MBUNGE
wa Iringa Mjini na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Peter
Msigwa (CHADEMA), amemtaka Rais Jakaya Kikwete awataje wahusika wa vitendo
vya ujangili.
Msigwa
alisema Tanzania ni moja ya nchi nane duniani ambazo ziko katika kiwango
cha juu sana katika biashara haramu ya ujangili na kati ya kilo 800
zinazokamatwa duniani, asilimia 37 ya meno ya tembo yanatoka Tanzania.
Msingwa
alitoa kauli hiyo hivi karibuni mjini hapa wakati wa maandamano ya Siku ya
Ujangili yaliyodhaminiwa na Shirika la Wildlife Connection na kufanyika
katika viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa.
Alisema
Rais Kikwete anawajua baadhi ya vinara wa ujangili, hivyo alimtaka awataje
na kuwachukulia hatua ili kukomesha vitendo hivyo.
“Namshinikiza
rais awataje majangili wote lakini nashangaa hakuna kauli hata moja ya
kuwataja na majangili hao wanaendelea kuwateketeza tembo kila mwaka,”
alisema Msigwa.
Alisema
suala la biashara haramu ya wanyamapori nchini limeendelea kukua kwa kasi
ya ajabu huku serikali ikionesha wazi kushindwa kudhibiti suala hili, hivyo
kutoa mwanya kwa majangili kuendelea kuteketeza wanyamapori.
Aidha,
Msigwa alisema jambo moja la msingi, wananchi wote tuungane katika
kupambana na majangili walioko katika maeneo yetu na kuwafichua bila
kuogopa kwa lengo la kuwanusuru tembo ambao wanateketea kila siku duniani,
hasa katika mbuga za taifa hili.
|
No comments:
Post a Comment