Thursday, December 12, 2013

Serikali yajipanga kukuza utalii

``
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Kaghasheki.picha na Journo Tourism
Na Peter Saramba, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Decemba12  2013 

Kwa ufupi
Akizungumza juzi jijini Arusha wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Chama Cha Wafanyabiashara wa Utalii nchini (Tato), Balozi Kaghasheki alisema ni lengo la Serikali kuongeza idadi ya watalii kutoka milioni moja mwaka huu mpaka kufikia watalii 1.5 milioni kufikia mwakani.
Arusha.Serikali inakusudia kupitia upya sheria na kanuni za kodi pamoja na mazingira yote ya biashara katika sekta ya utalii kwa lengo la kuwaondolea kero wadau wa sekta hiyo ili kuongeza mchango wake katika pato la taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi Kaghasheki alisema ili kufikia lengo hilo, Serikali itakuwa ikifanya vikao vya kila robo mwaka na wadau wa sekta hiyo kujadili changamoto zinazowakabili na njia za kuyakabili.
Akizungumza juzi jijini Arusha wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Chama Cha Wafanyabiashara wa Utalii nchini (Tato), Balozi Kaghasheki alisema ni lengo la Serikali kuongeza idadi ya watalii kutoka milioni moja mwaka huu mpaka kufikia watalii 1.5 milioni kufikia mwakani.
“Tanzania ni nchi ya pili kwa kwa na vivutio vingi vya utalii duniani baada ya nchi ya Brazil,” alisema Kaghashekil.
Aliongeza: “Lakini ni ya 114 kwa utoaji huduma za kitalii. Lazima tujiulize nini kifanyike ili tungoze katika sekta hiyo muhimu,” alisema Kaghasheki

No comments:

Post a Comment