Ngorongoro washauriwa
kutunza mazingira
Na Mussa Juma
Posted Oktoba5 2013
Posted Oktoba5 2013
Kwa ufupi
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi msitu wa Enguserosambu ili utunzwe na jamii, badala
ya kuwa chini ya Serikali Kuu leo, mkuu huyo wa wilaya alisema ili
mazingira yaendelee kutunzwa katika wilaya hiyo ni vyema upanuzi wa mashamba
ukasitishwa.
Loliondo.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha, Elias Wawa Lali, amewataka wakazi
wa wilaya hiyo, kusitisha upanuzi wa mashamba ili kuzuia uharibifu wa mazingira
na vyanzo vya maji.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi msitu wa Enguserosambu ili utunzwe na jamii, badala
ya kuwa chini ya Serikali Kuu leo, mkuu huyo wa wilaya alisema ili
mazingira yaendelee kutunzwa katika wilaya hiyo ni vyema upanuzi wa mashamba
ukasitishwa.
"Wakazi
wa Ngorongoro wengi ni wafugaji hivyo, ni vyema kuendelea kuboresha
mifugo na kuivuna badala ya kuanzisha mashamba makubwa," alisema Lali.
Aliwataka
wakazi wa Kata ya Enguserosambu kupitia bodi mpya ya kusimamia msitu huo,
kuendelea kuutunza sambamba na vyanzo vya maji ili uweze kudumu.
Msitu wa
Enguserosambu wenye ukubwa wa zaidi ya hekta 71, kuanzia sasa utakuwa
unasimamiwa na jamii kwa uratibu wa shirika lisilo la kiserikali la PALISEP
ambalo limeahidi kushirikiana na jamii kulinda na kutunza msitu huo.
Awali
Ofisa Nyuki Mkuu wa Serikali, Paulin Mafuru aliyezungumza katika hafla hiyo kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarish
alipongeza wakazi wa kata hiyo kwa kutunza msitu huo wa asili.
No comments:
Post a Comment