Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli akisoma ripoti hiyo bungeni juzi alisema Operesheni Tokomeza Ujangili, ulisababisha hofu miongoni mwa wananchi na viongozi na baadhi yao kuyakimbia makazi.
Posted Jumapili,Decemba22 2013 saa 11:22 AM
Kwa ufupi
Dar es Salaam. Unyama zaidi umebainika katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili baada ya kubainika
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Francis Miti, kukiri kujihifadhi
kwenye hoteli moja nje ya wilaya yake.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, James Lembeli akisoma ripoti hiyo bungeni juzi alisema
Operesheni Tokomeza Ujangili, ulisababisha hofu miongoni mwa wananchi na
viongozi na baadhi yao kuyakimbia makazi. Lembeli alisema watuhumiwa,
walikamatwa, walipekuliwa na kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo.
“Baadhi
ya wananchi wakiwemo viongozi, madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji na
watumishi wa Serikali, walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi
wanaowaongoza,” alisema Lembeli
Aliongeza;
“Watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa
adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao.”
Lembeli
alitoa mfano kuwa Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai
kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko
huku mwanawe wa kiume (11) akishuhudia huku akilazimishwa kuchora picha ya
Chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake.
Alisema
mwanamke mmoja wa Babati (jina tunalo) alidai kuvuliwa nguo na
kulazimishwa kufanya mapenzi na wakwe zake, pia kuingizwa chupa sehemu zake za
siri.
Aidha,
baadhi ya wanawake walidai kubakwa na kulawitiwa huku wilayani Ulanga, mwanamke
mmoja alidai kubakwa na Askari wawili wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya
usiku.
No comments:
Post a Comment