Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini akieleza athari ya ujangili kwa wahariri na wadau wa habari,kwenye ukumbi wa Siasa ni kilimo mjini Iringa-picha na Journo Tourism.
‘Wapo
viongozi tulidhani ndiyo wameguswa na operesheni hiyo, lakini kwa bahati mbaya
na kwa sababu majangili ni mtandao mkubwa unaotoka ndani ya Serikali na CCM,
walibadilisha mwelekeo masukudi.’ Peter Msigwa
Na Geofrey Nyang’oro, Mwananchi
Posted Alhamisi,Januari2 2014 saa 10:33 AM
Posted Alhamisi,Januari2 2014 saa 10:33 AM
Kwa ufupi
- Akihutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa
juzi, Mchungaji Msigwa alisema kasi ya ujangili ni kubwa na baadhi
ya wahusika ni vigogo ndani ya CCM.
Iringa. Mbunge wa Iringa
Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amesema kama Rais Jakaya
Kikwete anadhamira ya kweli kutokomeza ujangili nchini ni vyema akasafisha
kwanza Serikali na chama chake.
Akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika Viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa juzi, Mchungaji Msigwa
alisema kasi ya ujangili ni kubwa na baadhi ya wahusika ni vigogo ndani
ya CCM.
Alisema wengine wanatoka serikalini
hususan jeshini; Idara ya Usalama wa Taifa na Polisi jambo
linalosababisha operesheni hiyo kuwa ngumu kwa utekelezaji.
Alisema hali hiyo ndiyo chanzo hata
cha Operesheni Tokomeza Ujangili iliyositishwa kwa muda kupoteza mwelekeo.
“Tulipoanza kupiga kelele juu ya
vitendo vya ujangili tuliambiwa tunataka umaarufu kisiasa, lakini hali
ilipofikia wao wenyewe wamekubali na kuanzisha hata Operesheni Tukomeza
Ujangili, lakini niliwaambia mtandao wa ujangili ni mkubwa,” alisema Mchungaji
Msigwa na kuongeza:
“Unahusisha vigogo ndani ya CCM, si
mnakumbuka niliwahi kuwatajia majina na kuwaambia wawekwe mbali na Tembo...
baadhi yao ni polisi wengine ni wanajeshi, kama kweli Rais Kikwete ana nia ya
dhati kupambana na ujangili ni vyema akasafisha nyumba yake kwanza.”
Mchungaji Msigwa alisema Serikali
ilianzisha Operesheni Tokomeza Ujangili kwa nia njema, lakini kwa sababu
majangili wanatoka ndani ya Serikali hivyo imekuwa vigumu kufanikisha
kazi hiyo. Alisema ndiyo sababu hata malengo yake yalipotoshwa, huku walengwa
wakiachwa na kuanza kuua raia wasio na hatia.
Mbunge huyo alisema hivi sasa
kasi ya ujangili inatisha na kuongeza kuwa, kwa siku zaidi ya Tembo
60 wamekuwa wakiuawa jambo linalowafanya wanyama hao muhimu kuwa hatarini
kutoweka.
Alisema hatua ya mawaziri wanne
kujiuzulu inaonyesha dhahiri wabunge wa upinzani na Bunge kwa jumla
limetekeleza wajibu wake na kwamba, hiyo inatosha kujiaminisha kwa wapigakura
wao.
Hata hivyo, Msigwa alisema
msimamo wake ni kwamba Serikali ina viongozi mzigo, huku akimtaja Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kuwa ni kiongozi mzigo
No comments:
Post a Comment