Wednesday, January 8, 2014

Tuhuma za Ujangili Watumishi 21 Maliasili wasimamishwa kazi,





Kwa ufupi
Uamuzi huo ulitangazwa jana na naibu waziri katika wizara hiyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Dar es Salaam. Wizara ya Maliasili na Utalii, imewasimamisha kazi watumishi wake 21 kwa tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia ujangili wa nyara za Serikali.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Polisi mkoani Singida, kumkamata ofisa wanyamapori katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili na nyara za Serikali, kinyume cha sheria.
Akitangaza hatua hiyo jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema Serikali inasikitishwa na vitendo viovu vinavyofanywa na watumishi wake na haitavivumilia. “Tumesikitishwa na kitendo cha ofisa wanyamapori wilayani Singida kukamatwa na bunduki mbili na ndege aina ya Heroe 12 nyumbani kwake, hatua tuliyochukua ni kumsimamisha kazi na kufikishwa mahakamani,” alisema na kuongeza:
“Wizara baada ya kufanya uchunguzi, imegundua kuwa kuna watumishi wanaoshirikiana na mtandao wa ujangili, hivyo imewasimamisha kazi watumishi 21 wa Idara ya Wanyamapori na tutachukua hatua zaidi.”
Alisema kati ya watumishi hao, 11 wanatoka katika Kikosi cha Kuzuia Ujangili mkoani Arusha, wanne wanatoka Mkoa wa Rukwa katika Pori la Akiba la Lwafu, mmoja Kikosi cha Bunda, watatu Pori la Akiba la Maswa, mmoja Selous, na mwingine mapori ya Lupika, Lumesule na Lusangu.
Akifafanua kuhusu uhaba wa watumishi katika Idara ya Wanyamapori, Nyalandu alisema kwa zaidi ya miaka 10 wizara hiyo haikuwa ikiajiri watumishi hali inayosababisha kukosa watumishi wenye ujuzi.
“Tunajipanga kuajiri watumishi wengine wenye ujuzi na kuangalia maendeleo ya teknolojia hasa kwa kujifunza kwa wenzetu Afrika Kusini,” alisema.
Kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili, alisema Serikali imeunda tume ya kimahakama itakayowahoji askari waliohusika na kurudisha taarifa. Hata hivyo alisema wako mbioni kuendelea nayo.
“Rais Jakaya Kikwete ameunda tume ya kimahakama na itatoa taarifa, ila sisi hatutalala, tutahakikisha kuwa tunapambana na ujangili ili kulinda nyara za Taifa,” alisema Nyalandu.
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wizara yake kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kuwakamata wahalifu.
“Jitihada hizi siyo zetu wenyewe, tunashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Tunawaomba wananchi washirikiane kulinda na kutoa taariza zitakazowezesha kukamatwa kwa wahalifu. Tunawaomba watumishi wetu wafanye kazi kwa moyo na uaminifu,” alisema Nyalandu.
Mamlaka ya wanyamapori
Akiwa katika pori la akiba la Selous hivi karibuni, Nyalandu alieleza mkakati wa Serikali wa kuanzisha mamlaka ya wanyamapori ili kuwapa mamlaka watendaji wa sekta hiyo katika kutunza maliasili.

Saturday, January 4, 2014

Mwaka 2013; uliacha ‘vilio’ kwa tembo


Baadhi ya matukio yaliyowahi kuripotiwa ni pamoja na baadhi ya watumiaji silaha katika sekta ya ulinzi na usalama nchini wakiwamo askari huzikodisha silaha zao kwa ajili ya kutumika katika matukio ya uhalifu.Aidha, kuwepo kwa mianya ya uingizaji wa silaha nchini kwa njia haramu kutokana na udhaifu uliopo katika mipaka mipaka ya DR Kongo, Burundi, Rwanda na hata Zambia jambo ambalo ni hatari.    


Posted  Januari4  2014  saa 11:7 AM
Kwa ufupi
  • Mauaji sasa yamefikia tembo 10,950 kwa mwaka 2013, ni dhahiri bila juhudi za kutokomeza ujangili... tutafika mwaka 2020 tukiwa hatuna akiba ya tembo.
Dar es Salaam. Kama Tembo wa Tanzania wangeulizwa kuna jambo gani kubwa hawatalisahau kwa mwaka 2013, bila shaka jibu lingekuwa: “Tuliwindwa, tukauawa sisi na watoto wetu na bado tuna hofu.”
Ingawa tembo ni mnyama mbabe awapo porini, lakini uwezo wake wa kujilinda yeye na jamii yake ulipunguzwa nguvu kwa kiwango kikubwa mwaka 2013, baada ya mauaji ya hazina hiyo ya taifa kuongezeka kwa kiasi kikubwa hata kuisukuma Serikali kuanzisha Operesheni Tokomeza Ujangili.
Utekelezaji wa operesheni hiyo ambao ulilenga kuzuia uwindaji haramu wa wanyama hao na wengine walio katika mbuga na hifadhi za taifa huku taarifa zikionyesha kuwa shehena kubwa ya pembe za ndovu ambayo imekuwa ikikamatwa ndani na nje ya nchi. Ripoti ya operesheni hiyo, ilileta athari kubwa kwa wananchi na mifugo hatua iliyomlazimu Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wanne waliokuwa wakiisimamia wizara zilizotajwa kuzembea katika kusimamia Opereesheni Tokomeza Ujangili.
Mawaziri hao ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.
Hata hivyo, akizungumza katika salamu zake za Mwaka Mpya, Rais Kikwete alisema: “Tunakamilisha matayarisho ya kuanza awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza. Ni muhimu kuendelea nayo kwani tusipofanya hivyo majangili wataendelea na vitendo vyao viovu.
Kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili nchini, Mkataba wa Biashara ya Kimataifa kwa Viumbe vilivyo Hatarini (CITES), uliitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi nane duniani zinazoongoza kwa kufanya biashara ya pembe za ndovu.
Matukio yaliyotikisa
Polisi mjini Zanzibar hawataisahau Novemba 15, 2013, siku waliyopigwa na butwaa baada ya kukamata shehena kubwa ya pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi, zikiwa na thamani ya Sh7.4 bilioni.
 Awali mzigo huo ulikuwa umehifadhiwa katika Mtaa wa Darajabovu, mkoa wa Mjini Magharibi, kabla ya kusafirishwa hadi Malindi.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kuwa baada ya kukamilika kwa kazi ya kupakua na kuhesabu pembe hizo, walibaini kuwa vilikuwa vipande 1,021 vikiwa na uzito wa kilo 2,915.
Tukio jingine la kufunga mwaka ni lile lililotokea jijini Dar es Salaam, ambalo lilisimamiwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Tarish Maimuna ambapo pembe za ndovu 706 zilikamatwa.
Katika tukio hilo, ambalo lilithibitisha kuuawa kwa tembo 353, raia watatu wa China wakazi wa Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, walikutwa wakiwa wamehifadhi shehena hiyo nyumbani kwao. Watuhumiwa hao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung.
1Baada ya polisi kuongeza nguvu ya kukamata pembe za ndovu, wasafirishaji waliibuka na mbinu mpya. Agosti 16, 2013 Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na pembe za ndovu yenye thamani ya Sh18.4 milioni zilizotengenezwa kama bangili tayari kusafirisha kwenda nje ya nchi.
Pia, haitasahaulika siku polisi jijini Dar es Salaam walipomkamata mkazi wa Mwananyamala, waliyemtilia shaka kisha kumpekuwa na kumkuta akiwa na vipande 16 vya pembe za ndovu  vyenye uzito wa kilo 24.5.
Akizungumzia tukio hilo, Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kuwa mtuhumiwa alinaswa na Polisi saa 9 alasiri maeneo ya Msimbazi Center, Wilayani Kinondoni.
Wafanyabiashara wengine walikamatwa nchi jirani wakijaribu kupeleka pembe hizo katika masoko barani Asia, hata hivyo walikamatwa kabla hawajatimiza malengo yao.
Januari mwaka huu, Gazeti La Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba Serikali ya Kenya imekamata shehena ya vipande 638 vya pembe za ndovu ambavyo ni sawa tembo 320 waliouawa.
Mzigo huo wa tani mbili ulikuwa kwenye kontena la mawe ya urembo (marumaru) kutoka Tanzania.
Huko Ruvuma, Polisi walifanikiwa kumtia mikononi dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, akisafirisha vipande 16 vya pembe za ndovu vyenye uzito wa kilo 18 ambavyo zilikuwa na thamani ya Sh48, 000 milioni.
Akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni ya mwaka 2013/14, Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa alisema pembe za ndovu zenye uzito wa tani 4 kutoka nchini Tanzania na Kenya zimeripotiwa kukamatwa na vyombo vya usalama vya mamlaka ya Jiji la Hong Kong, huku zile zilizoibwa kutoka Tanzania zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh2.5 bilioni.
“Pembe za ndovu zilizokamatwa Wilaya ya Biharamulo… zikiwa  kwenye gari iliyosemeka  ya Serikali maeneo ya Mto wa Mbu; watu watatu waliokamatwa Masasi wakisafirisha; haya ni matukio machache tu ambayo yaliweza kuripotiwa na Jeshi la Polisi yanayotoa taswira ya tatizo kubwa la ujangili hapa nchini,” alisema Msigwa.
Msigwa aliongeza kuwa iwapo Tanzania itaendelea na kasi iliyopo ya kuuwa tembo, miaka saba ijayo nchi hiyo itakuwa na historia ya kuwa na akiba ya wanyama hao.
“Ikiwa tafiti za mwenendo wa mauaji ya tembo zikionyesha kukua na kuashiria kwamba mauaji sasa yamefikia temboa 10,950 kwa mwaka huu wa 2013, ni dhahiri bila juhudi za kutokomeza ujangili tutafika mwaka 2020 tukiwa hatuna akiba ya tembo tena,” aliongeza.
Akizungumza na Redio Umoja wa Mataifa, Septemba 2013, Kagasheki alinukuliwa akisema kuwa ongezeko la bei ya pembe za ndovu, umasikini wa wananchi na tamaa ya baadhi ya watu zimechochea kwa kiasi kikubwa ongezeko la ujangili nchini.
Imeandaliwa na Goodluck Eliona


Friday, January 3, 2014

Shehena ya meno ya tembo yanaswa Dar



Shehena ya meno ya tembo 

Na Mwandishi wetu
3rd January 2014

Shehena ya meno ya tembo ambayo bado haijajulikana idadi wala uzito wake, imekamatwa na maofisa wa Maliasili kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ndani ya kontena.

Hata hivyo, waandishi wa habari ambao walifuatana na Kaimu Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Tabu Nziku, jana kwenye Bandari hiyo ili wakashuhudie kukamatwa kwa meno hayo walizuiliwa kwa muda wa saa mbili na walinzi wa Suma JKT kwa sababu ambazo hazijajulikana.

Licha ya kujitambulisha kuwa ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, maafisa hao waliwazuia kufanya kazi yao, jambo lililozusha mjadala na mabishano kwa muda mrefu pamoja na kuwepo kwa maofisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

Huku mabishano hayo yakiendelea walinzi hao walikuwa wanashinikiza waandishi wa habari watolewe nje, pamoja na kuwa wakati huo walikwishaingia ndani, na kugoma katakata kuwaonyesha kontena hilo.

Kaimu Mrugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande, alithibitisha kuwapo kwa kontena hilo lenye meno ya tembo, lakini alisema yeye hana uwezo wa kulizungumzia suala hilo bali wenye mamlaka hiyo ni Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara.

Aliongeza kuwa kwa sasa anafanya mawasiliano na ngazi hizo za juu na atakapokuwa tayari atamjulisha Afisa Habari ili awaite waandishi kwa ajili ya kulizumgumzia suala hilo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu, alisema amezipata taarifa hizo, lakini kwa muda huo alikuwa njiani akitokea Maswa na kwamba wizara inaandaa taarifa rasmi ili kulizungumzia jambo hilo ambayo itasambazwa kwenye vyombo vya habari.

Hata NIPASHE ilipomtafuta Kamanada wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, simu yake ya mkononi ilipokelewa na msaidizi wake ambaye alisema kuwa Kamishna Kova alikuwa katika kikao.

Matukio ya kuuawa kwa tembo yamekithiri nchini na hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa sensa ya ndovu katika Pori la Hifadhi ya Selous imekamilika, lakini taarifa yake inatisha kwani kuna ndovu 13,084 tu wakati mwaka 1976 walikuwepo tembo 109,419.

Aliongeza kuwa watu 1,030 walikamatwa pamoja na silaha za kijeshi 18, za kiraia 1579, na shehena kubwa za meno ya tembo na nyara nyingine navyo vilikamatwa, na watu kadhaa wameshafikishwa mahakamani na kwamba awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza Ujangili itaanza.

CHANZO: NIPASHE
Habari Zaidi
 

Askari wa wanyamapori auawa na wafugaji




Na Ashton Balaigwa
3rd January 2014
Askari wa wanyamapori wa hifadhi ya mbuga ya Jukumu iliyoko katika Wilaya ya Morogoro, ameuawa kikatili na wengine kujeruhia baada ya kuvamiwa na kundi la wafugaji jamii ya Kisukuma.

 Baadhi ya askari waliojeruhiwa, Yahaya Ramadhani na Khalphan Shabani, walisema tukio hilo lilitokea juzi wakati askari hao wakiwa katika doria nyakati za usiku katika mbuga hiyo.

 Kwa upande wake, Shabani alisema kuwa wakati wakiwa katika doria hiyo, ghafla  walivamiwa na kundi la wafugaji wa jamii ya Kisukuma na kuanza kushambuliwa kwa silaha za aina mbalimbali ikiwamo mikuki na marungu na kusababisha kifo cha askari mwenzao.

Alimtaja askari aliyefariki dunia baada ya kuchomwa mkuki kuwa ni Ramadhani Magengere, ambapo askari watatu walijeruhiwa.

Kwa mujibu wa Shabani, hilo ni tukio la tatu kutokea katika mbuga hiyo.
Hata hivyo, askari huyo wa wanyamapori, alilishutumu Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa kushindwa kutoa ushirikiano kuhusiana na mauaji hayo licha ya kutolewa taarifa.

 Ofisa Maliasili Mkoa wa Morogoro, Joseph Chuwa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Chuwa alisema hilo ni tukio la sita kwa askari wa wanyamapori kujeruhiwa hadi kusababisha kifo huku Jeshi la Polisi kutokutoa uzito wa matukio hayo licha ya kupewa taarifa.

 Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile, pia alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba uchunguzi unaendelea wa kuwatafuta wahusika.
Hata hivyo, Kamanda Shilogile aliwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kupatikana kwa wahusika hao.

Wakati huo huo, mtu mmoja amefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Taqwa kupinduka katika eneo la Mikumi barabara ya kuu ya Iringa - Morogoro.

Basi hilo lilikuwa likitoka Harare nchini Zimbabwe kwenda jijini Dar es Salaam.
Kamanda Shilogile alisema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya dereva wa basi kujaribu kulipita lori aina ya Scania lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Alimtaja aliyefariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Tabu Khemed.
Aidha, Kamanda Shilogile alisema majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya St. Kizzito ya mjini Mikumi.  

CHANZO: NIPASHE
 

Container full of elephant tusks seized in Dar


By David Kisanga

3rd January 2014

Lazaro Nyalandu, Natural Resources and Tourism Deputy Minister
Only two days after President Jakaya Kikwete announced the imminent relaunch of Operation Tokomeza, customs officials at the Dar es Salaam Port seized a container of ivory tusks reportedly being shipped to China. It was not immediately established how many tusks were in the container or their value.

Natural Resources and Tourism Deputy Minister Lazaro Nyalandu confirmed the seizure of the haul but could not give further details.

The deputy Minister said that the ministry was examining the haul after which it would issue a statement.

Reports obtained at the Port yesterday said that the container arrived at the port on Wednesday escorted by people believed to be police officers.

Sources who preferred not to be mentioned told The Guardian that the container was set to be shipped to China.

Efforts to get responses from the police were unsuccessful as our reporter was informed that they were in a meeting.

Tanzania Ports Authority (TPA) Acting Director General Madeni Kipande told reporters at the scene that the container was seized late on Wednesday evening.
He said the move followed tips from impeccable sources over illegal transportation of ivory tusks.

“We impounded the tusks in a container that was to be shipped. However I am not on a position to give details,” Kipande, said urging reporters to seek clarification from the Minister.

Last Week, the Deputy Minister Nyalandu told a press conference that at least 60 elephants had been killed in various national parks and game reserves within the country after the suspension of Operation Tokomeza, aimed at fighting poachers and those behind the ivory trade.

The operation was suspended and four cabinet ministers forced to resign after a parliamentary report exposed abuse of human rights and the country’s mother law by the implementers.

President Jakaya Kikwete in his last month’s address, announced that the operation would be re-launched to safeguard wildlife, still threatened by poachers.

In a related move in November last year, anti-smuggling unit, the police and Tanzania Intelligence Services impounded tusks weighing 2,915 kilogrammes with a street value of $4.7million (over 7.48bn/-) at Malindi Port in Zanzibar, packed in 50-kilogramme plastic bags.

In order to cover up the haul, the suspects packed sea shells in some plastic bags before placing them at the entry point of a container. 

SOURCE: THE GUARDIAN
More News 

Review policy to attract tourism investors to Dar, govt urged


Charles Lupilya, Dar es Salaam Tourist Board (DTB) Chief Executive Officer 

By James Kandoya

3rd January 2014
Charles Lupilya, Dar es Salaam Tourist Board (DTB) Chief Executive Officer
The government has been urged to review its tourism policy as a way of ensuring that investors in the sector don’t incur losses for providing services to tourists visiting Dar es Salaam City.

Dar es Salaam Tourist Board (DTB) Chief Executive Officer, Charles Lupilya told The Guardian in an exclusive interview yesterday that the review of the policy will help investors in the tourism sector especially the ones investing in Dar es Salaam know how they benefit from tourism business.

“Tourism policy is very important for those entitled to run tourism businesses. The challenge with Dar es Salaam city is that investors are not assured of making profit if they invest in such business,” Lupilya said.

He said experience shows that most tourists visiting the city have a variety of needs; therefore a well established policy will attract private investors to invest even more hence increase revenues.

Lupilya reasoned that failure to have a well established policy will lead to uneven development in the country as some areas will be underdeveloped like arts and crafts, spectacular waterfronts, islands, migratory butterfly, hocking and beaches.

According to Lupilya, tourism within Dar es Salaam city has been taking a snail’s pace due to the fact that the government has not established a policy which can assure investors of profit.

He however said tourist attractions currently available in the city are not enough to attract more tourists and make the business viable.  

SOURCE: THE GUARDIAN 

Mchungaji Msigwa ambeza JK kuhusu ujangili


Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini akieleza athari ya ujangili kwa wahariri na wadau wa habari,kwenye ukumbi wa Siasa ni kilimo mjini Iringa-picha na Journo Tourism.
 ‘Wapo viongozi tulidhani ndiyo wameguswa na operesheni hiyo, lakini kwa bahati mbaya na kwa sababu majangili ni mtandao mkubwa unaotoka ndani ya Serikali na CCM, walibadilisha mwelekeo masukudi.’ Peter Msigwa 
Na Geofrey Nyang’oro, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Januari2  2014  saa 10:33 AM
Kwa ufupi
  • Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa juzi,  Mchungaji Msigwa alisema kasi ya ujangili ni kubwa na baadhi ya wahusika  ni vigogo ndani ya CCM.

Iringa. Mbunge wa Iringa Mjini,  Mchungaji Peter Msigwa (Chadema)  amesema kama Rais Jakaya Kikwete anadhamira ya kweli kutokomeza ujangili nchini ni vyema akasafisha kwanza Serikali na chama chake.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa juzi,  Mchungaji Msigwa alisema kasi ya ujangili ni kubwa na baadhi ya wahusika  ni vigogo ndani ya CCM.
Alisema wengine wanatoka serikalini hususan jeshini; Idara ya Usalama wa  Taifa na Polisi jambo linalosababisha operesheni hiyo kuwa ngumu kwa utekelezaji.
Alisema hali hiyo ndiyo chanzo hata cha Operesheni Tokomeza Ujangili iliyositishwa kwa muda kupoteza mwelekeo.
“Tulipoanza kupiga kelele juu ya vitendo vya ujangili tuliambiwa tunataka umaarufu kisiasa, lakini hali ilipofikia wao wenyewe wamekubali na kuanzisha hata Operesheni Tukomeza Ujangili, lakini niliwaambia mtandao wa ujangili ni mkubwa,” alisema Mchungaji Msigwa na kuongeza:
“Unahusisha vigogo ndani ya CCM, si mnakumbuka niliwahi kuwatajia majina na kuwaambia wawekwe mbali na Tembo... baadhi yao ni polisi wengine ni wanajeshi, kama kweli Rais Kikwete ana nia ya dhati kupambana na ujangili ni vyema akasafisha nyumba yake kwanza.”
Mchungaji Msigwa alisema Serikali ilianzisha Operesheni Tokomeza Ujangili kwa nia njema, lakini kwa sababu majangili wanatoka ndani ya Serikali  hivyo imekuwa vigumu kufanikisha kazi hiyo. Alisema ndiyo sababu hata malengo yake yalipotoshwa, huku walengwa wakiachwa na kuanza kuua raia wasio na hatia.
 Mbunge huyo alisema hivi sasa kasi ya ujangili  inatisha na kuongeza  kuwa, kwa siku zaidi ya Tembo 60 wamekuwa wakiuawa jambo linalowafanya wanyama hao muhimu kuwa hatarini  kutoweka.
Alisema hatua ya mawaziri wanne kujiuzulu inaonyesha dhahiri wabunge wa upinzani na Bunge kwa jumla limetekeleza wajibu wake na kwamba, hiyo inatosha kujiaminisha kwa wapigakura wao.
Hata hivyo, Msigwa alisema msimamo wake ni kwamba Serikali ina viongozi mzigo, huku akimtaja Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa ni kiongozi mzigo