Sunday, April 19, 2015

MATUKIO YA KUACHIWA KWA MBWA MWITU 13

Rais Jakaya Kikwete akisikiliza taarifa ya Mbwa mwitu kutoka kwa watafiti wa Tawiri katika eneo la Nyansirori ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti,kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi,Dc Serengeti Ally Mafutah,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri Dk Saimoni Mduma.
Rais Kikwete akijadiliana na viongozi wa Tanapa
Mkurugenzi Mtendaji wa Grumet Fund Dk Tim Tear akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kuachilia mbwa mwitu 13,kampuni hiyo ni miongoni mwa zilizofadhili mradi huo unaolenga kuongeza wayama hao waliokuwa katika hatari ya kutoweka katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Rais Kikwete akiongoza viongozi mbalimbali kuelekea eneo la tukio.
Rais Kikwete akiongoza viongozi mbalimbali wa taasisi za umma na kampuni binafsi kukata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi shughuli za kuachilia mbwa mwitu 13
Utepe ukikatwa
Mnaona wale ,walikuwa katika hatari ya kutoweka tunatakiwa kuwahifadhi ili tusianze kazi ya kuwaagiza nje,anaonekana akisema.
mijadala mbalimbali iliendelea eneo la tukio
Wanatoka ndani ya uzio na kuingia ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti,utawala binafsi.
Wanashuhudia wakitoka kwa zamu
Kila mmoja anafurahia tukio hilo
Wahifadhi wakishuhudia tukio hilo muhimu kwa upande wa utalii
Rais akimpongeza mtu anayewahudumia wanyama hao,
Mara baada ya shughuli kumbukumbu za picha  hupigwa kama inavyoonekana hapo kila mmoja na pozi lake
Ukumbusho ni muhimu
Ninyi ni wadau wa kubwa kwenye mradi huu tuendelee kusaidiana ili kurudisha heshima ya hifadhi hii,anaonekana akisisitiza
Kwa heri na asante sana kwa ufadhili wenu Dr Tim,endeleeni kufadhili sekta ya Uhifadhi na utalii.
Kazeni buti ili tunusuru wanyama hawa

No comments:

Post a Comment