Na Raymond
Kaminyoge, Mwananchi
Posted Jumatatu,Decemba23 2013
Kwa ufupi
- Kauli hiyo, imekuja baada ya
ripoti iliyosomwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ambayo imesababisha Rais
Jakaya Kikwete kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Dar es
Salaam.
Jeshi la Polisi, limekiri kutikiswa na ripoti ya Operesheni Tokomeza
Ujangili ambayo imemkumba Waziri wake wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi.
Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mungulu alisema jana kwamba operesheni
hiyo imelitikisa jeshi hilo kutokana na madhara yaliyojitokeza wakati wa
utekelezaji wake.
“Lengo la
operesheni hiyo halikuwa kuleta madhara kwa wananchi, yaliyotokea ni changamoto
kwa Polisi na sasa ni kujipanga upya ili haya yasije kutokea tena,” alisema na
aliongeza: “Kwa sasa tunaziachia mamlaka husika ziendelee kulishughulikia suala
hili kwa sababu limehusisha idara mbalimbali za Serikali.”
Kauli
hiyo, imekuja baada ya ripoti iliyosomwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ambayo
imesababisha Rais Jakaya Kikwete kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Kauli
hiyo, imekuja baada ya ripoti iliyosomwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ambayo
imesababisha Rais Jakaya Kikwete kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Mapema
Novemba, mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliunda Kamati ya Bunge ya
Maliasili, Ardhi na Mazingira kuchunguza utekelezaji wa Operesheni Tokomeza
Ujangili baada ya kutokea mjadala mkali bungeni kuhusu kadhia waliyopata
wananchi.
Katika
mjadala huo, wabunge walilalamikia watekelezaji wake wakisema ilitawaliwa na
mateso kwani waliokuwa wakiiendesha walikuwa wakiwatesa wananchi na hata
kusababisha vifo na majeruhi.
Taasisi
zilizokuwa zikiendesha operesheni hiyo kabla ya kusitishwa ni; Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi.
Kuzinduliwa kwa operesheni hiyo kulikuwa na
lengo la kulinda rasilimali za nchi hasa tembo ambao katika siku za hivi
karibuni wamekuwa wakiuawa kwa kasi na majangili kwa ajili ya pembe za ndovu
No comments:
Post a Comment