Saturday, December 21, 2013

Soko la asali lawanyima kipato wafugaji nyuki


Na Salim Mohammed,Mwananchi

Posted  Ijumaa,Decemba20  2013  saa 11:3 AM
Kwa ufupi
Msagati alisema kuna baadhi hawana kazi jambo linalowafanya kushinda vijiweni na kupanga kufanya mambo mabaya.
Handeni.Wafugaji nyuki wilayani Handeni mkoani Tanga, wameitaka Serikali kuwapatia soko la kuuzia asali ili waepuke kutapeliwa na walanguzi.
Wamesema kwa kufanya hivyo, watanufaika na zao hilo na kuwaongezea kipato zaidi wanachoshindwa kukufikia kwa sasa.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwa nyakati tofauti, wafugaji hao walisema Serikali imeisahau sekta hiyo na hivyo kuitaka kuitangaza pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji mjini na vijijini pamoja na kuwapatia soko la uhakika.
Walisema kwa sasa hawana soko la uhakika la kuuzia asali yao, hivyo kutegemea mteja mmoja mmoja na walanguzi kutoka nje ya wilaya na mkoa ni jambo linalowanyima kipato.
“Tumefurahi leo waandishi wa habari mmekuja eneo letu, hasa hapa sokoni. Tunashindwa kufahamu soko la uhakika wa bidhaa yetu ya asali, tunaomba mfikishe ujumbe kwa Serikali ili iweze kutusaidia,” alisema Juma Msagati
Msagati alisema kuna baadhi hawana kazi jambo linalowafanya kushinda vijiweni na kupanga kufanya mambo mabaya.
“Tunataka Serikali ilete wataalamu kutoa elimu kwa vijana ili waweze kushiriki katika kazi za ufugaji wa nyuki,” alisema Msagati. Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mkazi wa Misima, Khalid Gharib alisema Wilaya ya Handeni ina misitu mikubwa ambayo imekuwa ikitumiwa na wafugaji wa nyuki, lakini wamekata tamaa baada ya kukosa soko

No comments:

Post a Comment