WAHUKUMIWA
MIAKA 21 JELA KWA MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI
Oktoba 13,2013
Tarime:WATU wawili wamehukumiwa kwenda jela miaka 21 na mahakama ya
hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Tarime baada ya kupatikana na makosa ya uhujumu
Uchumi.
Waliohukumiwa kutumimikia adhabu
hiyo ni Paulo Pancho Wairanga(31)mkazi wa Gibaso wilayani Tarime aliyekuwa
anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 13/2013 na Marwa Mwita Mange(43)
mkazi wa Masanga wilayani humo,ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu
uchumi namba 36/2013.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa
Mahakama hiyo Adriano Kirimi alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo haukuacha shaka yoyote dhidi ya washitakiwa kutokana na makosa
yaliyokuwa yanawakabili.
Katika hukumu hizo Marwa Mwita
Mange amehukumiwa kwenda jela miaka 20
bila faini baada ya kukiri makosa yote matatu yaliyokuwa yanamkabili,ikiwemo
kosa la kuingia ndani ya hifadhi bila
kibali ambalo alihukumiwa faini ya sh,5,000 au kifungo cha miezi sita,na kosa
la kukutwa na silaha hifadhini alihukumiwa kwenda jela miezi 12 bila faini.
Katika kosa la tatu la kumiliki
nyara za serikali ambapo mshitakiwa alikutwa na mzoga wa nyumbu ikiwa na thamani ya
sh.mil.1.2 kinyume na namba 86(1)(c) ya
sheria ya wanyamapori sura ya 5 ya 2009 inayosomeka na aya ya 14(b) ya jedwali
la kwanza sura ya 57(1)60(2) ya sheria ya uhujumu uchumi sura namba 200 ya
mwaka 2002 mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 20,na adhabu inakwenda
pamoja hivyo atatumikia miaka 20 jela.
Kwa upande wa hukumu ya Wairanga
alihukumiwa kwenda jela mwaka 1 baada ya kupatikana na hatia kwa makosa mawili
ya kuingia hifadhini bila kibali na kumiliki silaha ndani ya hifadhi bila
kibali.
Mapema mwendesha mashitaka wa
Tanapa Shukrani Fadhili Msuya akisoma maelezo aliiambia Mahakama kuwa Paulo
Pancho Wairanga alikamatwa machi 22,mwaka huu katika eneo la Gong’ora ndani ya
hifadhi ya Taifa ya Serengeti akikabiliwa na makosa mawili.
Mwendesha mashitaka huyo alisema
katika kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2013 ilikuwa inawakabili washitakiwa
wawili ambapo Marw Mwita Mange akikiri kosa na kuhukumiwa ,mshitakiwa namba
moja katika kesi hiyo Chacha Nyagana Sira(47)alikana shitaka na yuko nje kwa
dhamana hadi novemba 12,2013 kesi hiyo itakaposikilizwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment