Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Posted Ijumaa,Novemba15 2013
Posted Ijumaa,Novemba15 2013
Kwa ufupi
Maofisa waliotiwa nguvuni ni Mohamed Hija Mashaka na Omar Hamad Omar
wote ni maofisa wa TRA kituo cha Bandari Malindi mjini Unguja wenye dhamana ya
uhakiki na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi.
Zanzibar. Maofisa wawili waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar
wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakihusishwa na mtandao wa usafirishaji wa
magendo ya meno ya tembo yaliyokamatwa Bandari ya Malindi, Zanzibar.
Kukamatwa kwa watu hao kunafanya idadi yao kufikia wanne.
Akizungumza na gazeti hili, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa
Ali Mussa alisema maafisa hao wamekamatwa na watafunguliwa mashtaka yao Tanzania
Bara kutokana na Zanzibar kutokuwa na Sheria ya Nyara za Serikali.
Maofisa waliotiwa nguvuni ni Mohamed Hija Mashaka na Omar Hamad Omar
wote ni maofisa wa TRA kituo cha Bandari Malindi mjini Unguja wenye dhamana ya
uhakiki na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi.
“Watafunguliwa mashkata Bara kwa vile Zanzibar hakuna sheria ya nyara za
Serikali,” alisema Mussa na kuongeza uchunguzi bado unaendelea.
Hata hivyo, alisema kampuni iliyokuwa ikisafirisha mzigo huo ya Island
Sea Shells imebainika kuwa haina ofisi na wala anuani zake hazifahamiki.
“Tumefuatilia kwa Msajili wa Kampuni Zanzibar, hatukuona jina la kama
hilo,” alisema Kamanda Mussa.
“Hii ni kampuni ya mifukoni (briefcase company), ingawa kuna majina ya
watu waliosajili kampuni hiyo.”
No comments:
Post a Comment