13/12/2013 | Posted by Sitta Tumma |Mara
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina-picha na Journo tourism.
MAENDELEO
duni, uchu wa madaraka, mila potofu na usimamizi mbovu wa sheria kwa wananchi
wanaoishi karibu na hifadhi za taifa, imetajwa kuwa ni kichocheo kikubwa cha
migogoro kati ya Shirika la Umma la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA), na jamii
husika.
Hayo
yalibainishwa juzi na mwezeshaji wa semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari
inayoendelea mjini hapa, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania Audio-Visual and
Communication Management, Charles Kayoka, wakati alipozungumzia chanzo cha
migogoro.
Kayoka
alisema hali hiyo inatakiwa kukomeshwa kwa kila mamlaka husika kuwajibika
ipasavyo katika suala zima la kusogeza huduma karibu za kimaendeleo kwa jamii
yote, ikiwemo inayozunguka hifadhi za taifa.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi huyo, mbali na hayo viongozi wa halmashauri zinazozunguka
maeneo hayo ya hifadhi za taifa, hawana budi kuwajibika katika kuboresha huduma
kwa wananchi wao.
“Migogoro
mingi katika maeneo ya pembezoni mwa hifadhi za taifa, inasababishwa na mfumo
duni wa maendeleo, usimamizi mbovu wa sheria, wanasiasa na mambo mengine kama
vile mila potofu.
“Kwa hali
hii, halmashauri lazima ziwajibike kuhakikisha zinaboresha mfumo bora wa
kiuchumi kwa wananchi wao. Suala hili siyo la TANAPA pekee,” alisema Kayoka.
Alisema
Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikichangia asilimia 17.5 katika fedha
zote zinazopatikana katika pato la taifa, hivyo ni lazima maeneo ya hifadhi
yaheshimiwe kwa mujibu wa sheria za nchi.
Baadhi ya
washiriki wa semina hiyo, waliwalaumu waandishi wa habari kwa kufanya kazi zao
maeneo ya mijini na kushindwa kufika katika maeneo ya vijijini ambako kuna
mahitaji na migogoro mingi.
Mhariri
wa habari wa gazeti la Rai, Masyaga Matinyi pamoja na Naibu Mhariri Mtendaji
gazeti la Jamhuri, Jackton Manyerere, walisema kamwe tatizo la ujangili
halitaisha iwapo serikali haitawajibika kuchukua hatua za kisheria kwa
wanaoonekana kuhusika na hujuma hizo.
No comments:
Post a Comment