Kwa ufupi
Katika mwaka huohuo, taasisi ya
Frankfurt Zoological Society iliandika kwenye ripoti yake kuwa uwindaji wa
kiuhalifu umekuwa ukiua tembo wapatao 30 kila siku ili kupata meno kwa ajili ya
biashara haramu.
Mwaka 2013, uwindaji halali
uliingizia Tanzania wastani wa Sh900 bilioni, ikiwa ni zaidi ya asilimia 90 ya
mapato ya sekta ya utalii yaliyotokana na wanyamapori.
Katika mwaka huohuo, taasisi ya
Frankfurt Zoological Society iliandika kwenye ripoti yake kuwa uwindaji wa
kiuhalifu umekuwa ukiua tembo wapatao 30 kila siku ili kupata meno kwa ajili ya
biashara haramu.
Operesheni kadhaa zimekuwa
zikiendeshwa kwa lengo la kukomesha uwindaji huo haramu pamoja na kuwakamata na
kuwachukulia hatua kali wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo.
Serikali imeendesha pia operesheni
kadhaa za kukabiliana na majangili hao ambao hawana huruma na rasilimali hizo
muhimu kwa ustawi wa uchumi wa taifa na badala yake wanaamua kujitajirisha kwa
manufaa ya kikundi hicho cha wachache.
Dunia inalinda ujangili?
Katika harakati za kuchukua
tahadhari zaidi, Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na
Hifadhi ya Wanyamapori Duniani (WildAid), liliandaa mkutano nchini kati ya
viongozi wa dini na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuongeza kasi ya vita
hiyo.
Katika mkutano huo, viongozi wa dini
na madhehebu mbalimbali walichangia mapendekezo yao huku wakikabidhiwa majukumu
ya kushirikiana na Serikali ili kufanikisha vita hiyo.
Katika mjadala huo, Mtume na Nabii
wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira alisema kabla ya kujadili ajenda hiyo
inatakiwa kuzingatia mawazo ya pande kuu mbili.
“Kwanza lazima tujue mijadala kama
hii tunahitaji kujadili kwa mrengo wa wageni au kama Watanzania? Lazima tufanye
hivyo kutokana na uzito wa jambo lenyewe,” alisema Mwingira.
Wakati vita hiyo ikiendelea ndani ya
nchi, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk
Valentino Mokiwa alisema vita hiyo inaibua maswali mengi kutokana na uhuru,
uwazi wa masoko ya nje ya nchi yanayotokana na malighafi ya meno ya tembo.
Alisema pamoja na mtandao wa
biashara hiyo ndani ya nchi masoko ya bidhaa yameendelea kulindwa katika
mataifa makubwa duniani na hakuna juhudi za vyombo vya ulinzi kushughulikia.
“Wahalifu ambao ni dagaa pekee ndiyo
wanakamatwa na kupewa adhabu, kwa mazingira hayo vita ya ujangili nchini
haitaweza kumalizika mpaka tuamue kukemea bila kuogopa,” alisema na kuongeza;
Lakini mambo ya kujiuliza ni nani anayefadhili mtandao wa biashara hiyo?
Inawezekanaje ujangili ukafanyika porini, meno yakasafirishwa kwa njia ya
barabara mpaka bandarini au uwanja wa ndege na kusafirishwa nje halafu unakuta
nje kuna masoko ya bidhaa ya meno ya tembo!”Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikiri changamoto hiyo huku akibainisha kuwa kweli masoko hayo yapo na ndiyo maana watu wanahamasika kuifanya.
Hata hivyo, alisema Serikali imeanza kushawishi mataifa makubwa yaweke maazimio ya kudhibiti uzalishaji wa bidhaa zinazochangia kukua kwa ujangili.
“Masoko ya bidhaa yanaonekana kuenea zaidi China, Korea, Thailand na maeneo kadhaa ya Asia. Lakini tulizungumza na Serikali zao, wakasema wamejaribu kila namna kuzuia wananchi wao lakini inaonekana kushindikana,” alisema Nyalandu na kuongeza:
“Pamoja na hatua hiyo lakini niliandaa mkutano Arusha na kuwashirikisha Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia na mataifa mengine tisa kujadili juu ya kuzuia masoko hayo na juhudi bado zinaendelea.”
Vita ya ujangili
Viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na msaidizi wa Askofu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), George Fupe, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salum, Askofu Mkuu wa Taasisi ya Wapo Mission International, Sylvester Gamanywa na masheikh wa misikiti mbalimbali ya Ilala, Temeke, Kinondoni.
Katika harakati za kutafuta ufumbuzi wa ujangili nchini, Waziri Nyalandu alisema pamoja na juhudi zinazoendelea, viongozi wa dini ni kundi lenye nguvu zaidi ya ushawishi kwenye jamii na kwa waumini wao.
Waziri Nyalandu alitoa mtamzamo wa njia mbili za ushiriki wa viongozi hao kufungua ukurasa upya juu ya sakata la ujangili nchini.
“Kwanza ninawaomba mkakati ya kufunga maagano na waumini wa dini iandaliwe, ili kubadili mitazamo ya vijana wanaotegemea biashara hizo kama sehemu ya kujikwamua kiuchumi nchini na waelezwe, kwa imani na hofu ya Mungu nadhani wataweza kubadilika,” alisema waziri huyo na kuongeza:
“Viongozi wa dini wanayo nafasi muhimu sana kuziba nafasi ya katikati kwenye vita hii.”
Sheikh Salum alisema viongozi wa dini wana uwezo wa kushawishi na kwamba jukumu lao ni kuhakikisha wanashiriki katika ulinzi wa wanyamapori hao.
Alisema licha ya kukiuka sheria, hata Kitabu kitakatifu kinakataza kufanya ukatili wa aina yoyote kwa wanyama.
“Tumepewa mamlaka ya kuwatawala wanyama, ujangili kwa wanyama ni dhambi inayotakiwa kukemewa na jamii yote kwa ujumla. Jukumu letu ni kuwalinda kwa faida ya kizazi cha baadaye,” alisema Sheikh Salum.
Mtandao wa biashara bado unaendelea kuitafuna Afrika na Tanzania kuonekana kinara wa ujangili, lakini kuna kila sababu ya kuhakikisha kwanza kunakuwapo na udhibiti wa mtandao wa ndani bila kuogopa jambo lolote.
Alisema jambo jingine ni kuomba ushirikiano na mataifa ya nje kupambana na soko la meno na bidhaa zake hasa katika Bara la Asia.
“Ikiwezekana, Serikali iombe masharti makali yatolewe kwa mataifa yanayoendesha biashara hiyo kwa utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na meno hayo.”
Hii inaashiria kwamba zikiwapo sheria za kimataifa katika kuzuia biashara na bidhaa za meno ya tembo, vita dhidi ya ujangili itakwisha maana itawavurugia soko wanaojihusisha na biashara hiyo.
No comments:
Post a Comment