POLISI mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na askari wa Tanapa wamefanikiwa kumnasa Donald Baya Burugu mkazi wa kijiji cha Busalu Kata ya Kisesa wilaya ya Meatu akiuza jiwe lililochongwa vizuri kuwa ni pembe ya faru kwa sh.mil.10.
Tukio hilo limetokea septemba 24 majira ya mchana Mwaka huu ,baada ya kuweka mtego na kumnasa kirahisi mtuhumiwa huyo ambaye habari zinasema kuwa alikuwa na wenzake ambao hawakukamatwa.
Afisa wanyamapori mkoa wa Shinyanga alithibitisha kuwa haikuwa pembe ya faru bali jiwe lililotengenezwa kiufundi,.
Zoezi hilo lilisimamiwa na Rco Shinyanga ,hata hivyo blog hii ilibaini kuwa mtuhumiwa alikaa kituo cha polisi kwa zaidi ya siku 5 bila kufikishwa mahakamani ,hatua ambayo ilitafsriwa na wachambuzi wa mambo kuwa kulikuwa na mchakato kwa ndugu wa mtuhumiwa kutafuta fedha ili aachiwe..
No comments:
Post a Comment