Na Kelvin
Matandiko, Mwananchi
Posted Alhamisi,Decemba12 2013 saa 10:4 AM
Kwa ufupi
“Naamini
Kamati zote za mizitu katika vijiji tutafanikiwa kuondoa changamoto hiyo,”
alisema na kwamba wanasiasa wanaingilia utendaji wao.
Dar es
Salaam. Ripoti
imebaini mapato yanayokadiriwa kufikia Sh6.8 bilioni yamekuwa yakipotea kila
mwaka, kutokana na ukusanyaji mdogo wa mirabaha na usimamizi mbovu wa leseni za
uvunaji misitu nchini.
Ripoti
hiyo iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mwaka 2013, imebainisha
hasara hiyo kupitia uwiano wa uvunaji haramu misitu inayokadiriwa kufikia hekta
400,000 za misitu kukatwa kila mwaka.
Kauli
hiyo ilitolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS), Nurdin Chamuya wakati wa uzinduzi wa tangazo la uhamasishaji wa kuzuia
ukataji misitu ovyo nchini.
Chamuya
alisema licha ya juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali, ukataji wa
misitu umezidi kuongezeka kwa kasi.
“Naamini
Kamati zote za mizitu katika vijiji tutafanikiwa kuondoa changamoto hiyo,”
alisema na kwamba wanasiasa wanaingilia utendaji wao.
harakati
za kuondoa changamoto hiyo, Afisa mwandamizi wa misitu, jumuiko la maliasili
Tanzania(TNRF),Cassian Sianga alisema changamoto hiyo imekuwa mwiba kwa kipindi
kirefu na kwamba wameaanda mfumo mpya utakaosaidia kukabiliana na tatizo hilo.
Baadhi ya
maeneo nchini yanadaiwa kukingiwa kifua na viongozi wa kisiasa pale wanapokutwa
wakikata misitu ovyo hatua inayoathiri harakati hizo kwa
“Mpaka
sasa tunapigania ujenzi wa sekta binafsi ili kuhakikisha wafanyabiashara
wanasimamia na kushughulikia changamoto zinazowakabili, mpaka sasa kuna
wafanyabiashara kutoka mikoa 13 imeshaanza kuandaa Katiba,” alisema Sianga.
No comments:
Post a Comment