilimia 7.0 umetokana na sekta ya mawasiliano na usafiri.
Sunday Feb 16, 2014

Kwa siku tatu mfululizo, yaani kuanzia Jumatatu hadi Jumatano (jana), gazeti hili lilichapisha taarifa ya uchunguzi kuhusu hali ya ujangili nchini, namna unavyofanyika na mianya inayochochea kushamiri kwake.
Wakati taarifa hiyo ikichapishwa, mambo kadhaa yalishajadiliwa kwenye jamii, huku shinikizo kubwa likielekezwa kwa serikali na mamlaka zake husika, kuwekeza zaidi katika mkakati utakaofanikisha ujangili dhidi ya rasilimali za taifa, hususani tembo, unakomeshwa.
Jamii haikulijadili tatizo hilo linalokua kwa kasi nchini kama sehemu ya malumbano ya kawaida, ama kuwa kielelezo cha chuki dhidi ya serikali iliyopo madarakani, la hasha.
Kuna kila viashiria vinavyoonyesha kuwa mijadala kuhusu kushamiri kwa ujangili nchini kulitokana na kiu ya umma, kutaka kushuhudia taifa likiudhibiti uovu huo, ili rasilimali zake zibaki kuwa endelevu, zikikinufaisha kizazi cha sasa na baadaye.
Ni kupitia mijadala inayohusu ujangili na namna ya kukabiliana nao, umma hautaki kuiona Tanzania ikipoteza rasilimali zake kama wanyamapori wakiwamo tembo walio katika hatari ya kutoweka, bali waendelee kuwapo.
Kuwapo kwa rasilimali hizo kutafuta uwezekano wa Watanzania kusafiri kwenda kuwaona nje ya nchi.
Hilo halitaepukwa ikiwa jitihada za kuudhibiti ujangili hazifanikiwa.
Ndiyo maana, kutokana na umuhimu huo, gazeti hili lilianzisha dawati maalum kwa ajili ya habari za uchunguzi.
Dawati hilo ndilo lililofanikisha kupatikana kwa taarifa na vielelezo mbalimbali vilivyofanikisha kuchapishwa kwa taarifa ya uchunguzi kuhusu hali ya ujangili na namna bora ya kuudhibiti, ili Tanzania iendelee kuwa mahali salama kwa wanyamapori.
Yapo mambo mengi yaliyoainishwa katika habari hiyo, lakini moja ya misingi yake mikubwa ni hitaji la kuifanya vita dhidi ya ujangili imilikiwe na umma wa Watanzania.
Kuimilikisha vita hiyo kwa umma kuna maana moja kubwa, kwamba hatua zozote zinazohusu ulinzi na usalama wa wanyamapori, zinapaswa kujulikana na kuushirikisha umma hasa jamii zinazoishi maeneo yaliyo karibu na hifadhi na mbuga za taifa, mapori ya akiba na mapori tengefu.
Hatua hiyo haipaswi kufanyika katika ‘taswira ya kisiasa’ lakini uhalisia wake ukabaki kuwa kinyume chake.
Umma unaposhiriki vita dhidi ya ujangili, kwa maana nyingine ni kuifanya kuwa rafiki wa rasilimali hizo na kwamba sheria, kanuni na taratibu zilizopo visiwe mfano wa nyenzo za kujenga uadui kati ya wenye dhamana ya ulinzi na usalama wa rasilimali hizo kwa upande mmoja na umma kwa upande mwingine.
Umma una nafasi kubwa kwa maana ndiyo unaochangamana na majingili wanapofika kwenye maeneo husika ili kutimiza nia ovu dhidi ya rasilimali zetu.
No comments:
Post a Comment