Polisi wadaiwa kumpiga
risasi kiziwi
Oktoba11 2013
Kwa ufupi
Naye
mganga aliyemfanyia vipimo, Tanu Warioba alisema taarifa kamili ya ukubwa wa
majeraha itatolewa baadaye.
Serengeti.
Mtu mmoja ambaye ni bubu na kiziwi, mkazi wa Kijiji cha Bisarara Kata ya Sedeco
wilayani Serengeti, amelazwa katika Hospitali Teule ya Nyerere akidaiwa kupigwa
risasi na askari waliokuwa wakiendesha operesheni ya kusaka nyara na silaha.
Habari
ambazo zimethibitishwa na polisi Mkoa wa Mara,uongozi wa kata na Hospitali
Teule ya Nyerere zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 9,mwaka huu kati ya
saa 8.30 hadi 11 alfajiri kijijini hapo.
Mganga wa
zamu katika hospitali hiyo, Nyanzirali Kitara amethibitisha kumpokea majeruhi
huyo Mnanka Machumbe Nyangige(18)ambaye amelazwa katika kitanda namba 5 wodi ya
wanaume .
Naye
mganga aliyemfanyia vipimo, Tanu Warioba alisema taarifa kamili ya ukubwa wa
majeraha itatolewa baadaye.
Jitihada
za kuwasiliana na majeruhi huyo hazikufanikiwa kutokana na ulinzi wa askari
polisi. Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa watu wanaomwuguza majeruhi huyo,
mkazi wa kijijini hapo, Joseph Ryoba Maseke(18), alisema kundi kubwa la askari
walivamia kijijini hapo wakisaka silaha na majangili wa tembo.
“Walivamia
mji huo na kubomoa milango, wakaingia ndani wakawa wanaamuru watu
wajisalimishe...lakini huyu majeruhi ni bubu na kiziwi akawa hasikii
…walichofanya ni kumfyatulia risasi na kumjeruhi ndipo akurupuka na kuanguka
nje,” alisema.
Alisema
baada ya kumjeruhi waliendelea kupiga watu ovyo wakiwamo wanawake, wakidai wanataka
bunduki, kumchukua mwenye mji huo Machumbe Nyangige na vijana wake wawili
Nyangige na Mwita kwenda nao polisi.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Mara Fernandi Mtui akizungumza kwa simu alikiri kutokea tukio
hilo: “Nimeambiwa na nimewaagiza kufuatilia kujua aliyepigwa risasi ni nani…
kapigwa na nani… ilikuwaje… mazingira hayo kisha wanijulishe ana mimi
nitawajulisha,” alisema.
No comments:
Post a Comment