Thursday, December 19, 2013
Kamati ya Lembeli kuwasilisha kesho
Posted Alhamisi,Decemba19 2013
Kwa ufupi
Kamati yajifungia hotelini huku hofu ikitanda kuwa huenda ikawang’oa baadhi ya mawaziri
Dodoma. Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili inayoongozwa na James Lembeli, inatarajiwa kuwasilisha taarifa yake Ijumaa siku ambayo Mkutano wa 14 wa Bunge utamaliza shughuli zake.
Taarifa zilizopatikana bungeni jana, zilisema kuna uwezekano kamati hiyo ikatumia nafasi hiyo kuwasilisha taarifa ya kamati yake ndogo iliyochunguza mwenendo wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Hata hivyo, kumekuwa na wasiwasi kuwa ripoti hiyo inaweza kutowasilishwa bungeni hasa kutokana na mambo mazito yanayotarajiwa kuibuliwa yanayoweza kusababisha baadhi ya mawaziri kung’olewa.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa wajumbe wa kamati hiyo ndogo ya uchunguzi ya Kamati ya Bunge la Ardhi, Mazingira na Maliasili imejichimbia Hoteli ya St. Gasper ikikamilisha ripoti yake. Kamati hiyo imezua hofu kubwa ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo zinazotarajiwa kuguswa na ripoti hiyo.
Ni ripoti kama hii inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni Ijumaa ndiyo iliyomng’oa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige kutokana na kashfa ya ugawaji vitalu vya uwindaji. Tayari, Kamati ya Lembeli iliyoanza kazi Novemba 25 imekamilisha kazi ya kuhoji watu mbalimbali, wakiwamo mawaziri watatu ambao wizara zao zilihusika moja kwa moja na operesheni hiyo.
Mawaziri waliohojiwa katika Hoteli ya Bahari Beach Dar Es Salaam ni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.
Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alipoulizwa jana alisema hana uhakika ila upo uwezekano wa ripoti hiyo ikawasilishwa Ijumaa.
sambamba na taarifa ya kamati mama ingawa hakuwa na uhakika. Miongoni mwa wanadaiwa huenda ripoti hiyo ikawang’oa ni Dk Mathayo na naibu wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment