Thursday, August 6, 2015

Ofisa Mhifadhi Wanyamapori atupwa jela miaka mitatu.



Ofisa Mhifadhi Wanyamapori atupwa jela miaka mitatu.


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, imemhukumu Ofisa Mhifadhi Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Richard Nchasi, kulipa faini ya Sh. 900,000 au kwenda jela miaka mitatu baada ya kukutwa na makosa matatu.
 
Hukumu hiyo ilisomwa na Hakimu Mkazi, Juma Hassan, juzi  baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri  na kumtia mshtakiwa hatiani kwa makosa hayo matatu.
 
"Kati ya makosa manne, mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kwa makosa matatu ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kwa kutoa hati za uwindaji wa wanyama," alisema Hakimu Hassan.
 
Hata hivyo, mahakama hiyo ilisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha shitaka la kuisababishia wizara hiyo hasara ya Dola 1,860 za Marekani (sawa na Sh. 2,976,000).
 
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Januari na Septemba, 2008, katika ofisi za wizara hiyo, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na wadhifa huo, aliandaa hati yenye namba 01235414 ya Agosti Mosi, 2008.
 
Inadaiwa kuwa hati hiyo ilikuwa ikionyesha kwamba Safari Club (T) Ltd, inatakiwa kulipa Dola 5,080 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh. milioni 8.5) ikiwa ni ada ya uwindaji wa wanyama sita katika eneo la Kilwa South Mbemkulu, huku akijua si kweli.
 
Nchasi anadaiwa kuwa katika kipindi hicho, aliandaa tena hati yenye namba 01235410 ya Februari 21 mwaka 2008, kuonyesha kwamba kampuni hiyo inatakiwa kulipa ada ya Dola 6,580 (sawa na zaidi ya Sh. milioni 11) ya uwindaji wa wanyama watano katika eneo hilo.
 
Ofisa Mhifadhi huyo anadaiwa katika kipindi hicho, aliandaa tena hati yenye namba 01235415 ya Agosti Mosi, 2008, kuonyesha kampuni hiyo inatakiwa kulipa Dola 6,335 (sawa na zaidi ya Sh. milioni 10.6) ikiwa ni ada ya uwindaji ya wanyama saba kwenye eneo hilo.
 
Katika shitaka la nne, Nchasi anadaiwa katika kipindi hicho, jijini Dar es Salaam, akiwa mwajiriwa wa wizara hiyo, kwa kuelewa na kwa uzembe, aliisababishia wizara hiyo hasara ya Dola 1,860 (sawa na zaidi ya Sh. milioni 2.9) .
 
Hadi NIPASHE inaondoka mahakamani hapo jana 7:30 mchana mshtakiwa alikuwa hajalipa faini hiyo. 
CHANZO: NIPASHE

BREAKIN NEWZZ!!:- KUKAMATWA KWA MENO YA TEMBO USWISS WAZIRI NYALANDU AFUNGUKA LIKE NEVER BEFORE SOMA HAPA LIVE!!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirYSCVlbkt-CenVRznMnNyyX0KxjRAHUHfLR-v3dbiawwXZz_OCl0H_N0hV0ZPEs0Ybp3UvD37Xezrchc3ZjGs5feo7ADPOot4B5UrqqpNqvtA3wuxhK3JqlAtNjE3hMwVVlfLmzvIvHPJ/s1600/2B16A65B00000578-3185470-image-a-7_1438728714802.jpg

Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea taarifa kupitia Vyombo vya Habari inayohusu kukamatwa kwa nyara zinazojumuisha meno ya tembo yenye uzito wa kilo 262, kucha na meno ya simba vyenye uzito wa kilo moja(1). Tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea kwenye uwanja wa ndege wa Zurich nchini Uswisi tarehe 06 Julai, 2015. Kwa mujibu wa taarifa hizo, nyara hizo zilipatikana ndani ya masanduku manane (8) zikiwa njiani kwenda Beijing-China kutokea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kupitia Zurich.
Wizara inachukua nafasi hii kupongeza Uongozi wa uwanja wa ndege wa Zurich, na Serikali ya Uswisi na wote walioshiriki kubaini na kukamata nyara hizo. Wizara imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizi na kwamba nyara hizo zimesafirishwa kupitia uwanja wa ndege wa JN Dar es Salaam. Tukio hili linadhihirisha kuwa tatizo la ujangili bado linaendelea ndani na nje ya nchi yetu licha ya jitihada nyingi zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Jumuiya za Kimataifa.
Wizara inapenda kuuhakikishia umma kuwa sisi kama nchi tunafanya na kutumia jitihada zote kupambana na vitendo vya ujangili unaotishia kutoweka kwa rasilimali za wanyamapori wetu.
Baada ya kupokea taarifa hizo, Wizara imeanza kufanya uchunguzi kwa kushirikisha mamlaka husika ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja kuwabaini wote waliohusika na kadhia hii. Wizara inapenda kutoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kufanya uchunguzi huu aziwasilishe kwenye mamlaka za Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na

Lazaro S. Nyalandu
Waziri wa Maliasili na Utalii.

Wednesday, July 1, 2015

UTALII WA NDANI HIFADHI YA TAIFA KISIWA CHA SAANANE























USIKU WA TUZO ZA UANDISHI WA HABARI ZA UTALII NA UHIFADHI

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiendelea na burudani mbalimbali kabla ya zoezi la utoaji wa tuzo halijaanza ,ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza.
Waandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi waliopata tuzo wakiwa na wahariri wao,kutoka kushoto ni Tom Mosoba mhariri wa gazeti la The Citizen,Mussa Juma kutoka Arusha aliyeshika nafasi ya pili tuzo ya uhifadhi,Phinias Bashaya toka Kagera aliyeshika nafasi ya pili tuzo ya utalii wa ndani,Reginald Miruko Mhariri wa habari Mwananchi,Anthony Mayunga toka Mara ,aliyeshika nafasi ya kwanza tuzo ya uhifadhi,Bernald mhariri gazeti la The Citizen na Daniel Mjema toka Kilimanjaro aliyeshika nafasi ya tatu tuzo ya uhifadhi,gazeti la Mwananchi ndilo lililoongoza kwa kuzoa tuzo nyingi.
Burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii zilikuwepo
Mkurugenzi  Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi akisalimiana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi Mrisho Salakikya ambaye alipewa tuzo maalum kutokana na kufanya utalii wa kupanda mlima Kilimanjaro kwa mara nyingi zaidi
Baadhi ya maafisa wa Tanapa na familia zao wakifuatilia mambo yanavyoendelea.
Maandalizi ya Tuzo yanaendelea kama inavyoonekana hapo.
Danie Mjema  toka Mwananchi Kilimanjaro akipokea hundi ya sh  1 milioni ,cheti baada ya kuibuka mshindi wa tatu tuzo ya uhifadhi
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akimpongeza
Waziri wa Maliasili na Utalii Nyalandu akimkabidhi hundi ya 1.5 milioni Mussa Juma toka Mwananchi Arusha aliyeshika nafasi ya pili tuzo ya uhifadhi.
Hongera sana Mussa
Pokea hundi na cheti chako ,kwa kazi yako iliyotukuka ,anasisitiza Waziri
Waziri wa Maliasili na Utalii Nyalandu akimpongeza Anthony Mayunga Mwandishi wa habari kampuni ya Mwananchi Mkoa wa Mara baada ya kushika nafasi ya kwanza katika tuzo ya uhifadhi,kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi,katikati ni Katibu Mkuu wizara ya Malisili na Utalii na Mkurugenzi Bodi ya Utalii.
Hongera sana na pokea hundi ya 2 milioni,cheti,ngao na safari ya mafunzo katika moja ya nchi za Sadc,ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi wakati wa kukabidhi tuzo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Nyalandu akisaidiana na Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa kukabidhi hundi,ngao na cheti.
Tunataumbua mchango wako kwenye uhifadhi wanasisitiza
Kwa kweli nimekukubali anasisitiza waziri.
Jimmy Mengere wa Channel Ten akipokea tuzo yake.
Hongera sana
Maarufu kama Mayunga wa Redio Saut akipokea tuzo
Hongera sana
Kasilida Mlimila wa Staa Tv akipokea zawadi
Kagunamo toka Itv Mbeya akipokea zawadi
Magessa Magessa akipokea zawadi baada ya kuibuka mshindi wa tatu kwa kazi aliyotuma akiwa star tv kwa sasa yuko Acacia Gold Mine
Hongera sana Magessa
hongera Kasilda kwa kushinda tuzo mbili
Phinias Bashaya mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Kagera akipokea zawadi baada ya kushika nafasi ya pili tuzo ya utalii wa ndani