HIFADHI
ZA TAIFA TANZANIA
TAARIFA
KWA UMMA
Katika Gazeti la
Mawio Toleo Namba 0062 la tarehe 26.9.2013 – 02.10.2013 na toleo Namba 0063 la
tarehe 03.10.2013 zimechapishwa habari zenye vichwa vya habari “Mtandao
wa Ujangili Huu Hapa” na “Wabunge CCM watajwa ujangili”.
Katika habari zote
hizo zimelihusisa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama chanzo cha habari
hizo.
Shirika
la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusiana na taarifa
hizi:
(i)
Shirika la Hifadhi za Taifa halijawahi kudhamini
ripoti iliyotajwa katika habari hizo kuhusiana na utafiti makini wa ujangili.
(ii)
Shirika
husimamia shughuli za uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi
za Taifa pekee kiutendaji, ambapo
baadhi ya maeneo yaliyotajwa
Katika habari hizo kama Selous na
Liwale kiutendaji hayapo ndani
ya Shirika la Hifadhi za Taifa.
(iii)
Kama Shirika la Umma, hufuata taratibu za
kisheria ikiwa ni pamoja na kushirikisha vyombo mbalimbali vya dola katika
kushughulikia uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo ujangili.
Ni
kwa mantiki hii basi, shirika linapenda kuweka bayana kuwa halihusiki na
taarifa hizo, na hata pale zinapopokelewa zina utaratibu wake wa kufanyia kazi.
Tunachukua nafasi
hii kuviomba vyombo vya habari kushiriki katika juhudi za kupambana na ujangili
kwa kuwa waangalifu katika kuandika habari za kutuhumiana kabla ya kuwa na
ushahidi kamili ambao ni haki ya kimsingi ya kisheria inayopaswa kuheshimiwa.
Imetolewa na Idara
ya Uhusiano
HIFADHI
ZA TAIFA TANZANIA
07/10/2013
No comments:
Post a Comment